Halotel wameninyang'anya Line ikiwa inatumika

Raia Mtata

JF-Expert Member
Feb 4, 2017
315
594
Habari wanajukwaa

Kwa masikitiko napenda kuelezea kitu kilichonitokea Tarehe 11 Nov 2021. Tokea huduma ya mitandao kuanza nimekuwa mteja wa Tigo, Airtel na Vodacom. Sasa nikaamua kutafuta Line spesho ya Haloteli nikaiweka kwenye smart yangu kubwa, ikawa hewani 24 hours.

Kilichonishangaza Tarehe 11 nikapata notification inayosema SIM not provisioned, kufuatilia nikaambiwa hiyo namba imefutwa. Wakati jana yake tarehe 10 Nov nilipigiwa simu na rafiki yangu na ushahidi upo. Nikaamua kupiga customer care kwa kutumia simu ya mtu mwingine nikajibiwa namba yangu ipo hamna atakayeichukua, sasa Leo nimeenda customer care najibiwa eti namba yangu imefutwa kwakuwa haikutumika siku 90, na pia hiyo namba imetumiwa na watu zaidi ya wanne, naomba kuuliza kwani kutumika kwa line ya simu maana yake nini?

Maana mimi sijawahi kuitoa hiyo line kwenye simu, na pia naweka vocha mara chache chache, na nikiwa sina kifurushi nafungua free basics ya haloteli natumia na pia watu wananipigia kupitia hiyo namba, Je naomba kuuliza hayo yote sio Matumizi?

Na pia naomba kuuliza Haloteli wanatoa namba moja kwa mtu zaidi ya mmoja? Kama ni kweli usalama wa Privacy zetu upo kweli? Naombeni ushauri kwenye kesi kama hii nianzie wapi? Maana ni siku 3 za nyuma hiyo line nimetumia.

Nimekuwa disappointed sana na Haloteli.

=====

Ili kujua namna ya data uliotumia fuata muongozo huu Jua namna ya kufahamu kiasi cha MB ulichotumia kwenye kifaa chako
 
Halafu hivi ukisharenew line,mfano nikirenew line ya HALOTEL wanaifungua baada ya muda Gani ? YAANI inaanza kufanya kazi baada ya muda Gani ?
 
Back
Top Bottom