Butiku: Sikufurahia ushindi wa Igunga

Butiku ungejitokeza kusema kabla ya siku ya Uchaguzi kwani haya yote unayoyasema yalikuwa yanajulikana kabla ya uchaguzi na yametokea kwenye chaguzi nyingine pia.

Ni kweli kabisa, ila hapa nimtetee Butiku kidogo. Kwa mtu aliyesoma upepo, atajua kuwa uchaguzi wa Igunga uliwafanya viongozi wa CCM na Serikali kurukwa na akili. Walikuwa Obsessed na kushinda hasa ukizingatia kuwa ilikuwa Test No. 1 ya secretariet mpya ya CCM. Kwao wao kazi nzuri ni ushindi. Ukiwashambulia katika mission yao hiyo basi tarajia retarliations za kiwendawazimu.

Kwa uhakika Butiku anasimamia misingi ya baba wa Taifa. Baba wa Taifa aliishawahi kueleza kuwa 'Suala la wabunge ni suala la kuwaachia wananchi waamue wamtakaye', yeye alikuwa akitumia nguvu zake kuwashawishi wananchi wamchagulie RAIS ambaye atakuwa na uwezo wa kuipeleka Tanzania mbele (UCHAGUZI WA 1995). Unapoona Chama kikongwe kinakuwa tayari kutumia misingi ya dini, rushwa, mauaji, vitisho, na hata uwongo wa kuhatarisha usalama wa nchi ni dalili mbaya kwa chama hicho kuwa kimekosa watu wenye busara na hivyo hakistahili kuongoza nchi tena, maana wataipeleka kwenye maafa.

Ningekuwa mimi ni M/Kiti wa CCM Taifa ningevunja uongozi wote ulioshiriki katika kampeni za Igunga kwa lengo lilelile la kujivua gamba. Otherwise 2015 tutarajie more than Igunga. Ninashauri VYAMA VINGI VIFUTWE KABLA YA 2015
 
na Mwandishi wetu
amka2.gif

MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amekishambulia tena Chama Cha Mapinduzi (CCM), safari hii akidai kutofurahishwa na ushindi wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Igunga.
Akizungumza juzi katika kipindi cha ‘Je, Tutafika’ kinachorushwa na kituo cha runinga cha Channel Ten, Butiku alidai kuwa CCM, ilimkera kwa kutumia mbinu chafu, vikiwemo ubabe, vitisho na rushwa ili kushinda nafasi hiyo.
Alidai kuwa kitendo cha viongozi wa CCM kutumia vyombo vya dola kutisha watu, licha ya kuwa ni kibaya lakini pia kilikiuka misingi ya utawala bora, hivyo kinapaswa kukemewa.
Kiongozi huyo na mwanachama wa siku nyingi wa CCM, alisema hakufurahia ushindi huo wa chama chake kwa vile ulipatikana kutokana na mbinu za udini, ukabila, matumizi makubwa ya fedha, kununua shahada, rushwa na vitisho.
“Ziko dalili kubwa za wanasiasa wetu kufanya mikakati na viongozi wa dini ili kuwasaidia kueneza ujinga wa udini. Mimi nawaomba viongozi wa dini watusaidie kutuondoa kwenye ujinga huu na si wao kugeuka wachochezi,” alisema.
Butiku alibainisha kuwa baadhi ya viongozi wa CCM ni wababaishaji na wabomoaji wa misingi ya uongozi aliyoiasisi Mwalimu Nyerere na viongozi wenzake.
“Tuliyoyaona Igunga ni ujinga. Kule tulikuwa tunatafuta uongozi, sasa kama tumechaguliwa kwa rushwa, kutumia vitisho, udini, ukabila tunaweza kujivunia nini cha kuigwa na vizazi vijavyo kama hizi si dalili za viongozi wetu kubabaika na kubomoa misingi?” alihoji Butiku.
Alisema misingi hiyo ndiyo tunu ya taifa na hivyo viongozi walipaswa kuonesha kwa vitendo kuwa wanaisimamia na kuifuata badala ya wao kugeuka wavunjaji.
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, alisema kuwa fukuto la udini lililojitokeza Igunga ni rasharasha na kwamba masika yake yataonekana katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Alisema hali ya nchi ni tete kutokana na CCM kushindwa kufanya vikao vya kujitathmini kwa mujibu wa ratiba ili kujua walipotoka, walipo na wapi wanakwenda.
“Kwa mfano, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) toka uchaguzi mkuu mwaka jana hata huu mdogo wa Igunga imeshindwa kuwakamata watoa rushwa wa CCM licha ya wahusika kufanya hivyo wazi wazi. Hapa tunategemea umakini gani wa chama kusimamia misingi?” alihoji Bashiru.
Aliongeza kuwa miaka 50 ya Uhuru kwa mtazamo wake imegawanyika mara mbili ambapo ile 25 ya Mwalimu Nyerere ilikuwa ya kujenga makuzi na misingi, wakati 25 ya warithi wake imekuwa ya
porojo.

source :TANZANIA DAIMA

Hawa wanafiki wasipomtaja mnafiki mwenzao nyerere hawawezi kusema kitu ..akili mgaondo nendeni mkamuabudu kaburi huko..ala

Udini ni zao la nyerere until we admit that we can solve the problem.
 
Ni kweli kabisa, ila hapa nimtetee Butiku kidogo. Kwa mtu aliyesoma upepo, atajua kuwa uchaguzi wa Igunga uliwafanya viongozi wa CCM na Serikali kurukwa na akili. Walikuwa Obsessed na kushinda hasa ukizingatia kuwa ilikuwa Test No. 1 ya secretariet mpya ya CCM. Kwao wao kazi nzuri ni ushindi. Ukiwashambulia katika mission yao hiyo basi tarajia retarliations za kiwendawazimu.

Kwa uhakika Butiku anasimamia misingi ya baba wa Taifa. Baba wa Taifa aliishawahi kueleza kuwa 'Suala la wabunge ni suala la kuwaachia wananchi waamue wamtakaye', yeye alikuwa akitumia nguvu zake kuwashawishi wananchi wamchagulie RAIS ambaye atakuwa na uwezo wa kuipeleka Tanzania mbele (UCHAGUZI WA 1995). Unapoona Chama kikongwe kinakuwa tayari kutumia misingi ya dini, rushwa, mauaji, vitisho, na hata uwongo wa kuhatarisha usalama wa nchi ni dalili mbaya kwa chama hicho kuwa kimekosa watu wenye busara na hivyo hakistahili kuongoza nchi tena, maana wataipeleka kwenye maafa.

Ningekuwa mimi ni M/Kiti wa CCM Taifa ningevunja uongozi wote ulioshiriki katika kampeni za Igunga kwa lengo lilelile la kujivua gamba. Otherwise 2015 tutarajie more than Igunga. Ninashauri VYAMA VINGI VIFUTWE KABLA YA 2015

Mkuu umeanza vizuri na kwakweli hata maelezo yako yameniingia akilini vema. Ila hapo mwisho umeni"confuse" nikapoteza mwelekeo. Kama ccm imeonesha kushindwa kuongoza nchi kwa waliyoyafanya Igunga, iweje tena tuvunje vyama vingi kabla ya uchaguzi? Si ndio tunawakabidhi fisi bucha!? Tafakari kidogo mkuu, au unifafanulie hapo maana umeniacha mbali!
 
Hawa wanafiki wasipomtaja mnafiki mwenzao nyerere hawawezi kusema kitu ..akili mgaondo nendeni mkamuabudu kaburi huko..ala

Udini ni zao la nyerere until we admit that we can solve the problem.

we dogo unatetea sisiem kwa id ya Topical halafu unajifanya umehamia cdm kwa id ya mwita25! Hatudanganyiki!!?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom