Cake bila oven

masai dada

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
15,678
12,348
Ni ya vanilla na maziwa nimeipika kwa gesi tu.
Nimetumia
Unga:250g
Sukari (icing suga):200g
Mayai:5
Maziwa:vijiko vitatu vya chai
Vanilla:kifuniko kimoja
Butter:250g
Baking powder:2teaspoon


Ukianza kumix kama huna mashine ya kumixia tumia ya mkono ila koroga kweli kweli na haraka haraka.
Stage ya kwanz
Chukua unga na baking powder chekecha mara kama 2 .inasaidia kuondoa chenga na pia kutawanyisha unga kama una mabonge
Alafu uweke pembeni
Stage ya pili
Anza kuweka butter kwenye bakuli la kukorogea weka na sukari koroga mpaka ianze kuwa nyeupe laini
Stage ya 3
Weka mayai anza na moja moja uku ukikoroga yaani yai zima
Stage ya nne
Anza kutia unga kidogo kidogo uku ukikoroga
Mwisho weka vanilla
Usirembe sana
Harakisha maana ukiuacha sana mchanganyiko unaharibika
Chukua sufuria nzito weka kwenye gesi yako moto wa chini
Ndani ya sufuria weka chuma ya kukalishia kama huna weka kile cha kwenye gesi
Kiokeo chako kiwe kimepakwa mafuta naunga kidogo
Mimina mchananyiko wako
Weka kwenye sufuria uliyoiweka jikoni funika na mfuniko mzito alafu unaweka kitaulo kwa juu
Moto uwe mdogo na usigunue mpka 40mints kuangalia
Chomeka stick kama kikitoka kikavu imeiva
Usiwe na haraka

20200829_175352.jpg
20200829_175851.jpg
20200830_200622.jpg
20200830_200604.jpg
 
Yummy Yummy, Ahsante sana kwa maujuzi haya, keki inaonesha tamu na laini,

Mimi natumia jiko la kuni je unanishauri nipike vipi?
 
Back
Top Bottom