Butiku: Sikufurahia ushindi wa Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Butiku: Sikufurahia ushindi wa Igunga

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by kupelwa, Oct 21, 2011.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]na Mwandishi wetu[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amekishambulia tena Chama Cha Mapinduzi (CCM), safari hii akidai kutofurahishwa na ushindi wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Igunga.
  Akizungumza juzi katika kipindi cha ‘Je, Tutafika’ kinachorushwa na kituo cha runinga cha Channel Ten, Butiku alidai kuwa CCM, ilimkera kwa kutumia mbinu chafu, vikiwemo ubabe, vitisho na rushwa ili kushinda nafasi hiyo.
  Alidai kuwa kitendo cha viongozi wa CCM kutumia vyombo vya dola kutisha watu, licha ya kuwa ni kibaya lakini pia kilikiuka misingi ya utawala bora, hivyo kinapaswa kukemewa.
  Kiongozi huyo na mwanachama wa siku nyingi wa CCM, alisema hakufurahia ushindi huo wa chama chake kwa vile ulipatikana kutokana na mbinu za udini, ukabila, matumizi makubwa ya fedha, kununua shahada, rushwa na vitisho.
  “Ziko dalili kubwa za wanasiasa wetu kufanya mikakati na viongozi wa dini ili kuwasaidia kueneza ujinga wa udini. Mimi nawaomba viongozi wa dini watusaidie kutuondoa kwenye ujinga huu na si wao kugeuka wachochezi,” alisema.
  Butiku alibainisha kuwa baadhi ya viongozi wa CCM ni wababaishaji na wabomoaji wa misingi ya uongozi aliyoiasisi Mwalimu Nyerere na viongozi wenzake.
  “Tuliyoyaona Igunga ni ujinga. Kule tulikuwa tunatafuta uongozi, sasa kama tumechaguliwa kwa rushwa, kutumia vitisho, udini, ukabila tunaweza kujivunia nini cha kuigwa na vizazi vijavyo kama hizi si dalili za viongozi wetu kubabaika na kubomoa misingi?” alihoji Butiku.
  Alisema misingi hiyo ndiyo tunu ya taifa na hivyo viongozi walipaswa kuonesha kwa vitendo kuwa wanaisimamia na kuifuata badala ya wao kugeuka wavunjaji.
  Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, alisema kuwa fukuto la udini lililojitokeza Igunga ni rasharasha na kwamba masika yake yataonekana katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
  Alisema hali ya nchi ni tete kutokana na CCM kushindwa kufanya vikao vya kujitathmini kwa mujibu wa ratiba ili kujua walipotoka, walipo na wapi wanakwenda.
  “Kwa mfano, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) toka uchaguzi mkuu mwaka jana hata huu mdogo wa Igunga imeshindwa kuwakamata watoa rushwa wa CCM licha ya wahusika kufanya hivyo wazi wazi. Hapa tunategemea umakini gani wa chama kusimamia misingi?” alihoji Bashiru.
  Aliongeza kuwa miaka 50 ya Uhuru kwa mtazamo wake imegawanyika mara mbili ambapo ile 25 ya Mwalimu Nyerere ilikuwa ya kujenga makuzi na misingi, wakati 25 ya warithi wake imekuwa ya
  porojo.

  source :TANZANIA DAIMA
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Tusubiri majibu ya Nape au Mkama. Hivi Makamba aliwaitaje hawa wazee wa Nyerere foundation?
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Taasisi hii inamdhalilisha mwalimu...
   
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,077
  Likes Received: 10,435
  Trophy Points: 280
  ukombozi unakaribia!!
   
 5. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Butiku ni miongoni mwa wa zee wachache sana waliobaki Chama cha mapinduzi. Wenzake wote wamehamia basi kubwa la Chama Cha Manyang'au ambacho kimeishika dola kwa sasa.
   
 6. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  MUNGU akupe maisha marefu kwa kubeba ujasiri wa kusema ukweli..........wape ukweli hao wanafiki.
   
 7. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee hajui tu vita anayopigana. Anadhani anapigana na wanachama wenzake, kumbe ni wapinzani wake wanaotumia kivuri cha nembo ya chama chake.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Butiku ungejitokeza kusema kabla ya siku ya Uchaguzi kwani haya yote unayoyasema yalikuwa yanajulikana kabla ya uchaguzi na yametokea kwenye chaguzi nyingine pia.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Akiunda Jumuhiya ya Wazee wa CCM, M/kiti - TAIFA asiwasahau hawa wazee kuwa ni miongoni mwa members
  • Sabodo
  • Butiku
  • Warioba
  • etc
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Watakuja kusema hapa Butiku anatafuta umaarufu
   
 11. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kila Mtu na maoni na mtazamo wake. Kwani madhambi hayo yanafanywa/yalifanywa na chama kimoja tu?
   
 12. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Hakuna mtu aliyefuatilia na kutathmini ukweli atapingana na butiku.Ni kweli katiba inatoa uhuru wa kutoa maoni , lakini haikuwa na maana ya kutoa maoni hasi yasiyokuwa ya kujenga.Maoni ya butiku ndo maoni ya waangalizi wengi wa uchaguzi ule.Leo kuna vifo vingi vimetokea kule igunga na wasiasa waligundua kuwa kuna genge limetayarishwa kufanya hivyo, lakini polisi hawajasema kitu.Ni ukweli usiopingika kuwa butiku anasema kwa masilahi ya umaa na si misimamo ya kupendela chama fulani.Ni vyema zaidi watanzania tukawa kama butiku kuzungumzia mstakabali wetu hasa masilahi ya umma.
   
 13. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  chambua, kivipi?kama huna hoja ya uchambuzi wa kisiasa , ni lazima kuchangia?
   
 14. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  nani aunde ?watu wajasiri wa kusema ukweli huwa hawapewi nafasi za kujenga nchia yao hasa kwa mfumo wa sasa.Nchi hii inawasomi na nawaadilifu sana , pia wenye hamu ya kuchangia nchia yao kimaendeleo, lakini hawapewi nafasi hizo.Sikweli kuwa TANZANIA hakuna waadilifu ,wapo lakini hawapewi nafasi
   
 15. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2011
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  tafadhali msimwamini huyo mzee ni mzee ambaye ameikula hii nchi wakati wa mwalimu yeye ndiye alibaeba mifuko ya pesa wakati wa safari na kugawa kiduchu kwa wenzake zingine ziliishia kwake sasa anakumbuka utamu wa ikulu sasa ndiyo anawashambulia akina jk wache wale nao, ni wakati wao .kwani tz ni shamba la bibi
   
 16. B

  BANNED 4EVER Member

  #16
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ungejua nini kinachoendelea ndani ya MWALIMU NYERE FOUNDATION!!! wala usingemsikiliza huyu mzee.
  siasa wengi wetu hatuziwezi
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Nyie hamjui kuwasoma watu na tabia zao, hakuna mtu mnafiki kama Butiku ! huyu ana hasira na serikali baada ya Taasisi ya mwalimu kuomba hela za mahitaji yao serikalini na kukataliwa
   
 18. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Hatuzungumzii majungu , tunazungumzia hoja zenye usitawi wa nchi na uchambuzi wa kina kwa masilahi na msitakabari wa nchi.Hilo lakunyimwa , mafungu na serikali , ni vyema utalitolea uthbitisho, lakini yeye alilosema lina uthibitisho na waangalizi wa uchaguzi huo wamelitolea maelezo ya uthibitisho huo.Je wewe kukumsikia magufuli kama waziri akitoa ahadi ya kujenga daraja lang'humbu?hili nalo linakubaliwa kwenye kampeni?huo ndo uthibitisho wa matumizi mabaya ya madaraka ya umma, kutoa ahadi kwenye kampeni kinyume na utaratibu.Funguka macho acha kutumiwa na mafisadi .
   
 19. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mkuu hakuna hasira hapa, kasema ukweli mtupu. Hayo yote yalitokea Igunga. Huna hoja hapa nenda kanye. Mbona WAMA wanapewa, wao wanafanya nini cha ziada ambacho Foundation ya Nyerere chini ya Butiku wanashindwa? Hizi asasi za wake za marais ni vichaka vya ufisadi, madawa ya kulevya na uzandiki tuu. Naona JK ana hasira sana na Jina hili la Nyerere sijui lilimfanyaje. Mbona Mzee wetu huyu ndiye aliyemtengenezea mazingira bora na akaja kuwa presida.

  Mungu ibariki Tz
   
 20. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  eeeH! haya uchafuzi kula pahala
   
Loading...