Unaweza kudhani ni kitu cha kawaida ukikichukulia juu juu, lakini kina maelezo yake tofauti kabisa. Juzi kwenye taarifa ya habari tuliambiwa kuwa changamoto za mashine za BVR ni pamoja na baadhi ya vidole vya watu kushindwa kusomeka alama zake kwenye scanner.
Sababu imetolewa eti ni kutokana na uchafu wa vidole lakini hata baada ya wahusika kuombwa kusafisha viganja vyao zaidi ya mara nne ilishindikana kusomeka. Sababu ya kusema ni uchafu ni majibu rahisi sana yaliyokosa tafakuri jadidi, kitaalam kinachosoma alama za vidole ni mwanga mkali wa laser, sasa hivyo vidole vilikuwa na uchafu kiasi gani laser kushindwa kupenya?
Kwa wenzetu watu hao wangechukuliwa kwa uchunguzi wa kina kujua ni nini hasa kinasababisha mionzi ya laser ishindwe kusoma alama za vidole vyao.
Kwenye ulimwengu wa roho kuna mapepo watu tunaishi nao katika Jamii lakini hawana utambulisho wowote, popote wapo, chochote wanafanya lakini hawaachi alama yeyote.
Mwaka 2000 tulikuwa na gari ndogo tukivuka mpaka wa Malaysia kuingia Singapore, ni mpaka wa kisasa mno lakini kuna watu wawili mke na mume scanner za mipaka yote miwili zilishindwa kuwatambua.
Ilikuwa jambo la ajabu sana mpaka wa Malaysia wakadhani system yao ina shida wakawachukua mpaka mpaka wa Singapore hali ilikuwa ileile, viganja vyao havisomi chochote kwenye mtandaoni hata details zao kwenye passport zao zilikuwa hazisomi kabisa mtandaoni, tuliwaacha pale na sikujua nini kiliendelea.
Zinatokeaga ajali nyingi watu wanafariki na kuumia sana lakini unapata kumbukumbu ya mtu uliyekuwa naye kwenye gari, lakini haonekani popote pale, kwenye mikusanyiko pia watu hawajui wapo, kwenye misosi na vinywaji pia wanaweza kukufanyia michezo unaagiza chakula lakini unakula chote lakini hushibi kumbe jamaa kakusaidia au unakula kidogo tu unashiba sana kumbe jamaa kakuongezea, mifano ni mingi.
Kilichotokea BVR ndio kinachotokea kila siku tunaishi na mapepo bila kujua.