Jamani hili swali majibu yake yameshindikana kabisa kupatikana humu jukwaani, lol?
Ninajaribu kuigiza statement ya ma-afande wangu jeshini. Ilikuwa tukifanya makosa wanaamua kutupa adhabu wanasema "kunja ngumi", yaani upige push-up zile za kutumia ngumi. Sasa afande akishasema kwa mara ya kwanza, mnakuwa manjiishauri shauri kidogo huku mkimwangalia usoni kwamba labda anaweza akabadilisha uamuzi na kuwasamehe. Mkiwa bado katika hali hiyo ya kujishauri shauri, halafu na yeye kumbe hana mpango wa kuwasemehe, mtamsikia anarudia tena kwa kusema "hivi hili zoezi la kukunja ngumi limeshindikana kabisa".
Akishasema hivyo ndiyo hapo mnagundua kuwa kumbe hana mpango wa kusamehe, inabidi wote mkunje nguni