Cadillac kuingia Formula 1 GP kuanzia msimu ujao wa 2026. Kwa kuanza, watatumia engine za Ferrari.

Cadillac kuingia Formula 1 GP kuanzia msimu ujao wa 2026. Kwa kuanza, watatumia engine za Ferrari.

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,139
Reaction score
88,800
Wazee, kuna hii habari nzuri kwa wapenzi wa Formula 1.

IMG_2058.jpeg


Tumezoea kuona team 10 kwenye F1 Grand Prix, ila kuanzia mwakani 2026 zitakua 11 ikiongezeka ya Cadillac, ilio chini ya General Motors (GM), Ila watatumia power unit na gearbox kutoka kwa Ferrari.

IMG_2055.png


Habari nzuri haijaishia hapa, ila ni madereva waliowasign. Hapa ndio pazuri. Valtteri Bottas na Sergio Perez.

Hawa ni moja ya experienced drivers kwenye F1, tatizo ni team walizokua wanaendesha wakawa shadow-banned.

IMG_2056.jpeg


Mfano, Bottas (mwamba huyo hapo juu) alikua Mercedes tokea 2017 ila kukawa na Lewis Hamilton. Hii ilipelekea Bottas kutoonekana kabisa juhudi zake na kuna tetesi kua gari lake lilikua detuned ukifananisha na la Hamilton.

IMG_2057.jpeg


Perez (hapo juu) nae alianza Red Bull tokea 2021 tatizo kukawa na Max Verstappen kama dereva mwenzie. Yes, the rest is history.
IMG_2059.jpeg


Utajiuliza Kwanini Cadillac wamewasign hawa jamaa, ila naamini lengo kubwa ni kuwasign watu wenye experience kubwa sana kwenye circuit ili wajenge foundation nzuri kabla hawajaanza kuwaleta rookies.

Ni jambo la furaha kuwaona hawa jamaa kwenye F1 tena.
 
Wazungu wenzetu wanabuni maendeleo kilasiku...
Hao madereva wanasajiliwa kama wachezaji mpira kitu ambacho ni faida Kwa timu wanazofanyia kazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom