Ndugu wana jamvi, kwa taarifa nilizozipata toka kwa wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma, wamefurahia sana namna ambavyo CAG na Katibu kiongozi walivyoumbuliwa na kamati teule ya bunge.
Furaha hii ya wanaudom inadaiwa ni kutokana na kuthibitishwa kwa hisia zao kuwa ukaguzi uliofanywa na CAG hapo UDOM katika kipindi cha mgomo wa wahadhiri ulilenga kuficha ukweli ndio maana CAG alitanganza kutoona ubadhirifu wowote.
Mambo yanayosababisha wanajumuiya hiyo wakose imani na CAG pamoja na Katibu kiongozi ni kutolewa kwa salary slip mbili tofauti kwa mtumishi mmoja na zote zina mishahara miwili tofauti hii kwa baadhi ya watumishi limefanyika kwa zaidi ya miaka miwili na ushahidi upo kabisa wa salary slip hizi.
Salary slip moja ni ya kutoka hazina ambayo inamshahara sahihi(mkubwa) na nyingine ni ya Udom yenye mshahara wanaojua wao(sio sahihi). katika hili pia wanajumuiya walijiuliza je uongozi wa chuo ulitumia utaratibu gani kubadilisha mishahara ya watumishi kwani hata watu wa hazina walipohojiwa juu ya hili walionekana kushangaa na kuonekana kuutambua mshahara unaotoka hazina pasipo mashaka yeyote, lakini huyu CAG hakuona tatizo lolote.
Matokeo ya kuwepo kwa salary slip mbili kumewafanya wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma kulipwa kwa kiwango cha chini tofauti na vyuo vingine vya umma. Ushahidi upo wazi, kwani mhadhiri msaidizi wa Udom(anayeanza bila kujali uzoefu PUTS 13) analipwa sawa na mkufunzi msaidizi wa chuo kingine cha uma(tutorial assistant) -angalia OUT AU UDSM
Jambo jingine linalojitokeza katika kuwepo kwa salary slip mbili ni je baada ya kuwa kata mshahara hawa wafanyakazi wa udom hicho kinachokatwa kinaenda wapi wapi?
Katika mateso yanayowakabili wafanyakazi wa UDOM imebainika kuwa katibu mkuu kiongozi ana mkono wake. Hili linadaiwa ni kutokana na mahusiano yake na makamu mkuu wa chuo ndugu Kikula hawa wote wanatokea sehemu moja huko Iringa(ukanda na ukabila). Kutokana na mahusiano haya ya karibu inadaiwa kuwa katibu mkuu kiongozi alitoa maelekezo ambayo si sahihi ya namna ambavyo ukaguzi wa kubaini ubadhirifu udom ufanyike. Matokeo yake ni kutoa mwanya wa ofisi ya fedha na utawala ya ndg Mlacha kuonekana kuwa ni safi. Kwani inadhaniwa kwamba isingekuwa rahisi kwa mlacha kuwa mchafu na kikula kawa msafi tumia mfano wa jairo na ngeleja.
Katika kutangazwa kuwa hakuna kosa lolote Pinda alionekana pia kudharirishwa(huenda ya bungeni kuhusu jairo ni ya pili) kwani alipokuja kutatua mgogoro wa wahadhiri aliwahakikishia wanajumuiya kuwa suala la Mlacha ni suala la muda. Kutokana na hali hii tunaona kwamba tabia ya katibu kiongozi kulinda au kujihusisha na ufisadi ni suala ambalo amebobea na matokeo yake ni kuidhalilisha serikali hii ya ccm.
Katika nsakata la udom, Huenda kutokana na madudu ya CAG na katibu kiongozi(mtazamo wangu) imesababisha kuleta hisia kwamba huenda mheshimiwa raisi anajikuta analinda mafisadi kwa kigezo cha udini( hoja iliyatawala kipindi fulani miongoni mwa wanajumuiya kwamba Mlacha anaandamwa kwa sababu ya dini yake), Kutokana na kazi nzuri ya kamati teule hata kwa baadhi ya waislamu wameanza kuona namna ambavyo dini yao nzuri inavyotumika kama kichaka cha kufichia mafisadi na watendaji wenye kiburi cha ajabu.
Hivyo basi wanajumuiya ya UDOM wananaiomba kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma kuipitia vema ripoti ya CAG ili kubaini ufusadi wake. CAG na Luhanjo dhambi ya UDOM imewaumbua! Ninawasilisha
Nikiangalia kwenye hayo maandishi, suala hilo sio la UDOM pekee, ni la vyuo vyote vya umma. Kuwepo kwa salary slip mbili kuna sababu zifuatazo. 1. Hazina hutoa salary slip yenye kuonyesha Basic salary na stahili zingine zinazolipwa na serikali moja kwa moja pasipo makato ya aina yoyote. Pesa zinapofika chuo inabidi chuo husika kiandae salary slip nyingine itakayoonyesha makato stahiki kwa mfanyakazi husika, makato kama ya PAYEE,NHIF, NSSF/PPF/LAPF, Michango ya hiari katika vyuo husika kama vile mfuko wa mazishi, SACCOS. contributions kwenye vyama vya kitaaluma (UDASA, UDOMASA n.k). Makato haya hayafanyi kutoka hazina, ni lazima yafanywe na vyuo husika. Kwa hiyo Net Pay kwenye Salary Slip ya hazina haiwezi kuwa sawa na Net Pay kwenye Salary slip ya chuo kwa sababu hazina hawafanyi makato ya aina yoyote. Pia kuna malipo ambayo chuo kinayafanya kutokana na OC, malipo kama ya house allowance, ambayo kwenye Slip ya hazina hayawezi kuoneka.
Isipokuwa, kama Basic salary inayotoka hazina na Basic salary inayolipwa na chuo zinatofautiana, hapa ndio kutakuwa na tatizo la kujiuliza ni kwa nini zitofautiane.
Kwa hiyo hoja nadhani siyo kuwepo kwa Salary slip mbili kwa sababu hiyo haikwepeki. Hoja ni ikiwa kuna tofauti ya Basic Salary katika slip zote mbili, then kutakuwa na tatizo la msingi la kushughulikia.