BVR imethibitisha kuna watu ni mapepo

BVR imethibitisha kuna watu ni mapepo

Mimi nilikuwa BVR operator somewhere. Niligundua kuwa 98% ya watu waliokuwa fingeprint zao hazisomi ni wale ambao walikuwa wanaugua ganzi ktk mikono yao. 2% iliyobaki walikuwa wazee sana!!

Wanaugua ganzi???? Je wewe ni nguli wa magonjwa?? Fafanua visuri juu ya huu ugonjwa mpay? Je ile miale haipiti kwenye ngozi wa wazee sana?
 
Ni michezo tu ili mpate muda wa kufikirisha bongo....viganja vinakuwa kama miti japo kwa macho ya kawaida unaona ni viganja kamili
Umeona ile video ya ifakara yule jamaa anayeshindwa kuangalia kabisa camera ili apigwe picha? Mwenye kuitaka aniambie nimtumie

Nitumie hiyo video mkuu.
 
Hii haina tofauti sana na kile walichofanyiwa wale walimu wa mwibara
- unapika chakula kizuri wali nyama ukianza tu kula kinageuka ugali maharagwe
- unalala chumbani na milango unafunga yote lakini kukicha unajikuta umelala nje
- unavaa nguo zako nzuri za gharama ukitoka nje unajikuta umevaa magunia
- unashikwa na kiu unachota Maji unywe ukianza tu yanageuka rangi

Hii hatareee sana lazima ukimbie mji aisee
 
Heshima yako mkuu Mshana Jr.
mm ni mmoja kati ya watu ambao finger print ziligoma kusoma lakini natumia simu aina mbili tofauti na zote zina fingerprint scanner nnazotumia kutoa lock na nimeregister 5 fingers
na ofisini kuna kakifaa wametuwekea kwa ajili ya staff registration nacho ni finger print scanner kwa hiyo nadhani pamoja na uliyosema nadhan na mashine zao zinachangia pia
 
piego I wish one day we can have a face to face argument about these things, it may unveil many ambiguous/anonymous staled facts about spirits, souls, witchcraft and the like

So u dont agree with my point or what i understand is be the truth is the truth n u want us to exchange ideas?
Binadamu wote wanaosema wana extra ordinary powers , the poweers arent theirs.. they are in some sort of agreement with these so called spirits
Mi nashangaa watu wanasema mambo ya majini ni uzushi. Hivi vitu ni kweli. Kama mtu abisha akamuulize beyonce "who is sasha fierce?"
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kudhani ni kitu cha kawaida ukikichukulia juu juu, lakini kina maelezo yake tofauti kabisa. Juzi kwenye taarifa ya habari tuliambiwa kuwa changamoto za mashine za BVR ni pamoja na baadhi ya vidole vya watu kushindwa kusomeka alama zake kwenye scanner.

Sababu imetolewa eti ni kutokana na uchafu wa vidole lakini hata baada ya wahusika kuombwa kusafisha viganja vyao zaidi ya mara nne ilishindikana kusomeka. Sababu ya kusema ni uchafu ni majibu rahisi sana yaliyokosa tafakuri jadidi, kitaalam kinachosoma alama za vidole ni mwanga mkali wa laser, sasa hivyo vidole vilikuwa na uchafu kiasi gani laser kushindwa kupenya?

Kwa wenzetu watu hao wangechukuliwa kwa uchunguzi wa kina kujua ni nini hasa kinasababisha mionzi ya laser ishindwe kusoma alama za vidole vyao.

Kwenye ulimwengu wa roho kuna mapepo watu tunaishi nao katika Jamii lakini hawana utambulisho wowote, popote wapo, chochote wanafanya lakini hawaachi alama yeyote.

Mwaka 2000 tulikuwa na gari ndogo tukivuka mpaka wa Malaysia kuingia Singapore, ni mpaka wa kisasa mno lakini kuna watu wawili mke na mume scanner za mipaka yote miwili zilishindwa kuwatambua.

Ilikuwa jambo la ajabu sana mpaka wa Malaysia wakadhani system yao ina shida wakawachukua mpaka mpaka wa Singapore hali ilikuwa ileile, viganja vyao havisomi chochote kwenye mtandaoni hata details zao kwenye passport zao zilikuwa hazisomi kabisa mtandaoni, tuliwaacha pale na sikujua nini kiliendelea.

Zinatokeaga ajali nyingi watu wanafariki na kuumia sana lakini unapata kumbukumbu ya mtu uliyekuwa naye kwenye gari, lakini haonekani popote pale, kwenye mikusanyiko pia watu hawajui wapo, kwenye misosi na vinywaji pia wanaweza kukufanyia michezo unaagiza chakula lakini unakula chote lakini hushibi kumbe jamaa kakusaidia au unakula kidogo tu unashiba sana kumbe jamaa kakuongezea, mifano ni mingi.

Kilichotokea BVR ndio kinachotokea kila siku tunaishi na mapepo bila kujua.

Nijuavyo mikono ikiwa misafi lakini ina jasho scanner haisomi. It happened to my friend who sweats a lot mikononi alipokua akijiandikosha nssf. Labda kweli kuna mapepo ila sio wote wanaoshindwa kusomwa kwenye scanner ni mapepo
 
Unaweza kudhani ni kitu cha kawaida ukikichukulia juu juu, lakini kina maelezo yake tofauti kabisa. Juzi kwenye taarifa ya habari tuliambiwa kuwa changamoto za mashine za BVR ni pamoja na baadhi ya vidole vya watu kushindwa kusomeka alama zake kwenye scanner.

Sababu imetolewa eti ni kutokana na uchafu wa vidole lakini hata baada ya wahusika kuombwa kusafisha viganja vyao zaidi ya mara nne ilishindikana kusomeka. Sababu ya kusema ni uchafu ni majibu rahisi sana yaliyokosa tafakuri jadidi, kitaalam kinachosoma alama za vidole ni mwanga mkali wa laser, sasa hivyo vidole vilikuwa na uchafu kiasi gani laser kushindwa kupenya?

Kwa wenzetu watu hao wangechukuliwa kwa uchunguzi wa kina kujua ni nini hasa kinasababisha mionzi ya laser ishindwe kusoma alama za vidole vyao.

Kwenye ulimwengu wa roho kuna mapepo watu tunaishi nao katika Jamii lakini hawana utambulisho wowote, popote wapo, chochote wanafanya lakini hawaachi alama yeyote.

Mwaka 2000 tulikuwa na gari ndogo tukivuka mpaka wa Malaysia kuingia Singapore, ni mpaka wa kisasa mno lakini kuna watu wawili mke na mume scanner za mipaka yote miwili zilishindwa kuwatambua.

Ilikuwa jambo la ajabu sana mpaka wa Malaysia wakadhani system yao ina shida wakawachukua mpaka mpaka wa Singapore hali ilikuwa ileile, viganja vyao havisomi chochote kwenye mtandaoni hata details zao kwenye passport zao zilikuwa hazisomi kabisa mtandaoni, tuliwaacha pale na sikujua nini kiliendelea.

Zinatokeaga ajali nyingi watu wanafariki na kuumia sana lakini unapata kumbukumbu ya mtu uliyekuwa naye kwenye gari, lakini haonekani popote pale, kwenye mikusanyiko pia watu hawajui wapo, kwenye misosi na vinywaji pia wanaweza kukufanyia michezo unaagiza chakula lakini unakula chote lakini hushibi kumbe jamaa kakusaidia au unakula kidogo tu unashiba sana kumbe jamaa kakuongezea, mifano ni mingi.

Kilichotokea BVR ndio kinachotokea kila siku tunaishi na mapepo bila kujua.

kwa hiyo hata yule mama yetu wa mboga mboga za milioni 10 na ushee hivi,kule muleba naye zombi kumbe!nasikia mtambo ulimkataa
 
Back
Top Bottom