BUTIKU: Vyama vya Kiraia vimsaidie Magufuli sasa na hata baada ya 2025.

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Kila mtu anamsaidia Raisi Magufuli kadri ya awezavyo.Mzee Butiku tumekusikia na tumekuelewa barabara.Kwamba viongozi wengine vikiwemo vyama vya kiraia vimsaidie Raisi katika vita hii ya kiuchumi ni jambo jema sana.Nilikwisha kushauri kuwa tunatakiwa kufanya aina ya fujo Fulani hivi ili dunia ielewe kuwa tumeumizwa sana na ushenzi wa hawa jamaa wanaojiita wawekezaji.

Nikisema fujo namaanisha tubebe wagonjwa wa Cancer wanaotaabika pale Ocean Road Hospital kwa sababu ya kukosa uwezo wa kupata matibabu tuandamane nao barabarani ili dunia ione jinsi wenzetu wanavyotaabika.

Tuchukue watoto wa shule za msingi wabebe matofali wanayokalia shuleni tena wakiwa wamevaa kaputula zao na sketi zilizochanika na kutoboka matakoni sababu ya kukwaruzika na mawe.Nasema tuandamane na watoto hao wakiwa hivyo dunia ione.

Kisha tubebe madreva bodaboda majeruhi wote kutoka MOI tuandamane nao wakiwa kwenye Wheel chairs.Hawa wengine wamepata ulemavu wa kudumu kwa sababu ya hospitali kukosa vifaa Tiba walivyofikishwa hospitalini.Tuwaweke barabarani dunia iwaone.

Tusiishie hapo tu.Tualike wananchi wenzetu kutoka vijijini waje na ndoa za maji yenye rangi ya maziwa ambayo ndio Maji yao wanakunywa miaka nenda rudi.Orodha ya waandamanaji ni ndefu kishenzi.

Sasa ili hayo yatokee na dunia ituelewe ndiposa alichokisema Mzee Butiku kinapata nafasi yake.Kwamba Civil Socities zishiriki "kupanga fujo hiyo" .Ndio kusema vyama hivi vinapaswa kuhamasisha watu waandamane.Kazi hii Mzee Butiku inatakiwa ianze sasa iendelee hadi 2025. Na ifikapo muda huo vyama vya kiraia vihamasishe watanzania tumpigie magoti Magufuli akubali kuwa Kiongozi wa Mpito wakati tunaendelea kutafuta Mtu sahihi wa kumrithi.Hii ndiyo kazi ambayo Mzee Butiku unapaswa kuifanya pamoja na vyama vya kiraia.Tumsaidie Raisi kwa staili hiyo.
 
Nyie watu mnataka watu wajiue sasa,2020 mie nategemea kuwa president na nimeshawekeza sana.
 
[HASHTAG]#RipotiYaKwanza[/HASHTAG]

Lissu: Tusihangaike na udongo, tuhangaike na mikataba na sheria mbovu za madini zilizotufikisha hapa. Tuangalie tulipojikwaa, tusiangalie tulipoangukia.

CCM: Lissu analinda wezi. Mikataba na sheria za madini hazina shida. Shida ipo kwenye udongo wenye makinikia. Tumeibiwa sana kwenye udongo. Hatukubali.

[HASHTAG]#RipotiYaPili[/HASHTAG]

JPM: Tumelogwa na nani? Watanzania tumeibiwa sana. Naagiza mikataba yote na sheria zote za madini zipitiwe upya.

CCM: Rais wetu mzalendo. Amefanya kazi kubwa sana. Tumuombee.!!

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Lugha ileile aliyoongea Lissu akaambiwa amehongwa, ndiyo aliyoongea JPM leo akaitwa mzalendo. Akili za CCM kama kifurushi cha jaza ujazwe .!
 
Kila mtu anamsaidia Raisi Magufuli kadri ya awezavyo.Mzee Butiku tumekusikia na tumekuelewa barabara.Kwamba viongozi wengine vikiwemo vyama vya kiraia vimsaidie Raisi katika vita hii ya kiuchumi ni jambo jema sana.Nilikwisha kushauri kuwa tunatakiwa kufanya aina ya fujo Fulani hivi ili dunia ielewe kuwa tumeumizwa sana na ushenzi wa hawa jamaa wanaojiita wawekezaji.

Nikisema fujo namaanisha tubebe wagonjwa wa Cancer wanaotaabika pale Ocean Road Hospital kwa sababu ya kukosa uwezo wa kupata matibabu tuandamane nao barabarani ili dunia ione jinsi wenzetu wanavyotaabika.

Tuchukue watoto wa shule za msingi wabebe matofali wanayokalia shuleni tena wakiwa wamevaa kaputula zao na sketi zilizochanika na kutoboka matakoni sababu ya kukwaruzika na mawe.Nasema tuandamane na watoto hao wakiwa hivyo dunia ione.

Kisha tubebe madreva bodaboda majeruhi wote kutoka MOI tuandamane nao wakiwa kwenye Wheel chairs.Hawa wengine wamepata ulemavu wa kudumu kwa sababu ya hospitali kukosa vifaa Tiba walivyofikishwa hospitalini.Tuwaweke barabarani dunia iwaone.

Tusiishie hapo tu.Tualike wananchi wenzetu kutoka vijijini waje na ndoa za maji yenye rangi ya maziwa ambayo ndio Maji yao wanakunywa miaka nenda rudi.Orodha ya waandamanaji ni ndefu kishenzi.

Sasa ili hayo yatokee na dunia ituelewe ndiposa alichokisema Mzee Butiku kinapata nafasi yake.Kwamba Civil Socities zishiriki "kupanga fujo hiyo" .Ndio kusema vyama hivi vinapaswa kuhamasisha watu waandamane.Kazi hii Mzee Butiku inatakiwa ianze sasa iendelee hadi 2025. Na ifikapo muda huo vyama vya kiraia vihamasishe watanzania tumpigie magoti Magufuli akubali kuwa Kiongozi wa Mpito wakati tunaendelea kutafuta Mtu sahihi wa kumrithi.Hii ndiyo kazi ambayo Mzee Butiku unapaswa kuifanya pamoja na vyama vya kiraia.Tumsaidie Raisi kwa staili hiyo.
Vyama vya kiraia vimsaidie arejee katiba ya tume ya Warioba
Kaogopa kusema yakiyokuwa moyoni mwake kaishia vysma vya kiraia vinsaidie
Katiba katiba katiba
 
Nyie watu mnataka watu wajiue sasa,2020 mie nategemea kuwa president na nimeshawekeza sana.

Endelea tu kuwekeza mkuu.Hiyo ndio afya.Tutaangalia muda ukifika uwekezaji wako kwa muda wote huo ulilenga nini.Ulilenga kuanzia pale JPM alipoishia na kusonga mbele tena kwa kasi sana au unakuwa umelenga kuturudisha nyuma kuanzia anapokuwa ameishia JPM.
 
Vyama vya kiraia vimsaidie arejee katiba ya tume ya Warioba
Kaogopa kusema yakiyokuwa moyoni mwake kaishia vysma vya kiraia vinsaidie
Katiba katiba katiba

Ni jambo jema kuwa na Katiba ya Warioba lakini pia imebainika shida ya nchi hii siyo ukosefu wa Sheria tu.Kwa mjibu wa Kamati ya Pili ya Raisi juu ya Suala la Madini ni kwamba baada ya Serikali kuuza hisa zake asilimia 15 ilikubaliwa na mwekezaji iwe inapata 100,000 kwa mwaka na vile vile ilipwe dola milioni 5 kwa hisa 5 ilizouza Serikali.Hadi leo hakuna makusanyo ya chochote kati ya hivyo viwili.Unafikiria hapo tatizo ni nini? Ni Kanuni,Sheria na taratibu au ni ukosefu wa Rasilimali watu mahiri na sahihi wa kusimamia hizo sharia na taratibu?
 
Hakuna muwekezaji aliyejileta hapa mwenyewe a kaamua kutuibia. Ni sisi wenyewe kwa uroho wa nafsi zetu tulipoamua kulipa azimio la arusha lililokuwa kama speed governor kwa viongozi tukaamua kuwaalika kwa sheria na mikataba mitamu mitamu ili wabebe kila alichokuwa amekihifadhi mwalimu kwa faida ya watanzania. Mara tu alipoondoka mwalimu nchi na rasilimali zote zikawa shamba la bibi. Hivi yule mtoto Vincent Kiboko yuko wapi? Kuna swali ninataka kumuuliza
 
Back
Top Bottom