mfanyabiashara maarufu mkazi wa mlandizi, mkoa wa pwani ndugu BON KAVISHE,amemuua babake mdogo kwa risasi majira ya saa 10 usiku nyumbani kwake mlandizi. tukio hilo limetokea siku ya jumamosi kuamkia jumapili ya tarehe 12.05.2013 baada ya kukamilika sherehe ya harusi ya mdogo wake.taarifa zinadai kuwa baada ya sherehe hiyo ndugu jamaa na marafik wakaenda kujipumzisha.ndipo ndugu KAVISHE ambaye ni mmiliki wa bar maarufu hapa mlandizi ya zimbabwe bar alipoenda kujipumzisha nyumbani yeye na babake mdogo, lakin wakati wa usiku babake mdogo akataka aende choon ndipo katka harakati akajikuta ameingia chumbani kwa mwanae na ndipo mke wa kavishe akapiga kelele akidhani ni mwizi na ndugu kavishe kumpiga risasi na kufariki papo hapo.mpaka sasa ndugu kavishe anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.