bcsolution
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 394
- 177
- Thread starter
-
- #41
Kumbe kushusha gharama ile mwanzo walipoanza na maofa tele ilikuwa kuwavutia watu ili wajazane kisha wamalize kama ule mtego wa tenga unaweka na chupa ya soda shingoni unaifunga kamba ndani unamwagia mtama njiwa wakishaingia unavuta kamba tenga linashuka, mateka kibao.
Kweli biashara mbinu
Ila wamesahau tenga lao bovu...tumetoka tehe tehe tehe
nimekuwa nikijiunga kifurushi cha 15000 kila mwezi . Sasa tigo wamekiondoa kwenye menu yangu sasa kuna cha 50.000 na cha 100.000 . Nimewapigia kuwauliza mbona sioni kifurushi cha 15000 ,nikaambiwa kimeondolewa kwangu kwa kuwa nimeonekana najiunga nacho sana .. Kwa iyo nimeonekana tajiri sana ...airtel nakuja kwenu nipokeeni..bye bye tigo
sijaona malalamiko ya airtel je wako safi ? Mwenye kutumia vifurushi vya airtel atupe data pls...
Mkuu kwani dar ndo kuna watanzania tuu ? huduma zao mbovu plus majanga..
Maanake vyote havinisaidii mi mimi mtanzania masikini...nazidi kuwa masikini. Vinawasaidia wachache..
Nimekuwa nikijiunga kifurushi cha 15000 kila mwezi . Sasa tigo wamekiondoa kwenye menu yangu sasa kuna cha 50.000 na cha 100.000 . Nimewapigia kuwauliza mbona sioni kifurushi cha 15000 ,nikaambiwa kimeondolewa kwangu kwa kuwa nimeonekana najiunga nacho sana .. kwa iyo nimeonekana tajiri sana ...Airtel nakuja kwenu nipokeeni..bye bye tigo
du...! kumbe tigo ni OVYO...!
Kinachoniuma sana hiki kifurushi wamekiondoa kimya kimya...na hawasemi kwenye matangazo yao.. Hapa hata mimi watakuwa wamenipoteza...elfu 50 ya lazima hiyo ngumu sana
huwa nawatania(tigo) kwa kuwaita ma-buzi(buzz)..wanachuna hao balaaaa.,..