kupelwa
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 1,090
- 454
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]na Mwandishi wetu[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]

MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amekishambulia tena Chama Cha Mapinduzi (CCM), safari hii akidai kutofurahishwa na ushindi wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Igunga.
Akizungumza juzi katika kipindi cha Je, Tutafika kinachorushwa na kituo cha runinga cha Channel Ten, Butiku alidai kuwa CCM, ilimkera kwa kutumia mbinu chafu, vikiwemo ubabe, vitisho na rushwa ili kushinda nafasi hiyo.
Alidai kuwa kitendo cha viongozi wa CCM kutumia vyombo vya dola kutisha watu, licha ya kuwa ni kibaya lakini pia kilikiuka misingi ya utawala bora, hivyo kinapaswa kukemewa.
Kiongozi huyo na mwanachama wa siku nyingi wa CCM, alisema hakufurahia ushindi huo wa chama chake kwa vile ulipatikana kutokana na mbinu za udini, ukabila, matumizi makubwa ya fedha, kununua shahada, rushwa na vitisho.
Ziko dalili kubwa za wanasiasa wetu kufanya mikakati na viongozi wa dini ili kuwasaidia kueneza ujinga wa udini. Mimi nawaomba viongozi wa dini watusaidie kutuondoa kwenye ujinga huu na si wao kugeuka wachochezi, alisema.
Butiku alibainisha kuwa baadhi ya viongozi wa CCM ni wababaishaji na wabomoaji wa misingi ya uongozi aliyoiasisi Mwalimu Nyerere na viongozi wenzake.
Tuliyoyaona Igunga ni ujinga. Kule tulikuwa tunatafuta uongozi, sasa kama tumechaguliwa kwa rushwa, kutumia vitisho, udini, ukabila tunaweza kujivunia nini cha kuigwa na vizazi vijavyo kama hizi si dalili za viongozi wetu kubabaika na kubomoa misingi? alihoji Butiku.
Alisema misingi hiyo ndiyo tunu ya taifa na hivyo viongozi walipaswa kuonesha kwa vitendo kuwa wanaisimamia na kuifuata badala ya wao kugeuka wavunjaji.
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, alisema kuwa fukuto la udini lililojitokeza Igunga ni rasharasha na kwamba masika yake yataonekana katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Alisema hali ya nchi ni tete kutokana na CCM kushindwa kufanya vikao vya kujitathmini kwa mujibu wa ratiba ili kujua walipotoka, walipo na wapi wanakwenda.
Kwa mfano, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) toka uchaguzi mkuu mwaka jana hata huu mdogo wa Igunga imeshindwa kuwakamata watoa rushwa wa CCM licha ya wahusika kufanya hivyo wazi wazi. Hapa tunategemea umakini gani wa chama kusimamia misingi? alihoji Bashiru.
Aliongeza kuwa miaka 50 ya Uhuru kwa mtazamo wake imegawanyika mara mbili ambapo ile 25 ya Mwalimu Nyerere ilikuwa ya kujenga makuzi na misingi, wakati 25 ya warithi wake imekuwa ya porojo.
source :TANZANIA DAIMA
[/TD]Akizungumza juzi katika kipindi cha Je, Tutafika kinachorushwa na kituo cha runinga cha Channel Ten, Butiku alidai kuwa CCM, ilimkera kwa kutumia mbinu chafu, vikiwemo ubabe, vitisho na rushwa ili kushinda nafasi hiyo.