CACHE ni nini?

CACHE ni nini?

Cache ni temporary storage.. huifadhi data kwa muda mfupi ili kurahisisha accessibility ya vitu mbalimbali katika PC/Micro computers/phones..
Cache inaweza sababisha device kuwa nzito kama simu ina run out of the memory.. Coz simu inahtaj a certain memory ili ku increase speed ya simu yako.. Sasa once memory ikiwa imejaaa cache inashindwa ku ji adjust/increase kwa hyo uwezo wa device ku access a certain data inakua kaz kidogo leading to uchelewashaj wa data loading. Kwa mfano unaweza fungua app ikakaa kidogo then ndio ikafunguka
 
Hizi ni data ambazo kifaa chako huifadhi kama kumbukumbu ya matumizi yako ili kukupa huduma faster pale utakaporudia process ile ya mwanzo. Chukua mfano wa Web Cache; unapotembelea tovuti kwa mara ya kwanza inaweza kuchukua muda kidogo kuload lakini baadae ukifungu tovuti ile ile load speed yake inakua haraka sana. Cache zipo aina tofauti kuna CPU cache, Web Cache n.k..lakini zote zinafanya kazi sawa kusave muda na bandwidth.
Yees
 
CACHE ni aina ya memory yenye speed kubwa sana inayopatikana kwenye hardware mfano processor au application. Hiyo memory kazi yake ni kuhifadhi address ya vitu ulivyovifanya kwenye hardware yako au application. Mfano case yako wewe ni ya application kwa hiyo application ina handle hiyo cache ili utakapotafuta kitu ulichokifanya/peruzi ijisearch automatically kwenye hiyo cashe halafu ikija hiyo tovuti we una iclick una endelea moja kwa moja tofauti na kama haingekuwepo wewe ungelazimika kuandika address nzima ya mtandao unaotembelea.

Hivyo hivyo simu au computer inapata msaada pale unapo search kitu ulichokifanya.

Faida ya cache technology ni kwamba ina speed up computing.
 
Umewahi kujaza form yeyote kwenye tovuti? Wengi watasema ndiyo maana ata ku-login hapa JF lazima ujaze form yenye username na password.. Pale unapofanya hivi browser(Chrome, Edge, Opera) itakuomba ruhusa ya kukumbuka password na username, baadae utakapofungua ile website utaona username na password yako ziko pale kwenye form zikiwa highlighted kwa rangi ya njano.
Hivyo basi cookies hutumika na tovuti kukumbuka taarifa muhimu za watembeleaji wa tovuti husika iwe ni majina, passwords, shopping cart customization.
Kuna tofauti gani kati ya cookies na cache files??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom