Butiku aionya CCM kuelekea uchaguzi 2015

Butiku aionya CCM kuelekea uchaguzi 2015

Alexandry Nemesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2014
Posts
1,508
Reaction score
590
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere,Joseph Butiku amekionya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa kipo hatarini kupoteza madaraka katika uchaguzi mkuu wa 2015 iwapo kitafanya makosa na kuendekeza ubinafsi na utawala wa kiimla unaotokana na utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.

Butiku ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba,Alisema kuwa iwapo chama hicho kitasahau kuwa kinaongoza nchi kwa mujibu wa katiba ya nchi ambayo sasa Watanzania wanataka iandikwe upya na kuendelea kukumbatia maovu kinaweza kuondolewa madarakani 2015.

Source Mwananchi toleo la leo Jumamosi

butiku+clip.jpg

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku

Na Exuper Kachenje, Mwananchi

Posted Julai19 2014 saa 10:20 AM Kwa ufupi
Butiku ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema kuwa iwapo chama hicho kitasahau kuwa kinaiongoza nchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo sasa Watanzania wanataka iandikwe upya na kuendelea kukumbatia maovu kinaweza kuondolewa madarakani.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa kipo hatarini kupoteza madaraka katika uchaguzi mkuu ujao, iwapo kitafanya makosa na kuendekeza ubinafsi na utawala wa kiimla unaotokana na utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.

Butiku ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema kuwa iwapo chama hicho kitasahau kuwa kinaiongoza nchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo sasa Watanzania wanataka iandikwe upya na kuendelea kukumbatia maovu kinaweza kuondolewa madarakani.

Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, Jumatano wiki hii katika mahojiano maalumu na gazeti hili ambapo alizungumzia mambo mbalimbali.

“…Kosa moja la msingi ni CCM kusahau misingi ya Katiba ya chama chao na Katiba ya nchi. Watanzania wengi wanaikubali Katiba ya CCM na Katiba ya nchi, lakini ambayo wanasema itazamwe upya, iandikwe Katiba Mpya,” alisema Butiku.

Huku akisisitiza, Butiku alisema:

Alifafanua kuwa hali hiyo itaikumba CCM kwa kuwa ndiyo kanuni ya maisha ya binadamu akisema:

“Vyama vyote tawala vilivyosahau masilahi ya wananchi wake, demokrasia, uhuru na haki, vikakumbatia uovu vinaanguka. Huo siyo utabiri wangu binafsi, bali historia itawahukumu.”

Butiku alitoa mfano akieleza: “Mfumo wa kibabe zaidi wa makaburu wa Afrika Kusini, uliangushwa na wasio na viatu. Nani anaweza kujenga ubabe wa sura kama ule wa makaburu, nani ataruhusu? Ni muhimu CCM nayo ijitazame.”

Rushwa

Alisema kuwa alipoondoka madarakani, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema taifa linanuka rushwa hali ambayo imeota mizizi hata sasa.

“…Leo rushwa ni kawaida, ni mfumo wa kuuza na kununua uongozi, kama taifa mkifika hapo ni hatari. Mkishanunua uongozi basi mmekwisha. Mkijenga mfumo huo, mnaondoa haki.

Ikiwa kura yako imekuwa biashara umekwisha, hakuna ushirikiano tena kati ya kiongozi aliyenunua nafasi na mwananchi. Hapo mnajenga kundi la viongozi la wafanyabiashara wa kura katika uchaguzi, mnajenga mfumo wa raia kuwa maskini.”

“Raia wakiuza haki yao na kununua hakutakuwa na taifa lenye utulivu. Wanunua kura wajue ni vita, siku moja wauza kura wataamua kuwaondoa nao watagoma kwa kuwa walinunua uongozi, hapo damu itamwagika, watu watauana.

Wanyonge hawapotezi haki ya unyonge wao, unaweza kuiangusha CCM…

huyu sasa kaisha kisiasa akalale
Mbona unakosa heshima wewe?Hivi unawezaje kumdharau mzee kama Butiku kwa kumwambia akalale kisa ameongea busara na maoni yake kuhusu mwelekeo wa siasa za CCM.Kwanini mnalewa kiasi hicho?Butiku penngine ni baba yako,hata pengine babu yako,lakini kwa kulewa sifa na posho za kifisadi uko radhi hata kumtukana au kumdhihaki kama ulivyofanya.Lakini sishangai,kuna mmoja wenu aliwahi hata kumdhihaki waziri mkuu mstaafu mzee jaji Warioba kwa kumwita mpumbav, kwenye radio moja hapa jijiini kisa tu baba anamadaraka makubwa.
 
Hata wafanye kufa kwao lazma "intarahamwe"
 
Butiku,warioba,salimu ahmed salim wameleta mfumo wa katiba mpya huo maksudi kuimaliza magamba,na kweli wanakufa 2015 magamba hawana pakutokea kupitia katiba mpya wamekwisha
 
Wana wa maccm yeyote mwenye akili timamu na kuikosoa ccm basi wao huwaporomoshea matusi tu. Yani kila anaye ishabikia ccm lazma awe tahira na msukule wa mvunguni cjui kwanini hawawez kujikomboa.
 
kiukweli kama kuna fair game intarahamwe wanang'oka,luboreshe daftari tu
 
Ngoja mipepo ya ccm iwapande uone watakavyokuja kuharisha hapa tusubiri kidogo tu.
 
Ngoja mipepo ya ccm iwapande uone watakavyokuja kuharisha hapa tusubiri kidogo tu.

Well said kamanda, yani haya maccm yakishapandisha mapepo yao hayajui cha mkubwa wala mtoto ni kutukana tu.
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere,Joseph Butiku amekionya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa kipo hatarini kupoteza madaraka katika uchaguzi mkuu wa 2015 iwapo kitafanya makosa na kuendekeza ubinafsi na utawala wa kiimla unaotokana na utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.

Butiku ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba,Alisema kuwa iwapo chama hicho kitasahau kuwa kinaongoza nchi kwa mujibu wa katiba ya nchi ambayo sasa Watanzania wanataka iandikwe upya na kuendelea kukumbatia maovu kinaweza kuondolewa madarakani 2015.

Source Mwananchi toleo la leo Jumamosi

ccm imeshakufa
 
Huu ndio ukweli tukisema sisi unasikia nichadema sasa wamesema wao wenyewe sijui lumumba watakuja na lipi tena
 
Hawa wazee kuna kitu wanaona nadhani wangesikilizwa!!!!!

hawa wazee hawasaminiki kabisa ccm ametukanwa mzee warioba na kamati yake bila kujali elimu zao, umri, uzoefu mapepo yakiwqpanda ccm ni kutukana tu hawa wazee kama Warioba, Ahamed Salim,
 
hawa wazee hawasaminiki kabisa ccm ametukanwa mzee warioba na kamati yake bila kujali elimu zao, umri, uzoefu mapepo yakiwqpanda ccm ni kutukana tu hawa wazee kama Warioba, Ahamed Salim,
Labda ni kundi la kujifunza kwa njia ngumu!!!!
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere,Joseph Butiku amekionya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa kipo hatarini kupoteza madaraka katika uchaguzi mkuu wa 2015 iwapo kitafanya makosa na kuendekeza ubinafsi na utawala wa kiimla unaotokana na utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.

Butiku ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba,Alisema kuwa iwapo chama hicho kitasahau kuwa kinaongoza nchi kwa mujibu wa katiba ya nchi ambayo sasa Watanzania wanataka iandikwe upya na kuendelea kukumbatia maovu kinaweza kuondolewa madarakani 2015.

Source Mwananchi toleo la leo Jumamosi

Butiku baba,sikia kawimbo haka wape wape maccm vidonge vyao wakimeza wakitema shauri zao, na huu ndo utabiri wa mwisho kwa maccm lazima waachie ikulu kwa sanduku la kula 2015 wapende wasipende.
 
Back
Top Bottom