habari za kuaminika kutoka London zinasema ya kwamba ,mheshimiwa Lowassa alikuwapo London 17 februari mwaka huu,siku ambayo mkataba wa Buzwagi ulitiwa saini,
Lowassa aliingia London tarehe 16 february akitokea Paris,Ufaransa ambako alikuwapo kikazi kwa muda wa siku nne,pia mheshima Lowassa alifikia katika Hoteli ya Churchil hill jijini Londoa ambako waziri karamagi alikuwa amefikia.
na katika Hoteli hiyo ndipo mkataba wa buzwagi uliposainiwa,
akiwa London,Lowassa alipokutana na watendaji wa serikali waliokuwa na Rais kikwete na kwa Upole wakamuuliza 'Mheshimiwa huko hapa?'Basi naye akawaambia alikuwa amekwenda kufanya Shopping..na kabla ya hapo alimpigia Balozi wa London na kumuelezea kwamba anakuja Lodnon ila asimpangie chumba..
Je kwa maelezo haya,kwa kuwa Lowassa alikataa asifanyie booking ya chumba ,je wana wa watanzania hamuoni tayari kuna mazingira tata kuhusus mkataba huu?
huyu Lowassa ana nia gani na SISI?
Source:Mwanahalisi
Hii habari inaukweli kiasi fulani.
Lowassa ahudhuria mkutano wa Afrika UfaransaBy
Saidi Nguba | Published 02/15/2007 |
Habari Mpya |
Na Mwandishi Maalum, Nice, Ufaransa
WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amekuwa miongoni mwa viongozi na wakuu wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa siku mbili mjini hapa ulioanza leo (Alhamisi Feb. 15, 2007)kujadili hali ya baadaye ya Afrika.
Lowassa anamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano huo wa 24, unaoitwa Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na Ufaransa ambao mada yake mwaka huu ni Afrika na uwiano wa utulivu duniani (Africa and Global Balance).
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Rais Jacques Chirac alisema kuwa yapo matumaini makubwa ya kuleta maendeleo ya kiuchumi katika Afrika, kwa vile Afrika ni tajiri ila watu wake ndiyo masikini.
Chirac alisema kuwa kwa kuwa Afrika peke yake ina zaidi ya theluthi moja ya madini yote duniani, ikisaidiwa na kama madini hayo hayakuporwa, bara hilo na watu wake watapiga hatua kubwa ya maendeleo.
Afrika mpya inakuja
naipenda Afrika kwa moyo wangu wote, Rais huyo wa Ufaransa alisema na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuusaidia kwa hali na mali Umoja wa Afrika katika jitihada zake za kuleta maendeleo ya kisiasa na kiuchumi ya Afrika.
Aliongeza: Hali inayoonekana kwamba Afrika ni bara masikini siyo ukweli wa mambo
kuna mambo mawili ya kufanya, tuiache Afrika mali zake ziporwe au tuisaidie Afrika ipate maendeleo
tukiisaidia Afrika watu wake watapata maendeleo.
Mapema, akizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika, Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU) Rais John Kufour wa Ghana alisema Afrika inabidi kuheshimiwa na kwamba hali ya Afrika sasa inabadilika kuwa nzuri kutokana na kukua kwa demokrasia na uchumi.
Viongozi wengine aliozungumza ni pamoja na Rais wa sasa wa Umoja wa Ulaya, Kiongozi wa Ujerumani, Chansela Angela Merekel ambaye alisema hakuna jinsi nyingine ila kuisaidia Afrika kwa ajili ya mandeleo yake na dunia nzima kwa jumla.
Waziri Mkuu Lowassa aliwasili Nice jana (Jumatano Feb. 14, 2007) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo kumwakilisha Rais Kikwete.
Miongoni mwa waliomo kwenye ujumbe wa Tanzania ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe; Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mahmood Thabit Kombo.
Kesho (Ijumaa Feb. 16, 2007) mkutano huo utafungwa rasmi mchana na kutakuwa na mkutano wa waandishi wa habari kuelezea matokeo yake.