Button Mushroom,hii aina ya uyoga wazalishaji wengi wanaiogopa sana

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,917
Button Mushroom, ni aina ya uyoga ambao ni ghar saba sokoni ukilinganisha na varieties zingine kama Oysters.Shida ni kwamba wazalishaji wanaiogopa hii aina kwa sababu nazani ya process zake za kuizalisha.

Button inapendwa sana sokoni kuliko Oster shida inakuja kwenye price yake ni ghari sana ambapo robo huwa inatembea hadi sh 15,000/

Button inalimwa na Mzungu mmoja yuko Iringa wanajiita Mafisio, huyu ndio suppliers wa Button Tanzania nzima, ingawa inaonekana ana changamoto za kuzalisha kiasi kwamba kwa sasa Button inatoka Kenya kampuni moha inaitwa Majestic, hawa ndio wana supply Button Tanzania kwa sasa.

Local prodycer wengi wanaiogopa hasa process zake.

Button kama uko ukanda wa Baridi kama Iringa, Mbea, Arusha na sehemu za Kilimanjaro unaweza izalisha ingawa pia hata sehemu za joto sema gharama zitakuwa juu.

Wazalishaji wengi wamejikita kwenye hii Oryster ambayo ni cheap sana na ni rahisi sana kuzalisha na imejaaa masokoni.

Rocess zake ndio zinafanya watu waiogope kuizalisha, ina process nyingi na ngumu ukilinganisha na hizi aina zingine.
IMG_20231205_135058.jpg
IMG_20231205_135134.jpg
 
process yake ina ugumu gani? soko pia litakuwa changamoto nafikiri wazungu wanakuja kulima huku wakiwa tayari na soko
 
Hao wanaokuuzia 15k unadhani ukienda kuwauzia watanunua kwa ngapi ? Mara nyingi tukifanya upembuzi yakinifu kuangalia retail prices ni kupotoka...
 
Soko la wapi changamoto? wakiwa na soko wapi? Nimesema Button ina changamoto kuzalisha, ila ndio aina inayo pendwa na wala uyoga.

Hakuna mtu anaye kuwa na soko tiyali watu wanaangalia gap wanazalisha.
 
Hao wanaokuuzia 15k unadhani ukienda kuwauzia watanunua kwa ngapi ? Mara nyingi tukifanya upembuzi yakinifu kuangalia retail prices ni kupotoka...
Button ni ghari tu hata bei ya jumla, nado ni ghari. si chini ya Tsh 8000 kwa bei ya jumla.
 
Market ipoje ? Kwahio tumetoka kwenye 15k, Button sio shida kuzalisha; kwenye shida kuna kina Shiitake; Like always shida ya haya mambo huwa ni soko la uhakika
 
Una mzigo au aunaulizia Soko wakati huna kitu uko kwenye AC unauliza soko likoje?

Nimesema currently Mafisio hawazalishi kwa wingi kwa sababu walipata ajari ya moto kwenye mabanda yao. Hivyo button inatoka Nairobi.

Unategemea uione ikiuzwa pembeni ya Barabara? Nisha semakwa sasa supplier anatoa Nairobi Kenya,hii ingetosha kukupa picha Soko lilivyo.
 
Button Mushroom, ni aina ya uyoga ambao ni ghar saba sokoni ukilinganisha na varieties zingine kama Oysters.Shida ni kwamba wazalishaji wanaiogopa hii aina kwa sababu nazani ya process zake za kuizalisha.

Button inapendwa sana sokoni kuliko Oster shida inakuja kwenye price yake ni ghari sana ambapo robo huwa inatembea hadi sh 15,000/

Button inalimwa na Mzungu mmoja yuko Iringa wanajiita Mafisio, huyu ndio suppliers wa Button Tanzania nzima, ingawa inaonekana ana changamoto za kuzalisha kiasi kwamba kwa sasa Button inatoka Kenya kampuni moha inaitwa Majestic, hawa ndio wana supply Button Tanzania kwa sasa.

Local prodycer wengi wanaiogopa hasa process zake.

Button kama uko ukanda wa Baridi kama Iringa, Mbea, Arusha na sehemu za Kilimanjaro unaweza izalisha ingawa pia hata sehemu za joto sema gharama zitakuwa juu.

Wazalishaji wengi wamejikita kwenye hii Oryster ambayo ni cheap sana na ni rahisi sana kuzalisha na imejaaa masokoni.

Rocess zake ndio zinafanya watu waiogope kuizalisha, ina process nyingi na ngumu ukilinganisha na hizi aina zingine.View attachment 2833854View attachment 2833855
Ivi vitu inabidi nivijaribu kuvila sio daily ugali na ubwabwa...Sasa huu unakaangwa au unachemshwa
 
Una mzigo au aunaulizia Soko wakati huna kitu uko kwenye AC unauliza soko likoje?
Sasa mtu utakuwa na mzigo kabla ya kufahamu soko lipo vipi ? Hii akili ya wapi hii ? Kipi kinaanza au watu waliosema ufanye due dilligence walimaanisha nini ?
Nimesema currently Mafisio hawazalishi kwa wingi kwa sababu walipata ajari ya moto kwenye mabanda yao. Hivyo button inatoka Nairobi.
Hivi una uhakika hizo story za mafisio uliziweka mwanzo au umeziweka sasa hivi na mimi ulitaka niingie akilini mwako kupata points ambazo zipo kichwani mwako
Unategemea uione ikiuzwa pembeni ya Barabara? Nisha semakwa sasa supplier anatoa Nairobi Kenya,hii ingetosha kukupa picha Soko lilivyo.
Vitu vingapi vinatoka Kenya ila haimaanishi kwamba soko ni kubwa..., huenda ni suppliers ambao wana uhakika na watu wanapenda kufanya nao kazi sababu ni reliable... Nenda supermarket yoyote soma labels za bidhaa uone ngapi zinatoka nje lakini haimaanishi kuna uhaba; Je wewe ukianza kuwapelekea Hoteli fulani leo wataacha kuchukua mzigo kwa supplier wao wa Kenya ?

Tupende kujibu maswali tukiulizwa sio kuleta longo longo nyingi tunakuwa hatujengi
 
Back
Top Bottom