Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Kada wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa zamani wa jimbo la Kilwa Kusini Selemani Saidi Bungara (Bwege) amesema anaamini kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiko sahihi kusimamia 'No Reforms, No Election' na kwamba vyama vyote vya upinzani nchini ikiwemo chama chake ilipaswa waungane pamoja 'kususia' uchaguzi wa mwaka huu badala yake wangepambana kudai 'reforms'
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Septemba 04.2025 mwanasiasa huyo mkongwe nchini amesema hafurahishwi kuona ndani ya vyama vya upinzani kuna kile alichokitaja uwepo wa 'madalali' ambao wamekuwa wakitumika kwa namna moja au nyingine kukandamiza vyama vyao kwa maslahi yao binafsi.