CAG akamilisha ukaguzi Udom

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
CAG akamilisha ukaguzi Udom Tuesday, 01 February 2011 21:12

Sadick Mtulya
TIMU ya wakaguzi kutoka ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), imekamilisha ukaguzi wa fedha katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Ukaguzi huo ulifanyika kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutaka CAG kufika Udom na kukagua kitengo cha fedha chuoni baada ya kulalamikiwa na wanafunzi pamoja na wahadhiri kuwa mmoja wa viongozi chuoni hapo amekuwa akitafuna fedha zao.

Mkaguzi huyo alipewa muda wa wiki ili awe amekamilisha na kutoa taarifa ya kile atakachobaini ili kuondoa utata huo.

Juzi jijini Dar es Salaam, CAG Ludovick Utouh aliliambia Mwananchi kuwa ukaguzi umekamilika na kwamba anatarajia kukutana na menejimenti ya chuo hicho wiki hii kabla ya kumkabidhi Pinda, ripoti ya uchunguzi huo.

“Kazi ya ukaguzi si ya kuwindana, kiutaratibu unapomaliza ukaguzi unakutana na wahusika na kuwaeleza mlichokipata katika ukaguzi na kisha unawasilisha ripoti kwa mhusika aliyekuagiza,’’ alisema Utouh.

Akaongeza: “Kiufupi timu yangu ya ukaguzi imemaliza kazi yake Udom, na wiki hii tutakutana na menejimenti ya chuo na kisha tutakabidhi ripoti kwa aliyetutuma kufanya kazi hii(Waziri Mkuu).’’

Kabla ya kuanza kwa ukaguzi huo Januari 18, mwaka huu, Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Idrisa Kikula alinukuliwa akisema katika mawasiliano baina yake na CAG, alimwambia kuwa vijana wake walipitia Hazina, na baadaye Bodi ya Mikopo kabla ya kupitia tena Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kuingia Udom.

Akiwa Chuoni hapo Pinda alisema kuwa kitengo cha utawala na fedha chuoni hapo kinatiliwa shaka kubwa kutokana na Hazina kuonyesha baadhi ya fedha za malipo kwa watumishi, lakini cha ajabu fedha hizo hazijawafikia watumishi hao.

Malalamiko makubwa kwa watumishi hao ni kwa kiongozi wa Kitengo hicho ambaye siku hiyo wahadhiri walimtaka Waziri Mkuu kuondoka naye kwa madai kuwa hawamtaki.

Pinda aliwataka watumishi kuwa wavumilivu akisema kuwa hawezi kuondoka naye kwani alipaswa kukaguliwa na kujibu baadhi ya maswali yatakayomhusu katika kazi ya ukaguzi huo.


 
Ukiona hiyo taarifa haipendekezi Porofesa kikula kuachia ngazi basi ujue kuwa CAG anafanyakazi ya kutoa majibu ya kisiasa kwa matatizo ya kitaalamu...........................
 
Back
Top Bottom