SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,338
- 4,675
Kila mtu anamsaidia Raisi Magufuli kadri ya awezavyo.Mzee Butiku tumekusikia na tumekuelewa barabara.Kwamba viongozi wengine vikiwemo vyama vya kiraia vimsaidie Raisi katika vita hii ya kiuchumi ni jambo jema sana.Nilikwisha kushauri kuwa tunatakiwa kufanya aina ya fujo Fulani hivi ili dunia ielewe kuwa tumeumizwa sana na ushenzi wa hawa jamaa wanaojiita wawekezaji.
Nikisema fujo namaanisha tubebe wagonjwa wa Cancer wanaotaabika pale Ocean Road Hospital kwa sababu ya kukosa uwezo wa kupata matibabu tuandamane nao barabarani ili dunia ione jinsi wenzetu wanavyotaabika.
Tuchukue watoto wa shule za msingi wabebe matofali wanayokalia shuleni tena wakiwa wamevaa kaputula zao na sketi zilizochanika na kutoboka matakoni sababu ya kukwaruzika na mawe.Nasema tuandamane na watoto hao wakiwa hivyo dunia ione.
Kisha tubebe madreva bodaboda majeruhi wote kutoka MOI tuandamane nao wakiwa kwenye Wheel chairs.Hawa wengine wamepata ulemavu wa kudumu kwa sababu ya hospitali kukosa vifaa Tiba walivyofikishwa hospitalini.Tuwaweke barabarani dunia iwaone.
Tusiishie hapo tu.Tualike wananchi wenzetu kutoka vijijini waje na ndoa za maji yenye rangi ya maziwa ambayo ndio Maji yao wanakunywa miaka nenda rudi.Orodha ya waandamanaji ni ndefu kishenzi.
Sasa ili hayo yatokee na dunia ituelewe ndiposa alichokisema Mzee Butiku kinapata nafasi yake.Kwamba Civil Socities zishiriki "kupanga fujo hiyo" .Ndio kusema vyama hivi vinapaswa kuhamasisha watu waandamane.Kazi hii Mzee Butiku inatakiwa ianze sasa iendelee hadi 2025. Na ifikapo muda huo vyama vya kiraia vihamasishe watanzania tumpigie magoti Magufuli akubali kuwa Kiongozi wa Mpito wakati tunaendelea kutafuta Mtu sahihi wa kumrithi.Hii ndiyo kazi ambayo Mzee Butiku unapaswa kuifanya pamoja na vyama vya kiraia.Tumsaidie Raisi kwa staili hiyo.