Bwege ajiondoa ACT, atimkia CHADEMA

Bwege ajiondoa ACT, atimkia CHADEMA

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671
BWEGE.jpg
Mwanasiasa machachari na aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Senior Selemani Said Ally Bungara, maarufu "Bwege," ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama cha ACT Wazalendo kuanzia jana, Februari 18, 2026.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa umma, Bwege ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na hiyari yake mwenyewe kama mtu huru, baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kugundua kuwa ACT Wazalendo si "rafiki sahihi" katika safari yake ya kisiasa kama alivyokuwa amefikiria awali.

Bwege, ambaye anajulikana kwa msimamo wake thabiti na lugha za mvuto majukwaani, amebainisha kuwa mwelekeo wa sasa wa ACT Wazalendo ni tofauti na matarajio yake, jambo lililompelekea kuamua kutafuta jukwaa lingine la kuendeleza mapambano ya kisiasa.

“ACT Wazalendo si rafiki sahihi kwangu, nilivyofikiria ni tofauti na nilivyohisi. Kuanzia sasa mimi si mwanachama wa ACT Wazalendo tena kuanzia tarehe 18/2/2026. Mengine nitaongea baadaye. Ninategemea kushirikiana na kulitumia jukwaa la CHADEMA katika siasa za kudai demokrasia na maendeleo la taifa langu nilipendalo-Tanzania”, ameandika Bwege.

e3d2cc84-e24a-4797-9b95-542841a361ad.jpg
 
Utakaa na Zitto ufanye siasa gani wakati yeye Zitto Ccm wenyewe wamemdhalilisha Kigoma, kawekewa chawa tu na kapigwa.

Kimsingi ACT ni chama kilichochukuliwa na Wazanzibar kama replacement ya CUF Zanzibar, baada ya Maalim kuamuwa kumuachia CUF Lipumba.

Upande wa Tanganyika ACT, Bwege amezisoma nyakati vyema kupata platform mpya 2030 tukiwa na katiba mpya Ccm haiwezi kupanga wabunge jimbo hili mbunge awe nani au jimbo lile mbunge awe nani, wananchi ndio watachaguwa wabunge wao.
 
View attachment 3545966
Mwanasiasa machachari na aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Senior Selemani Said Ally Bungara, maarufu "Bwege," ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama cha ACT Wazalendo kuanzia jana, Februari 18, 2026.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa umma, Bwege ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na hiyari yake mwenyewe kama mtu huru, baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kugundua kuwa ACT Wazalendo si "rafiki sahihi" katika safari yake ya kisiasa kama alivyokuwa amefikiria awali.

Bwege, ambaye anajulikana kwa msimamo wake thabiti na lugha za mvuto majukwaani, amebainisha kuwa mwelekeo wa sasa wa ACT Wazalendo ni tofauti na matarajio yake, jambo lililompelekea kuamua kutafuta jukwaa lingine la kuendeleza mapambano ya kisiasa.

“ACT Wazalendo si rafiki sahihi kwangu, nilivyofikiria ni tofauti na nilivyohisi. Kuanzia sasa mimi si mwanachama wa ACT Wazalendo tena kuanzia tarehe 18/2/2026. Mengine nitaongea baadaye. Ninategemea kushirikiana na kulitumia jukwaa la CHADEMA katika siasa za kudai demokrasia na maendeleo la taifa langu nilipendalo-Tanzania”, ameandika Bwege.

Chanzo: Jambo TV

Amefanya VYEMA ..... hicho chama cha Zitto kiko kwa maslahi ya Zanzibar tu. Huku Bara ni Washirika wa CCM.
 
Uamuzi mzuri
 
bwege lilikua suala la muda tu, anaikubali sana chadema ya TAL
 
maskini dah,
ubwege na ulofa wa kisiasa unajidhihirisha waziwazi kabisa mchana kweupe :1Head:
 
Hata hivyo wanasiasa wenye elimu duni jamii ya Bwege hatuna matumizi nao.

Tulipofikia tunahitaji Bunge liwe la watu wasomi, critical &great thinkers sio waleta viroja na vihoja mara waruke sarakasi bungeni na mapambio kwa watawala.
 
Back
Top Bottom