Buzwagi: Lowassa Alikuwa London Siku Ya Mkataba

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
habari za kuaminika kutoka London zinasema ya kwamba ,mheshimiwa Lowassa alikuwapo London 17 februari mwaka huu,siku ambayo mkataba wa Buzwagi ulitiwa saini,
Lowassa aliingia London tarehe 16 february akitokea Paris,Ufaransa ambako alikuwapo kikazi kwa muda wa siku nne,pia mheshima Lowassa alifikia katika Hoteli ya Churchil hill jijini Londoa ambako waziri karamagi alikuwa amefikia.
na katika Hoteli hiyo ndipo mkataba wa buzwagi uliposainiwa,
akiwa London,Lowassa alipokutana na watendaji wa serikali waliokuwa na Rais kikwete na kwa Upole wakamuuliza 'Mheshimiwa huko hapa?'Basi naye akawaambia alikuwa amekwenda kufanya Shopping..na kabla ya hapo alimpigia Balozi wa London na kumuelezea kwamba anakuja Lodnon ila asimpangie chumba..

Je kwa maelezo haya,kwa kuwa Lowassa alikataa asifanyie booking ya chumba ,je wana wa watanzania hamuoni tayari kuna mazingira tata kuhusus mkataba huu?

huyu Lowassa ana nia gani na SISI?

Source:Mwanahalisi
 
..............ukishangaa ya musa.............
 
Mmhh,
Sasa ndo ndo mambo yanaanza kufunguka taratibu.Wakiambiwa hii ni serikali ya kishkaji na kisanii wanakuja juu,sasa ni kwa ethics zipi za kiuogozi Waziri Mkuu anmwambia Balozi asimpangie chumba cha kulala?Je ratiba ya Waziri Mkuu ilimruhusu kwenda kufanya shopping huko?Ina maana kuna tofauti kubwa sana (iwe ya bei,aina au ubora wa bidhaa) kati ya maduka ya London na Paris kiasi cha kumfanya huyo Lowassa ashindwe kufanya shopping Paris?kama hakuwa na muda Paris huo wa London ulitoka wapi?

Ndugu zangu kweli nimeamini huyu jamaa uwezo wake wa kufikiri na kutenda ni afadhali wa yule Ziro wa Mtanzania (kama bado yupo),ndo sababu juzi kule Mbeya ati anasema mkataba wa Buzwagi safi.Na je hii ni kudhihirisha alichosema Zitto kuwa Muungwana hakujua utiaji saini wa Buzwagi na kwa maana hiyo Karamagi na Lowassa walimpiga changa la macho swahiba wao Muungwana?Kama ndo hivyo basi mwaka huu kazi ipo.Na labda ndo sababu za mino'ngono hapa mjini kuwa Muungwana na Lowassa hawaivi tena yani ni paka na panya.Kama hivi ndivyo I pity you my beloved Tanzania...yaani wengine wapo buzy kuiba,kuuza nchi...!!!
 
habari za kuaminika kutoka London zinasema ya kwamba ,mheshimiwa Lowassa alikuwapo London 17 februari mwaka huu,siku ambayo mkataba wa Buzwagi ulitiwa saini,
Lowassa aliingia London tarehe 16 february akitokea Paris,Ufaransa ambako alikuwapo kikazi kwa muda wa siku nne,pia mheshima Lowassa alifikia katika Hoteli ya Churchil hill jijini Londoa ambako waziri karamagi alikuwa amefikia.
na katika Hoteli hiyo ndipo mkataba wa buzwagi uliposainiwa,
akiwa London,Lowassa alipokutana na watendaji wa serikali waliokuwa na Rais kikwete na kwa Upole wakamuuliza 'Mheshimiwa huko hapa?'Basi naye akawaambia alikuwa amekwenda kufanya Shopping..na kabla ya hapo alimpigia Balozi wa London na kumuelezea kwamba anakuja Lodnon ila asimpangie chumba..

Je kwa maelezo haya,kwa kuwa Lowassa alikataa asifanyie booking ya chumba ,je wana wa watanzania hamuoni tayari kuna mazingira tata kuhusus mkataba huu?

huyu Lowassa ana nia gani na SISI?

Source:Mwanahalisi

Hii habari inaukweli kiasi fulani.

Lowassa ahudhuria mkutano wa Afrika UfaransaBy Saidi Nguba | Published 02/15/2007 | Habari Mpya |

Na Mwandishi Maalum, Nice, Ufaransa

WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amekuwa miongoni mwa viongozi na wakuu wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa siku mbili mjini hapa ulioanza leo (Alhamisi Feb. 15, 2007)kujadili hali ya baadaye ya Afrika.

Lowassa anamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano huo wa 24, unaoitwa ‘Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na Ufaransa’ ambao mada yake mwaka huu ni “Afrika na uwiano wa utulivu duniani” (Africa and Global Balance).

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Rais Jacques Chirac alisema kuwa yapo matumaini makubwa ya kuleta maendeleo ya kiuchumi katika Afrika, kwa vile Afrika ni tajiri ila watu wake ndiyo masikini.

Chirac alisema kuwa kwa kuwa Afrika peke yake ina zaidi ya theluthi moja ya madini yote duniani, ikisaidiwa na kama madini hayo hayakuporwa, bara hilo na watu wake watapiga hatua kubwa ya maendeleo.

“Afrika mpya inakuja…naipenda Afrika kwa moyo wangu wote,” Rais huyo wa Ufaransa alisema na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuusaidia kwa hali na mali Umoja wa Afrika katika jitihada zake za kuleta maendeleo ya kisiasa na kiuchumi ya Afrika.

Aliongeza: “Hali inayoonekana kwamba Afrika ni bara masikini siyo ukweli wa mambo…kuna mambo mawili ya kufanya, tuiache Afrika mali zake ziporwe au tuisaidie Afrika ipate maendeleo…tukiisaidia Afrika watu wake watapata maendeleo”.

Mapema, akizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika, Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU) Rais John Kufour wa Ghana alisema Afrika inabidi kuheshimiwa na kwamba hali ya Afrika sasa inabadilika kuwa nzuri kutokana na kukua kwa demokrasia na uchumi.

Viongozi wengine aliozungumza ni pamoja na Rais wa sasa wa Umoja wa Ulaya, Kiongozi wa Ujerumani, Chansela Angela Merekel ambaye alisema hakuna jinsi nyingine ila kuisaidia Afrika kwa ajili ya mandeleo yake na dunia nzima kwa jumla.

Waziri Mkuu Lowassa aliwasili Nice jana (Jumatano Feb. 14, 2007) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo kumwakilisha Rais Kikwete.

Miongoni mwa waliomo kwenye ujumbe wa Tanzania ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe; Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mahmood Thabit Kombo.

Kesho (Ijumaa Feb. 16, 2007) mkutano huo utafungwa rasmi mchana na kutakuwa na mkutano wa waandishi wa habari kuelezea matokeo yake.
 
Huo mkataba ni mzuri kwa sababu JK, EL wanafaidika nao binafsi na ndiyo sababu Karamagi wala hashituki, anaendelea kula kuku na biskuti.

Hadi pale Wananchi wa Tanzania na ambao ndio walipa kodi watakaposema basi ndio hawa mafisadi wataacha (Hawawezi kuacha kwa hiari). Uhujumu wa uchumi sheria yake lazima iwe kunyongwa hadi kufa na kufilisiwa.
 
1. Hii habari ya kuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Lowassa alikuwepo London, tena kwenye hotel ya Churchill uliposiniwa mkataba wa Buzwagi, siku mkataba uliposainiwa mbona haikuwahi kusemwa huko nyuma?

2. Kama alikwenda London kufanya shopping kama inavyodaiwa, ukizingatia alikuwa Ufaransa hapo jirani tu je ni kosa?

3. Vilevile alipokwenda London bila shaka alikuwa na taarifa za Waziri Karamagi kuwepo huko akaamua kwenda kumsalimia hapo hotelini, je ni kosa?

4. Ikiwa alimpigia simu Balozi na kumtaarifu kuwa anakuja London ila asimfanyie booking ya hoteli hamuoni kwamba hakuwa anajaribu kuficha chochote vinginevyo angejiendea kimyakimya.

5. Sidhani kama alienda kwa kujiiba au kujificha, yeye ni waziri mkuu na anajua kuna Watanzania huko London tena wengi tu na wanamjua na watamwona na watamuuliza.

6. Hii hoja ya kumlundika na Mheshimiwa Karamagi ingekuwa na nguvu kama Waziri Mkuu angejiiba kimyakimya toka Dar kwenda huko hotelini London. Lakini tayari alikuwa huko Ufaransa kikazi.

Kwa kutumua msemo wa mwanaJF mmoja hapa "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni"
 
..uchambuzi mzuri wa pumba ipi,mchele upi!
 
Unajua mwakilishi wanasheria wana kitu kinaitwa `circumstancial evidence` ushaidi wa mazingira.kitendo cha lowassa kwenda London,wakati mkataba ukisainiwa huko,na leo anajitokeza hadhalani kuutetea kwamba hauna kasoro kwa mtu mwenye uelewa lazima atilie shaka.
 
Nakusikia Kufakunoga, ila mimi nadhani kinachoendelea hapa ni waziri mkuu amejaribu bila mafanikio kumsitiri waziri Karamagi mbele ya wananchi.

Nisingetegemea amkane au amshutumu waziri wake wa madini mbele ya kadamnasi, especially ukichukulia kuwa Mheshimiwa Rais mwenyewe ambaye ndie bosi wao kauchuna. Wote wanafahamu huo mkataba bomu lakini ndio hivyo hakuna wa kumfunga paka kengele.
 
Mwakilishi inaonekana kuwa wewe ni mgeni wa kujua protocal za nchi .
Waziri mkuu ni kiongozi na hawezi kwenda kimya kimya tena London na kumwambia balozi wake asimfanyie booking ya chumba , hii sio sahihi hata kidogo.

Na pia kwenye hili kuna kila sababu ya watanzania kuilalamikia uingereza kwa kumpokea kiongozi wetu na bila kufuatia protocal za kumpokea kiongozi mkubwa wa nchi na ndio maana hata wakiwa wanasafir wakiwa wanajaza mafuta kwenye viwanja vya ndege huwa protocal inazingatiwa je?kwenda kulala hotelini na tena hata balozi hajamwandalia mazingira ya ulinzi n.k hii ni sawa?

Huyu alikwenda na walinzi wanagapi?
Ni kwa nini walinzi tuliowapa jukumu la kumlinda waziri wetu mkuu wamruhusu kwenda na mlinzi mmoja?
Hapa kuna deal tena inawezekana hawa jamaa walipokea cha kwao in cash ndio maana jamaa kaamua kufuata hadi london kwenyewe.
 
nchi imejaa usaniii mtupu,mambo yote sasa hivi yanafanywa kisanii sana,kuna jambo linakuja.kuna msanii mmoja anakaribia kupewa madaraka pale magogoni,na alihusika kusuka dili la Richmond.stay tuned
 
Mpaka Kieleweke,

Naomba nivumilie kidogo mkuu, inawezekana kabisa sielewi vizuri hizi taratibu za kiitifaki lakini:

1. Kama alikuwa anakwenda shopping yake binafsi (kama tulivyoelezwa) baada ya kazi Ufaransa, sioni sababu ya yeye kupokewa kiserikali na Uingereza, angekuwa amekwenda kikazi bila shaka hilo lingefanyika.

2. Si ajabu alikwenda na mlinzi mmoja katika jitihada za kubana matumizi, yaani asionekane anatumbua pesa ya walipa kodi kwa kuandamana na msafara mzima kwa ajili ya shopping yake binafsi, angeandamana na msafara wake wote kwa ajili ya shopping binafsi bila shaka tungelalamika ubadhirifu wake.

3. Kitendo cha kumtaarifu Balozi na kumwambia asimtafutie chumba hotelini sioni kama kina tatizo, kwani angeshindwa nini kumwambia balozi am-bookie chumba hapo Churchill hotel? Mimi nadhani hakuwa na mpango wa kulala huko labda alirudi Paris siku hiyohiyo(sina uhakika lakini)

Mimi hapa najaribu kuangalia pande zote za hili suala.
 
We Mwakilishi unatoka dunia ipi?
Hivi ni sawa kwa Waziri Mkuu kwenda London bila kuwa na utaratibu wowote ule wa kiprotokali?swala la kwamba eti angetokea hapa Dar ndo ingekuwa issue halina msingi kabisa,ndhani wewe unataka kuimply kwamba Karamagi na Lowassa kukutana hapo Churchill ilikuwa ni coincidence,as a matter of fact and with due respect,coincidences do not work that way,kuhusu kuwa hii habari haikuwa hapo nyuma,kumbuka kuwa hili ni swala la ushahidi,na ushahidi si lazima upatikane muda huo huo tukio linapotokea ndo sababu leo hii katika inquest ya Diana kuna ushahidi mpya wa CCTV kutoka kwenye ile lift ya hotel kule Ufaransa na ni mwaka 1997,hivyo basi swala la msingi hapa ni kuwa tume huru iundwe na kuchunguza mienendo ya viongozi wote wanaohusishwa na Buzwagi,kwa nini wakutane Churchill wao wawili (coincidence!!!),pili kwa nini amzuie Balozi Maajar asimpangie chumba?what was so special mpaka akatae chumba?Lowassa ana maswali ya kujibu...just let's wait and see as...THE DRAMA KEEPS UNFOLDING...
 
habari za kuaminika kutoka London zinasema ya kwamba ,mheshimiwa Lowassa alikuwapo London 17 februari mwaka huu,siku ambayo mkataba wa Buzwagi ulitiwa saini,
Lowassa aliingia London tarehe 16 february akitokea Paris,Ufaransa ambako alikuwapo kikazi kwa muda wa siku nne,pia mheshima Lowassa alifikia katika Hoteli ya Churchil hill jijini Londoa ambako waziri karamagi alikuwa amefikia.
na katika Hoteli hiyo ndipo mkataba wa buzwagi uliposainiwa,
akiwa London,Lowassa alipokutana na watendaji wa serikali waliokuwa na Rais kikwete na kwa Upole wakamuuliza 'Mheshimiwa huko hapa?'Basi naye akawaambia alikuwa amekwenda kufanya Shopping..na kabla ya hapo alimpigia Balozi wa London na kumuelezea kwamba anakuja Lodnon ila asimpangie chumba..

Je kwa maelezo haya,kwa kuwa Lowassa alikataa asifanyie booking ya chumba ,je wana wa watanzania hamuoni tayari kuna mazingira tata kuhusus mkataba huu?

huyu Lowassa ana nia gani na SISI?

Source:Mwanahalisi

Oh jamani, hivi mangapi ambayo bado yako sirini. Sishangai sasa kusikia kuwa kabla hoja ya Buzwagi haijaletwa bungeni Lowasa aliwaita wabunge wa ccm na kuwapa somo. Hivi kuna mangapi hapa yanafichwa?
 
Mpaka Kieleweke,

Naomba nivumilie kidogo mkuu, inawezekana kabisa sielewi vizuri hizi taratibu za kiitifaki lakini:

1. Kama alikuwa anakwenda shopping yake binafsi (kama tulivyoelezwa) baada ya kazi Ufaransa, sioni sababu ya yeye kupokewa kiserikali na Uingereza, angekuwa amekwenda kikazi bila shaka hilo lingefanyika.

2. Si ajabu alikwenda na mlinzi mmoja katika jitihada za kubana matumizi, yaani asionekane anatumbua pesa ya walipa kodi kwa kuandamana na msafara mzima kwa ajili ya shopping yake binafsi, angeandamana na msafara wake wote kwa ajili ya shopping binafsi bila shaka tungelalamika ubadhirifu wake.

3. Kitendo cha kumtaarifu Balozi na kumwambia asimtafutie chumba hotelini sioni kama kina tatizo, kwani angeshindwa nini kumwambia balozi am-bookie chumba hapo Churchill hotel? Mimi nadhani hakuwa na mpango wa kulala huko labda alirudi Paris siku hiyohiyo(sina uhakika lakini)

Mimi hapa najaribu kuangalia pande zote za hili suala.

Wewe hapa unaangalia huo upande wa Lowasa kwenda kufanya shoping na kwenda na mlinzi mmoja. Mimi naangalia upande wa Lowasa kukutana na Karamagi London kwenye kusaini mkataba wa Buzwagi. Pande zote mbili zimeangaliwa au sio!
 
Lowassa lazima ajibu hili kuwa ilikuwaje akaenda londoni bila kuwa na ulinzi wala kupita ofisi za ubalozi wetu huko.

Nguba uje hapa utupe majibu mapema iwezekanavyo kuwa ilikuwaje akaenda mpaka churchil hotel wakati hajautaarifu ubalozi wetu?
Angeumia ingekuwaje? balozi wetu angelikuwa na wakati mgumu sana kujieleza jinsi alivyomfanya waziri mkuuu wetu kimya kimya.

Waziri mkuu asema kama balozi zetu haziwezi kumfanyia booking za hotel ili tuweze kujua hilo mapema na balozi nyingine nazo zitaarifiwe mapema ili kutokumfanyia booking.
 
KUna habari kwamba LOWASA akiwa Mbeya amejibu na kusema kwamba yeye hahusiki na MKATABA WA BUZWAGI, tusubiri taarifa zaidi. Nadhani wataandika ktk magazeti
 
EL amekuwa akijaribu kuutetea kwa nguvu zake zote mkataba huu wa Buzwagi na Karamangi, ni kwa sababu anajua yuko nyuma ya pazia.

EL alijaribu kwa kushirikiana na spika na wa wabunge wa SISIEM kuizima hoja hii, lakini haijawezekana.

Jitihada za mwisho za EL nikujaribu kudanganya wananchi kwenye majukwaa ya siasa, hili nalo limepata dawa yake sasa.

Ningetegemea kabisa EL angesema mkataba huu hauna matatizo kwani wakati wa kusainiwa na mimi nilikuwepo tulikuwa chumbani na Kara. Sio kweli kwamba una manufaa kwetu sisi wawili yaani mimi EL na fisadi Kara pamoja na familia zetu.

Nchi imefakamiwa na walanguzi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom