Bwana wangu anaendesha bodaboda, nifanyaje?

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,921
14,821
Dear Money Penny

YAH: BWANA WANGU ANAENDESHA BODABODA
Mimi NI binti ambae sikuwahi kuwa kwenye mahusiano nikiwa chuoni.

Nilikuwa busy na masomo na ibada za casfeta.

Mapenzi yangu yalikuwa Kwa Yesu.

Baada ya kumaliza masomo sikupata KAZI, nikasota benchi Kwa Miaka 5, wenzangu nilisoma NAO walishaolewa na kuzaa na KAZI wanazo.

Nimevumilia lakini dadangu akaniambia tafuta bwana angalau uzae UMRI unaenda.

Siku Niko kwenye fellowship nikakutana na Kaka mmoja mlokole mwenzangu, nae NI graduate lakini Hana ajira
Amenunua bodaboda Kwa mkopo WA kampuni ya "WATU" pale Tegeta ndio anafanya nayo biashara apate kipato

Lakini ni mwaminifu, ananipenda mno na KAOKOKA,

Hatujawahi zini, Ila naogopa Sana kuolewa nae, maana kipato chake NI bodaboda Tu naona aibu mpaka aje kununua gari haya maisha yatakuwaje?

Kweli money penny bwana wangu anaendesha bodaboda lakini naona aibu kumtambulisha kwetu, ananipenda Sana nifanyaje??

Wako
Eliza."

Jamaa. Eliza anaomba msaada huku

Kumbuka maisha ni kuvumiliana na kusaidia pia kupendana huenda wewe ndiye mwenye nyota ya usaidizi na nguvu za kimsaidia kupata hiyo gari mapema na maendeleo mengine zaidi ila kama unampenda na anakupenda anzisha nae maisha tu..unaweza subiri mwenye na navyo ila asiwe na mapenzi nawewe kama huyo mlokole wako.
 
Dah Ila maisha sio poa ee
Degree holder anaendesha bodaboda😭😭😭
Tena WA chip UDSM
 
Back
Top Bottom