Butiku: Rais tembo hatufai

Butiku: Rais tembo hatufai

By Assasyria3
“Tunachosema ni kwamba miiko ilikuwa inasema ukitaka kuwa rais utambue na uwe na imani kuwa watu wote ni sawa usiwe wewe ni tembo,” alisema Butiku: source: Mtanzania

Maneno haya ya Mzee Butiku (waliosoma Enzi za Kiingereza cha Cambridge), mimi wa shule za kata, nimetafsiri anaona kuna tatizo kubwa ktk nchi yetu ambalo hata watu kuliongelea wanasita/ogopa/gwaya n.k yanafanana na kamsemo ktk lugha ya Kiingereza ikiwa na maana :
an elephant in the room
you mean that there is an obvious problem or difficult situation that people do not want to talk about. The idiomatic expression also applies to an obvious problem or risk no one wants to discuss. Source: Cambridge Dictionary
 
Katibu Mkuu naye kawa kimya kupita maelezo. Hata kuonekana haonekani.

katibu mkuu akimuachia chama,basi,ccm mazishi yake saa nane,katibu mkuu ndiye pekee ndani ya ccm.anayeweza kumkoromea,wengine wameufyata kulinda ugali
 
Mbona asilimia kubwaya Watanzania mpaka keshi kutwa wengi wao bado wanamkubali sana Baba wa Taifa pamoja na mapungufu yake? Mwalimu hakuwa malaika lakini alikuwa kiongozi mzuri sana hakuwa fisadi wala mwizi kama hawa waliokuja baada yake, aliipenda Tanzania na Watanzania kwa moyo wake wote tofauti na hawa wanaojali matumbo yao kila kukicha hata mikataba ya nchi wanaisaini uvunguni wakiwa wamefunga pazia na kwa sauti za kunong'ona wakati wakisaini mikataba hiyo..

Hii nchi yetu hata malaika tutamkataa!
 
MAGUFULI I III PIGA KAZI BABA USIHOFU MANENO YA WALIMWENGU NDO WALIVYO...
 
Na JONAS MUSHI

DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesema kutokana na miiko iliyowekwa na mwasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julias Nyerere, mtu yeyote anayekuwa rais wa nchi lazima atambue watu wote ni sawa na “usiwe wewe ni rais tembo.”

Hayo aliyasema jana wakati akiwasilisha mada ya miiko ya uongozi katika kongamano la kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya TANU ya mwaka 1954 imani ya chama ilikuwa binadamu wote ni sawa, kila mtu anastahili heshima na kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa.

Alisema nchi ambayo mwalimu aliijenga ilikuwa na misingi ya “binadamu wote ni ndugu zangu” na kwamba msimamo kama huo aliuweka hata alipotoka nje ya mipaka ya Tanzania.

“Tunachosema ni kwamba miiko ilikuwa inasema ukitaka kuwa rais utambue na uwe na imani kuwa watu wote ni sawa usiwe wewe ni tembo,” alisema Butiku na kuongeza:

“Lazima utambue kuwa unatokana nao (watu) na lazima kiongozi huyo atambue kuwa anaongoza watu hivyo anapaswa kuwaongoza kwa heshima.”

Akizungumzia miiko ya uongozi, Butiku alikumbusha hoja ya kutenga siasa na biashara ambayo alisema imeonekana kupuuzwa na viongozi katika miaka ya hivi karibuni.

Alisema miiko ya uongozi ilikuwa ni pamoja na kiongozi lazima awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika shughuli zozote za ubepari.

Katika hilo aliwataka viongozi kuchagua ama kuwa kuwatumikia watu au kutafuta utajiri.

“Katika siasa za hivi sasa wanasiasa wote wanajitahidi sana kukataa kanuni hii na wamekuwa wakibabaisha. Msibabaishe,” alisisitiza Butiku.

Mbali na Butiku, naye Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mkama wakati akiwasilisha mada ya miiko ya uongozi alibainisha kuwa viongozi lazima wapatikane kwa haki na uwazi.

Alionya kuwa ni hatari kwa viongozi kupatikana kwa njia za vitisho, ujanja, ulaghai na rushwa na kwamba kufanya hivyo ni kupoteza sifa za uongozi.

“Asili ya uongozi ni watu na viongozi lazima wapatikane kwa haki na uwazi na si kwa njia za ujanja ujanja, vitisho, ulaghai na rushwa na inapokuwa hivyo tunapoteza sifa ya uongozi,” alisema Mkama.

Pamoja na hilo Mkama alipongeza kauli mbiu inayotumiwa na Rais Magufuli ya ‘Hapa Kazi tu’ akisema kiongozi lazima afanye kazi kwa kufuata utaratibu wa kisiasa uliowekwa.

“Watu wamekuwa wakitafsiri siasa vibaya lakini ukweli ni kwamba siasa ni namna ya kutengeneza utaratibu wa maisha na maamuzi ya kisiasa ndio yanayoijenga jamii,” alisisitiza.

Naye Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Philip Mangula, akiwasilisha mada ya ‘Viongozi na Maadili’ alisema kwa kiasi kikubwa chama chake kimekuwa kikizingatia maadili ya viongozi.

Alisema kwa sasa chama hicho chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli kinahakikisha kinatokomeza rushwa serikalini na katika chama hasa wakati wa uchaguzi.

“Katika mkutano Mkuu wa mwaka 2012 ambao ndio ulinichagua kuwa makamu mwenyekiti na nikapata uenyekiti wa kamati ya maadili, tuliazimia kuchukua hatua haraka kwa viongozi wala rushwa na ndio kazi anayofanya Rais Magufuli,” alisema Mangula.

Mangula ambaye amepewa jina la utani la ‘Mzee wa mafaili’ kutokana na timu yake kujihusisha na uchunguzi wa masula yote yanayohusu maadili hasa kwa wanachama wanaotaka uongozi kupitia CCM, alisema mafaili bado yanaendelea kurekodiwa na mwisho yatafunguliwa kwa kila atayetaka uongozi.

Alionya kuwa wapo watu ambao wameshaanza kutoa zawadi na misaada bila kuzingatia taratibu za chama kwa lengo la kutengeneza mazingira ya kupata uongozi katika uchaguzi ujao na kusisitiza kwamba “safari hii imekula kwao.”

Kauli hiyo ya Mangula inafanana na ile aliyoitoa Rais Magufuli Julai mwaka huu baada ya kukabidhiwa mikoba ya Uenyekiti wa chama hicho mjini Dodoma.

CHANZO: Mtanzania
 
Mtu yeyote atakayedharau wazee atajichimbia kaburi .
 
Mtu kuwa Rais tu anajiona yeye ndiye yeye dharau chungu nzima, vitisho kwa raia kila kukicha, wengine kuitwa mashetani na vila.za, kuwapuuza wananchi waliopatwa na maafa, kudharau katiba ya nchi na kutaka kujifanya yeye kama Mfalme vile na hata kutaka kudhibiti mijadala muhimu Bungeni vile atakavyo yeye!!!
Kweli Watanzania hatuhitaji Rais ambaye ni Tembo.

Mtu yeyote atakayedharau wazee atajichimbia kaburi .
 
Mbona asilimia kubwaya Watanzania mpaka keshi kutwa wengi wao bado wanamkubali sana Baba wa Taifa pamoja na mapungufu yake? Mwalimu hakuwa malaika lakini alikuwa kiongozi mzuri sana hakuwa fisadi wala mwizi kama hawa waliokuja baada yake, aliipenda Tanzania na Watanzania kwa moyo wake wote tofauti na hawa wanaojali matumbo yao kila kukicha hata mikataba ya nchi wanaisaini uvunguni wakiwa wamefunga pazia na kwa sauti za kunong'ona wakati wakisaini mikataba hiyo..
Unauzungumziaje msimamo wa Tundu Lisu kuhusiana na Nyerere?
 
Soma nilichoandika mimi halafu kasome msimamo wa Tundu Lissu kisha tafakari kwa kina na kufanya hitimisho lako. Mimi si bendera kufuata upepo na hivyo kukubali kila kinachosemwa na Tundu Lissu pamoja na kuwa namkubali sana kama kiongozi.

Na wewe si CCM mbona hujawahi kutamka haya yanayotamkwa na Butiku, Mwinyi na Jaji Warioba? KULIKONI? Umezibwa mdomo?

Butiku si ccm imekuaje tena? Au umeshahamia ccm kimya kimya? Maana hawa ndio wazee wetu!
 
Soma nilichoandika mimi halafu kasome msimamo wa Tundu Lissu kisha tafakari kwa kina na kufanya hitimisho lako. Mimi si bendera kufuata upepo na hivyo kukubali kila kinachosemwa na Tundu Lissu pamoja na kuwa namkubali sana kama kiongozi.
Bado hujajibu swali langu!
 
Na wewe si CCM mbona hujawahi kutamka haya yanayotamkwa na Butiku, Mwinyi na Jaji Warioba? KULIKONI? Umezibwa mdomo?
Sio lazima utamke hayo aliyotamka butiku ndio uonekane Mzalendo! Kila mtu ana namna yake ya kufikisha ujumbe pale anapoona inastahili! By the way! Hata Lowasa naye alisubiri awe mzee ndio akahamia chadema, tena baada ya kunyimwa fursa ya kugombea urais? So sio lazima kila kinachotamkwa kiwe kweli kwa aslimia zote! Mwenyewe pia kauli zako humu ni kama kinyonga! At least msimamo wangu haukuwahi kubadilika over the years huo ndio uanaume!
 
Power of words; sifa za tembo ni zipi? Isije ikawa sio matusi kumuita mtu tembo.
 
Back
Top Bottom