Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,719
- 215,830
Bwana Chapati alikuwa classmate miaka hiyo, tulipata bahati ya kuonana jana kwenye sherehe ya harusi tukiwa wote kama wageni. Ilikuwa ni furaha kukutana na mtu mnaefahamiana na furaha inazidi kama mtu huyo hamjaonana kwa miaka inayozidi 20.
Katika maongezi yetu, bwana Chapati alinifahamisha ni mhasibu na amehitimu CPA miaka kama mitano iliyopita, Sky na wewe uko wapi sikuhizi basi na mimi kumfahamisha kuwa ninaishi Kwamtogole na kile kibiashara changu cha vitafunwa kinanisaidia sana maana nilishidwa kusema ninauza chapati na maandazi, asijeona ninamdhihaki bure.
Bwana Chapati amefikisha miaka 33 mwaka huu, hana familia wala hategemei kuoa, anasema wanawake wote ni wachunaji, jamani, kwani unaweza kula bila kuliwa? Katika maongezi kumbe na yeye aliisikia hii habari Hata kama ningeombwa na Adamu na Hawa, mimi simtaki tena Na yenyewe imezidi kumtoa mawazo yake ya kuoa.
Ananiambia akipata mwanamke wa kumzalia watoto wawili basi inatosha, nimemwambia ni bahati sana kumpata huyo mwanamke na wengine watakupeleka ustawi wa jamii na hiyo pesa unayoionea ubahili utaishia kumtuza huyo mama na watoto mpaka watoto wafikishe umri wa miaka 18.
Jamani kuna wanaume wabahili kiasi wanaogopa kuoa.
Jina la Chapati ni lakubuni na ninamwomba radhi yeyote nitakae mkwaza kwa matumizi ya jina hilo.