CAG Report yaonesha madudu NSSF; Vipi PPF

mchukiaufisadi

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
546
193
Nimesoma kwa haraka haraka ripoti ya CAG ya mashirika umma. Naandaa uchambuzi yakinifu nitauleta next week.

Kwa huo uharaka nimegundua kuwa NSSF imetajwa sana kwenye mapungufu mengi lakini PPF kimya. Hii ni ishara kuwa either CAG si mwaminifu au aliowatuma sio waaminifu.

Katika ripoti yake amekua either ni mbaguzi au hakuletewa taarifa sahihi juu ubadhirifu na udanganyifu uliopo PPF

1.Kuhusu UDOM, hata PPF wana mikataba kama ya NSSF. Majengo ya PPF ndio mabovu kupita yote, kama alivyo yashtukia Mwandosya juzi.

2 PPF wamekikopesha kiwanda cha Kagera Sugar, miaka inapita hakuna dalili za kulipwa, CAG kimya!!!!!!!!!!!

3. PPF wana shares TOL na TATEPA hadi leo hakuna dividend, CAG kimyaaa!!!

4 PPF wakurugenzi hununua kwa mkopo mashangingi ya milioni mia hamsini, kodi yake hulipiwa na PPF kila baada ya miaka mitatu mengine..CAG Kimyaa!!!!!!!!!!!! Kodi not less than 60milion kwa mkurugenzi mmoja na wapo tisa

5 PPF Wakurugenzi hulipwa Pension, gratuity na Group endowment kinyume na sheria za utumishi wa umma.. CAG Kimya!!!!!!!!! Waziri wa utumishi alisisitiza kwa walio kwenye mikataba walipwe gratuity tu.

6 PPF mishahara ya wakurugenzi kupanda kila mwaka kwa 25% wakati watumishi wengine hawapandishiwi.. CAG Kimyaaaa!!!!

7 PPF vibarua kufanyishwa kazi zaidi ya miaka minne, watoto wa wakubwa hupewa ajira baada ya miezi mitatu.. Temporary work gani huwa mtu yuleyule miaka mitatu hadi minne? Kila miezi mitatu new contract. CAG kimyaa!!! Wizara ya kazi mnajua hili?

8 PPF haijakusanya madeni ya pango (rent) zaidi ya bilioni 1 lakini CAG kimyaa!!!!!

9 PPF haikufuata taratibu za manunuzi kwenye tenda za UDOM, PPF waliilipa kampuni ya Photo Medica 40 milioni, nashangaa CAG analipoti 2milioni za NDC, CAG vipi?????????

10 PPF Mkrugenzi wa Fedha alijiuzia viwanja vinne kwa mpigo kwa 16milion tu wakati vilinunuliwa kwa 56milion (1996) value for money iko wapi!!! Kufunika kombe, akammegea viwili Chief Internal Auditor, wakashusha maghorofa bahari Beach...CAG huoni tu???????????

11 Wakurugenzi wamejilipa 220milioni, na Mkurugenzi mkuu 520milion isivyo halali, CAG kimyaa!!!!!!!!!! HATI SAFI.

12 PPF Wafanyakazi wananyanyaswa , wanatukanwa na wakurugenzi, wanadhurumiwa haki, marupurupu yote yako kwa wakurugenzi, na mameneja. CAG kimyaaaa!!!


ZITTO AMEAGIZA CAG ARUDIE AUDIT YA GROUP ENDOWMENT 2008. Zitto aandike maumivu. TAKUKURU walijidai kulifanyia kazi, wakapewa chao na kuondoka. Hadi leo hii kimya itakuwa CAG asiye na meno?



Haya ngoja niazie hapa na wengine mchangie. Nitaleta uchambuzi mzuri next week. Sasa hivi masikio yote yako kwenye katiba na kuvuana nguo or sorry ni magamba.
 
mwelekeo wa thread hii kwa ilivyowasilishwa ni chuki tupu!! ebu eleza kwanza masilahi yako na PPF ndipo tujadili hili kwa haki.
 
mwelekeo wa thread hii kwa ilivyowasilishwa ni chuki tupu!! ebu eleza kwanza masilahi yako na PPF ndipo tujadili hili kwa haki.

hakuna chuki, huyu ametoa hata data TO SUBSTANTIATE HIS CLAIMS, wewe unataka nini tena. Kuwa realistic, kama kuna ndugu yako au wewe UNA/ananufaika na ufisadi wa PPF, we nyamaza watu waseme kama itasaidia. How come mtu anaweka hela yake PPF for decades anastaafu anapata 5 MTsh wakati mkurugenzi anapata 500 M Tsh baada ya miaka mitatu. TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Mwanalugali.

Pole sana kama utajadili hoja kwa kuangalia maslahi yangu. Angalia maslahi ya PPF, wanachama wa PPF, Umma wa watanzania na serikali kwa ujumla.

Mimi ni mwanachama wa PPF nachangia 10% ya mshahara wangu kila mwezi na mwajiri wangu ananichangia 10%. Haya ndiyo maslahi yangu, endelea sasa kuchangia kama unacho cha kuchangia.

Kama huna au hujui chochote kaa kimya.




mwelekeo wa thread hii kwa ilivyowasilishwa ni chuki tupu!! ebu eleza kwanza masilahi yako na PPF ndipo tujadili hili kwa haki.
 
Yale yaleeee!!! Jamani hivi SSRA iko wapi? Au haijaanza kazi mpaka leo?
 
Huyo ndio Bwana Ludovick Utuoh..pasco anakwambia ni mtu makini sana katika serikali ya Tanzania

Ukweli tunajua the man is bogus tena ubogus wake unaanzia kwenye hiyo kazi yake mpaka kwenye kuwasilisha ripoti yake
 
Nisichoelewa ni kuwa hakuna ambacho Utouh amekisema leo ambacho hakikusema mwaka jana, mwaka juzi au mwaka wa majuzi! Nisichokielewa ni kuwa kwanini hadi hivi sasa hajajiuzulu!? Haiwezekeni awe anarudia vitu vile vile kwa watu wale wale, na kwa maneno yale yale halafu anatuambia tusubiri ripoti nyingine mwakani. Hata mazingaombwe huwa yana tricks mpya!!
 
Nisichoelewa ni kuwa hakuna ambacho Utouh amekisema leo ambacho hakikusema mwaka jana, mwaka juzi au mwaka wa majuzi! Nisichokielewa ni kuwa kwanini hadi hivi sasa hajajiuzulu!? Haiwezekeni awe anarudia vitu vile vile kwa watu wale wale, na kwa maneno yale yale halafu anatuambia tusubiri ripoti nyingine mwakani. Hata mazingaombwe huwa yana tricks mpya!!

sasa subiri PASCO aje akusome

maana in Pacos's eyes this old idiot cant do wrong japo mwaka jana aliandika ripoti bila kufanya EXIT MEETING
 
Back
Top Bottom