mtoto yeyote ambaye umri wake ni chini ya miaka saba is presumed kuwa anatakiwa kuishi na mama yake, labda kama yapo mazingira yanayohatarisha ustawi wa mtoto kwa hasa kile wanachoita kwa ujumla "best interest of the child". mfano wake ni pale kama, unaona akiishi na mama yake kwa huyo mume mwenza haki zake kadhaa zilizoko kwenye sheria namba 21 ya 2009 zitaathirika. labda atakosa haki ya elimu, labda pale kuna cruelty/mateso kwa mtoto, na mambo mengi ambayo kama yakionekana utatakiwa kufanya application mahakamani kuomba mtoto aondolewe pale ili akae na wewe, la sivyo kama anaishi vizuri tu utatakiwa kuendelea kutoa matunzo palepale hadi atakapofika miaka saba. hata akifika miaka hiyo saba, bado hata yeye mawazo yake/opinion yake itahitajika pamoja na kwamba sio binding kwa sheria kwa kupima best interest of him/her. akifika miaka saba sasa, ndio utafanya application court ili mahakama iamuru kwamba mtoto akae kwako.
akianza kukaa kwako, mtu yeyote hata mama yake akija kumuiba au kumtorosha, basi atapata adhabu kulingana na ilivyo kwenye sheria namba 21 ya 2009 na penal code.
USHAURI; jitahiti kukaa karibu na mtoto, yaani mtembelee mara kwa mara ukimpelekea zawadi nzuri nk ili uteke moyo wake. mtoto hata kama hakai na wewe kisheria unayo haki ya kumtembelea hata yeye mtoto kukutembelea. ukishateka moyo wake, atakuwa anakupenda hivyo akifika miaka saba hatakataa kuishi na wewe. kuna watoto wengine akili zao huwa zinakaa kwa mama hadi anakuwa mtata ile mbaya, hivyo akifika miaka saba ukamwambia aishi na wewe na hakupendi inamuathiri hadi masomo anaanza kutoroka shule, anaanza kukimbilia mtaani etc hivyo mama akiona hivyo anaenda mahakamani kutoa hiyo kama sababu kuwa mtoto kwa maslahi yake bora anatakiwa kuishi naye...ukifanya mchezo mamake na mume mwenza anaweza kumlisha maneno mabaya akakuchukia,.....jitahidi kama nilivyokwambia....hii ni kwasababu opinion ya mtoto hata kama haisupersede sheria inafikiriwa pale inapotakiwa kuamriwa wapi mtoto akaishi. you need to win her/his heart, unless kama mtoto huyo kweli si wa kwako ni wa jamaa yako, labda wewe ulifikiri wa kwako kumbe jamaa likuwa anakuibia wakati wewe ulipokuwa unaishi na huyo mwanamke, ulivyoenda ulaya wakaamua wamalizie kabisa...nendeni mkapime DNA. anayemjua mtoto ni wa nani ni mama sio wewe.