nilibahatika kufanya kazi ya bvr, kwa muda wa wiki nne niliofanya kazi hiyo nilizalisha vitambulisho 1700 na ushee hivi. Kituko pekee nilichokutana nacho ni hiki, alikuja mama mmoja kipofu alivaa kaniki huku amejifunga kamba nyekundu kiunoni, kichwani na mikononi, wanaovaa hivyo huwa wanasema wana majini. Ilipofika zamu yake kazi ikaanza ya vidole kukataa kusoma, nilijaribu mara tano pamoja na kufuta vidole vyake kwa kitambaa ilishindikana. Mama mmoja kati ya wawili waliomsindikiza akamwambia yule mama kipofu kwani wewe si unamajini waombe wakuruhusu. Basi yule mama kipofu aliomba sekunde kadhaa kwa kilugha ya kabila lake alichanganya na kiswahili, nachokumbuka alisema hicho anachotaka kufanya ni kwa ajili ya kupata kitambulisho cha kupigia kura hakina madhara na wao majini. Baada maombi yake hayo nikaanza tena kuchukua alama za vidole vilikubali na watu wengine waliokuwepo wakisubiri zamu yao tukaishia kucheka tu na yule Mama alipata kitambulisho chake.