Bustani ya 'Eden' ipo nchi gani?

Bustani ya 'Eden' ipo nchi gani?

jamani wana israel walitoka misri kuelekea kanaani.
kanaani ni wapi?
 
Ni kweli jf imekuwa ya ajabu na maswali fulani hebu umiza kichwa soma genesis 2:10 labda utapata hint
Ila kila mtu anasema lake now days wengine wanakwambia Ilikuwa ngorongoro,wengine olduvai george etc ndomana bakini nkachomekea koromije

Ova
Kama una jibu lilio straight si unasema tu? Kama kila mtu angekuwa anajua kila kitu hii forum ingekuwa haina maana kabisa.
 
Bustani ya Eden ilikuwa katika nchi ya IRAQ kati ya mito ya Tigris na Euphret. Humo walikaa Adam na Hawa ambao yamkini walikuwa Waarabu kwa sababu ndipo walipoumbiwa. Kwa hiyo watu wote duniani chimbuko lao ni Waarabu.Hata hivyo haijulikani ni tarehe gani watu walianza kugawanyika na kuwa mataifa mengi tofauti, kama vile Waafrika,Wazungu,Wachina na wengineo.Historia nayo inasema mtu wa kale kabisa alipatikana katika bara la Afrika.Kwa hiyo inamaanisha Adam na Hawa walitoroka Uarabuni na kuja kufia Africa.Ukweli huu ndio unaomfanya Mwarabu kuwa na imani kuwa hata Mungu ni wa kwao na wala hawachangii na taifa lolote."Hakuna Mungu ila ALLAH" Allah ni Mungu wa Waarabu tu.
 
Bustani ya Eden ilikuwa katika nchi ya IRAQ kati ya mito ya Tigris na Euphret. Humo walikaa Adam na Hawa ambao yamkini walikuwa Waarabu kwa sababu ndipo walipoumbiwa. Kwa hiyo watu wote duniani chimbuko lao ni Waarabu.Hata hivyo haijulikani ni tarehe gani watu walianza kugawanyika na kuwa mataifa mengi tofauti, kama vile Waafrika,Wazungu,Wachina na wengineo.Historia nayo inasema mtu wa kale kabisa alipatikana katika bara la Afrika.Kwa hiyo inamaanisha Adam na Hawa walitoroka Uarabuni na kuja kufia Africa.Ukweli huu ndio unaomfanya Mwarabu kuwa na imani kuwa hata Mungu ni wa kwao na wala hawachangii na taifa lolote."Hakuna Mungu ila ALLAH" Allah ni Mungu wa Waarabu tu.
Hakuna Mungu ila Allah.
Hii sentensi inanipa tabu sana,
Kwanini isisemwe tu kuwa
Allah ndiye Mungu. au
Allah ni Mungu apaswaye kuabudiwa.

Sentensi hiyo kimuundo lazima ikae hivi.
Hakuna Mumgu, ila Allah.
Haiwezi tu kusomwa mojakwamoja
Hakuna Mungu ila Allah.
Lazima iwe na kituo baada ya neno Mungu.

Labda ni muundo wa lugha ya Kiarabu. Ila kama inaandikwa kwa Kiswahili inabidi Syntax yake ikae Kiswahili pia ili ilete Semantic ya Kiswahili.

La sivyo inaleta mkanganyiko.
 
Bustani ya Mungu ilikuwa mahali ambapo kuna nchi ijulikanayo kama IRAQ. ile mito 4 yaan gihon,hedekeli ,frati na mwingine ipo kule. mwan 2:10 -14.
 
Nikijua ilipo hakika kwa garama yoyote nitakwenda
 
Bustani ya Adeni ilikuwa nchi ya Irak.
Kwani ndio kwenye mito iliyokuwa inatumika kumwagilia bustani hiyo.
Mito hiyo ni, Pishoni, wenye dhahabu, Gihoni, unaozunguka nchi ya Kushi, Hidekeli anaopita hadi Ashuru, na mto Frati ambao uko Irak hadi hivi leo.

Ref, Mwanzo 2 : 8 - 15
 
Kwa nini watu wana shaka kuhusu jambo hilo? Huenda falsafa ilichangia kuwapo kwa shaka hizo. Kwa karne nyingi, wanatheolojia walikuwa wakifikiria kuwa bustani ya Mungu bado ilikuwa mahali fulani. Hata hivyo, kanisa liliathiriwa na wanafalsafa Wagiriki kama Plato na Aristotle, walioamini kuwa hakuna kitu kikamilifu duniani. Ukamilifu ungeweza kupatikana mbinguni pekee. Kwa hiyo, wanatheolojia wakakata kauli kuwa lazima Paradiso ya kwanza iwe ilikuwa karibu na mbinguni.* Wengine walisema kuwa bustani hiyo ilikuwa juu ya mlima mrefu sana hivi kwamba haingeweza kuathiriwa na dunia iliyopotoka; wengine walisema ilikuwa katika Ncha ya Kaskazini au Ncha ya Kusini; nao wengine walisema ilikuwa karibu na au juu ya mwezi. Haishangazi kuwa simulizi kuhusu bustani ya Edeni lilianza kuonekana kama jambo la kuwaziwa tu. Wasomi fulani wa kisasa wanasema kuwa habari kuhusu mahali ambapo Edeni ilikuwa ni upuuzi mtupu, wakisisitiza kuwa hakujawahi kuwapo na mahali kama hapo.

Hata hivyo, Biblia haielezi kuhusu bustani ya Edeni kwa njia hiyo. Katika Mwanzo 2:8-14, tunajifunza mambo kadhaa kuhusu eneo hilo. Bustani hiyo ilikuwa mashariki ya eneo linaloitwa Edeni. Maji katika bustani hiyo yalitoka katika mto ambao ulikuwa chanzo cha mito minne. Majina ya mito hiyo yote minne yanatajwa na pia maelezo mafupi kuhusu mahali ilikoelekea. Wasomi wengi wametamani sana kujua habari kuhusu eneo la Edeni, hivyo wengi wao wametumia sehemu hii ya Biblia kujaribu kutafuta eneo hilo la kale liko mahali gani. Hata hivyo, wasomi hao wametoa maoni mengi tofauti-tofauti kuhusu eneo hilo. Je, hilo linamaanisha kuwa maelezo halisi kuhusu eneo la Edeni, bustani hiyo, na mito yake ni uwongo au ni hadithi tu?

Wazia: Matukio ya simulizi la bustani ya Edeni yaliyotokea miaka 6,000 hivi iliyopita. Musa ndiye aliyeandika simulizi hilo, na huenda alitumia masimulizi yaliyopitishwa kwa mdomo au hata maandishi fulani yaliyokuwapo wakati huo. Hata hivyo, Musa aliandika simulizi hilo miaka 2,500 hivi baada ya matukio hayo. Tayari matukio katika Edeni yalikuwa historia ya kale. Je, baada ya karne nyingi kupita, huenda alama hizo kuu kama mito imebadili mikondo yake? Uso wa dunia unabadilika kila mara. Eneo ambapo bustani ya Edeni ilikuwa linaathiriwa sana na matetemeko ya ardhi—asilimia 17 ya matetemeko yote duniani, yanatukia katika eneo hilo. Katika maeneo kama hayo, mabadiliko katika uso wa dunia ni jambo la kawaida. Zaidi ya hayo, huenda Gharika ya siku za Noa ilibadili uso wa eneo hilo katika njia ambazo hatuwezi kuzielewa leo.*

Hata hivyo, kuna mambo machache ya hakika tunayojua: Simulizi la kitabu cha Mwanzo linataja kuwa bustani ya Edeni ilikuwa mahali halisi. Mito miwili kati ya mito minne inayotajwa katika simulizi hilo—Efrati na Tigri, au Hidekeli—bado ipo hadi leo, na baadhi ya vyanzo vyake viko karibu-karibu. Simulizi hilo linataja majina ya maeneo ambapo mito hiyo ilipitia na hata inataja kihususa maliasili zinazojulikana sana katika eneo hilo. Habari hizo ziliwasaidia Waisraeli wa kale waliosoma simulizi hilo kuelewa mambo mengi.
 
aiswe..ndo kulikua na maziwa na asali?
Ndio, waliwakuta wapalestina hapo Israel wakiwa na Ng'ombe nyingi tu. Na pia kulikuwa na msitu wenye nyuki wengi na asali tele.
Pitia vitabu vya historia ya Mashariki ya Kati utaona.
 
Back
Top Bottom