Bustani ya Eden ilikuwa wapi?

Bustani ya Eden ilikuwa wapi?

WanaJamii,

Kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na huruma kwa kufika siku ya leo. Nimeona leo tuweze kuelemishana kuhusu biblia na maandiko matakatifu.

Mwenyezi Mungu anasema, watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa. Kusoma biblia ni sehemu ya kujua mambo na kumjua uweza na utukufu wake Mwenyezi Mungu muumbaji.

Swali la leo, ningependa kujua bustani ya Eden ilikuwa wapi katika ulimwengu wa leo? Kwa kifupi tu naweza kusema, wazungu wamepotosha sana khusu hili na kuhusu image halisi ya Mungu wetu pamoja alituumba kutokana na mfano wake; lakni Mungu anaonekana ni mtu mweupe tu.

Kwahyo na mambo mengine nahisi yatakuwa yamepotoshwa kuhusu bibilia tofauti na wenzangu waislam ambao wao vitabu vyao vimebaki kama vilivyo na hadithi zao hazina utofauti na bibilia, tofauti yetu mimi sijui ni wapi!

Hivyo nafungua majadala tujuzane ni wapi bustani ilikuwepo na tutazidi kuulizana maswali pale utata unapokuwa.

Nawakaribisha waislam pia maana wengi wao wanao ufahamu wa kwenye biblia na naomba huu mjadala uwe wa amani..
Bustani ya edeni ni Mwili wa mwanadamu, na tunda lililokuwa katikati ya bustani ni Papuchi na dushe full stop!! baada ya adamu na hawa kugegedana ndo wakaona raha utamu, ndo wakawa wamefunguka akili. before hawakuwa kamilifu. we kaa muda mrefu bila kugegeda au kugegedwa uone unakuwa kama chizi. ndo ilivokuwa kwa adamu na hawa
 
Chosen generation endelea na mawazo mazuri.
Shalom, naamini tu wazima. Naomba niendelee kuchangia kidogo mada hii.

Naomba tujikumbushe kidogo maana ya Edeni au Adeni kutoka katika post ya nyuma; Hili ni neno la Kiebrania likimaanisha "delight/beatiful place/paradise" au sehemu nzuri na ya kupendeza mno.

Maandiko yanasema "Hapo Mwanzo Mungu aliumba Mbingu na nchi." - Mwanzo 1:1 ... Maandiko yanaendelea kusema, "Kila kitu katika nchi/dunia kilikuwa kinavutia sana. Dunia ilikuwa sehemu nzuri, na yenye kupendeza sana kiasi cha Mungu kuifananisha na "Bustani nzuri sana." Sote twajua namna bustani zinavyopendeza.

"Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya." - Mwanzo 2:8

Ukisoma hiyo verse hapo juu tunaona, kuwa Edeni ilikuwa eneo kubwa, na ndani yake kulikuwa kuna bustani. Hii ni parable km nilivyosema hapo awali ... Issue sio kwamba kulikuwa na bustani as bustani bali Uzuri wa Dunia ulifananishwa na "bustani nzuri sana."

Baada ya dhambi dunia/Edeni iliharibiwa ... Na Mungu ameahidi kuifanya tena dunia kama Edeni/sehemu ya kuvutia, amani & kupendeza sana.

Nabii Isaya anapata maono namna wanyama & wanadamu walivyokuwa wanaishi & wataishi tena hivyo katika Dunia/Edeni ijayo ... Haya ndio yalikuwa maisha ya dunia ya awali isiyokuwa na uasi, kulikuwa na amani, upendo, na urafiki miongoni mwa viumbe;Uasi ulileta uadui.

"Mbwa-mwitu alikaa/atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui alilala/atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono walikuwa/watakuwa pamoja, na mtoto mdogo aliwaongoza/atawaongoza, Ng’ombe na dubu walilisha/watalisha pamoja; watoto wao walilala/watalala pamoja; na simba alikul/atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye alicheza/atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira..." - Isaya 11:6-9

Hebu tuangalie hii;

“Tena neno la BWANA, na kusema, Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie Bwana MUNGU asema hivi; ... Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu;kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamasi, na dhahabu;kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako;katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto..." - Ezekieli 28:11-13

Nabii Ezekieli anatuambia hapo juu kuwa, Mfalme wa Tiro/Shetani alikuwa katika bustani ya Adeni (Dunia) katika wakati fulani, lakini pia alikuwa katika Mlima wa Mungu (Mbingu) kwa wakati fulani.

Ukisoma historia, Tiro ulikuwa mji unaopatikana mashariki mwa pwani ya bahari ya mediteranean; hivyo mfalme wake asingekuwa anaishi ndani ya bustani ya Adeni.

Huu ni ufunuo au fumbo/parable. Ufunuo huu unatufundisha nini? Kuwa shetani (mfalme wa Tiro) hakuwa anaishi Edeni, ila aliingia Edeni kama mgeni kwa kuchukua umbo la nyoka, aliyekuwa anaishi Edeni.

Ukisoma Waebrania 13:2 inasema, “…wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.” Hii inatuonyesha kuwa malaika wote kama ilivyokuwa kwa shetani wana uwezo wa kujibadlisha kwenye maumbo tofauti. (Soma kisa cha Baalamu, punda na malaika ... Hesabu 22)

Ezekieli anachotuambia ni kuwa shetani hakuwa anaishi Adeni, hivyo ili aingie Adeni ilimbidi ajibadilishe na kuwa mfano wa kiumbe kimojawapo kilichokuwa kinapatikana bustanini Adeni (ambaye alimchagua nyoka), kwani angeingia kwa sura na umbo lake Adamu na mkewe Eva wangemtambua, na huo uwezo wa kubadilika na hata kuwa “invisible” ni sifa ya malaika wote (Nimeelezea katika somo lingine)

Kwa hiyo wapendwa tunapojadili haya, lazima tujue kuwa mwandishi wa kitabu hiki hakuwepo kipindi cha uumbaji bali alipata Ufunuo. Na ufunuo ni mpana. Bustani hapa, sio kama bustani tunayoijua bali imetumika kuelezea sifa bainifu ya dunia ile.

Julize! Ni bustani kubwa kiasi gani iliweza kubeba wanyama wote na binadamu? Tunaposema "Mungu aliweka makerubi kuilinda mwanadamu asiingie tena" ina maana gani? Kumbe ipo, wapi?! ... Soma kitabu cha Ufunuo kuhusu hiyo dunia ilipo.

Watu wengine hupotosha kuwa tunda walilokula Adam na mkewe ni tendo la ndoa. Kuwa Mungu aliwazuia kufanya tendo la ndoa ...Huu ni upotoshaji mkubwa.

"Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi." -
Mwanzo 1:28

Je! Watu watazaa bila tendo la ndoa?! Hapana, Hawa walikuwa mke na mume.

Hapa, Mungu aliweka sheria kwa kutumia mfano wa mti wenye matunda. Hii inatufundisha kuwa, Mungu alikuwa anawajaribu wanadamu kuhusu "Utii/Obedience."

"Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika." - Mwanzo 2:16-17

Kama ilivyokuwa kwa viumbe wengine wa mbinguni, Mungu aliwawekea wanadamu taratibu na sheria za kufuata. Mfano mmoja wapo ni "Kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya." Lakini shetani baada ya kuasi amri ya Mungu, alitupwa Duniani/Edeni (Ufununo 12:7...) na tunamwona akiingia kwa umbo la nyoka ... Nyoka ni symbol inayotambulisha uwerevu na ujanja. Na alifanikiwa kuwadanganya wanadamu na wao wakaasi amri ya Mungu na kumkasirisha. They disobeyed Him & listened to satan.

Mungu akubariki, naomba niishie hapa kwa leo.
 
Bustani ya Edeni ni "biblical parable" iliyotumika to describe the "ancient beatiful earth" kabla ya uasi wa Ibilisi na then wanadamu

Kwa Kiebrania neno "Adeni/Edeni" linamaanisha "sehemu nzuri na yenye kuvutia mno." Kutokana na uzuri huo, dunia ilifananishwa na bustani. Sote twajua namna bustani zinavyopendeza na zilivyo sehemu za utulivu na amani.

Kumbuka mwandishi wa kitabu cha Mwanzo, Musa hakuwepo kipindi cha uumbaji ila alipata maono kutoka kwa Mungu. Kama ilivyo kwa kitabu cha Ufunuo wa Yohana, Danieli, Ezekieli, Zekaria nk, kitabu cha Mwanzo kina portions za apocalyptic writings (mafumbo, alama, namba nk). Kwa mfano: Tunda la mti wa katikati, mti wa ujuzi wa mema na mabaya, mti wa uzima, nyoka nk... Haya ni sehemu ya mafumbo hayo.

Jiulize kama Edeni ingekuwa ni sehemu moja duniani, iko wapi sasa? Mungu alipowafukuza watu kutoka Edeni ile na kuweka walinzi alimaanisha nini?

Nikipata muda nitakuja kuelezea.
It is not a Biblical parable. It is real. Halafu kwa bahati mbaya sana wala husemi kwa mtazamo. Acha kupotosha maandiko.
 
*Naomba kuuliza maswali yafuatayo*

Hivi hiyo bustani bado ipo?
Kama ipo je ipo nchi gani?
Na je Adam na Eva ndio walikuwa binadam wa kwanza? Mbona hii inapongana na History ya darasani?
 
*Naomba kuuliza maswali yafuatayo*
Hivi hiyo bustani bado ipo?
Kama ipo je ipo nchi gani?
Na je Adam na Eva ndio walikuwa binadam wa kwanza? Mbona hii inapongana na History ya darasani?
Dah..ukikua utakuja kujua kwamba kila kitu hapa duniani kinagonganga na kingine..yote kwa sababu ya vitu vinavyoitwa KODI/SADAKA/ZAKA🙂
 
Maswali nzuri sana mkuu ESPIRIT,

•Hivi hiyo bustani bado ipo?

Inasemeknna kuwa hiyo bustani ilikuwepo nchini Iraq ingawa sijui kama mpaka sasa hivi watu wa pale watakuwa wanalichukulia hilo kuwa ni bustani ya edeni kama inavyoelezwa kwenye biblia.

Kwa upande mwingine kuna watu wengine wanakataa kwa hoja nzito kuwa hapajawahi kuwa na eneo kama hilo eti ni upuuzi mtupu kabisa.
 
Back
Top Bottom