Bustani ya Eden ilikuwa wapi?

aminiusiamini

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,577
2,221
WanaJamii,

Kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na huruma kwa kufika siku ya leo. Nimeona leo tuweze kuelemishana kuhusu biblia na maandiko matakatifu.

Mwenyezi Mungu anasema, watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa. Kusoma biblia ni sehemu ya kujua mambo na kumjua uweza na utukufu wake Mwenyezi Mungu muumbaji.

Swali la leo, ningependa kujua bustani ya Eden ilikuwa wapi katika ulimwengu wa leo? Kwa kifupi tu naweza kusema, wazungu wamepotosha sana khusu hili na kuhusu image halisi ya Mungu wetu pamoja alituumba kutokana na mfano wake; lakni Mungu anaonekana ni mtu mweupe tu.

Kwahyo na mambo mengine nahisi yatakuwa yamepotoshwa kuhusu bibilia tofauti na wenzangu waislam ambao wao vitabu vyao vimebaki kama vilivyo na hadithi zao hazina utofauti na bibilia, tofauti yetu mimi sijui ni wapi!

Hivyo nafungua majadala tujuzane ni wapi bustani ilikuwepo na tutazidi kuulizana maswali pale utata unapokuwa.

Nawakaribisha waislam pia maana wengi wao wanao ufahamu wa kwenye biblia na naomba huu mjadala uwe wa amani..
 
WanaJamii,

Kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na huruma kwa kufika siku ya leo.Nimeona leo,tuache siasa za magufuli kidogo na tuweze kuelemishana ni kuhusu biblia na maandiko matakatifu.
Mwenyezi Mungu anasema,watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa.Kusoama biblia ni sehemu ya kujua mambo na kumjua uweza na utukufu wake Mwenyezi Mungu muumbaji.

Swali la leo,ningependa kujua bustani ya eden ilikuwa wapi katika ulimwengu wa leo.Kwa kifupi tu naweza kusema,wazungu wamepotosha sana khusu hili na kuhusu image halisi ya Mungu wetu pamoja alituumba kutokana na mfano wake;lakni Mungu anaonekana ni mtu mweupe tu.Kwahyo na mambo mengine nahisi yatakuwa yamepotoshwa khusu bibilia tofauti na wenzangu waislam ambao wao vitabu vyao vimebaki kama vilivyo na hadithi zao hazina utofauti na bibilia,tofauti yetu mimi sijui ni wapi.

Hivyo nafungua majadala tujuzane ni wapi bustani ilikuwepo na tutazidi kuulizana maswali pale utata unapokuwa.Nawakaribisha waislam maana wengi wao wanao ufahamu wa kwenye biblia na naomba huu mjadala uwe wa amani?

we maku unausingiz kakojoe ukalale
 
" ;lakni Mungu anaonekana ni mtu mweupe tu."

mkuu unausingizi?!

" tofauti yetu mimi sijui ni wapi." inasemekana bangi inaisha baada ya muongo mmoja, hili ni kweli?
 
WanaJamii,

Kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na huruma kwa kufika siku ya leo.Nimeona leo,tuache siasa za magufuli kidogo na tuweze kuelemishana ni kuhusu biblia na maandiko matakatifu.
Mwenyezi Mungu anasema,watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa.Kusoama biblia ni sehemu ya kujua mambo na kumjua uweza na utukufu wake Mwenyezi Mungu muumbaji.

Swali la leo,ningependa kujua bustani ya eden ilikuwa wapi katika ulimwengu wa leo.Kwa kifupi tu naweza kusema,wazungu wamepotosha sana khusu hili na kuhusu image halisi ya Mungu wetu pamoja alituumba kutokana na mfano wake;lakni Mungu anaonekana ni mtu mweupe tu.Kwahyo na mambo mengine nahisi yatakuwa yamepotoshwa khusu bibilia tofauti na wenzangu waislam ambao wao vitabu vyao vimebaki kama vilivyo na hadithi zao hazina utofauti na bibilia,tofauti yetu mimi sijui ni wapi.

Hivyo nafungua majadala tujuzane ni wapi bustani ilikuwepo na tutazidi kuulizana maswali pale utata unapokuwa.Nawakaribisha waislam maana wengi wao wanao ufahamu wa kwenye biblia na naomba huu mjadala uwe wa amani?
umesigina katiba,kama ulitaka watu wa kada fulani wakujibu usingeuliza huku
 
Tafuta katika ramani ulipo mto Tigris na Euphrates then ndo bustani ya eden ilikua hapo, kwa akili ya makisio, lakini kumbuka ghalika kuu ya wakati wa noah ilibadilisha sana jografia ya mito na maziwa, kwa hiyo si rahisi kujua kama kweli ile mito ya wakati eden ndo hii ya sasa pale Iraq.

Pia kumekuwa na mabadiliko makubwa sana ya hali ya hewa, kumbuka hata lilipo jangwa la SAHARA kwa sasa zamani ilikuwepo bahari, pia hata kule antactica zamani palikuwa ni green vegetation.

Kwa kifupi wana historia mpaka sasa wameshindwa kujenga hoja kuwa ilipo tigris na Euphrates ndo hasa ilipokuwa eden zamani, by the way inakosekana mito miwili mingine (pishon na gihon) ili kukamilisha puzzle, so its a mystery..

Lakini kama hutaki kusumbua kichwa then bustani ilikuwa Iraq!
 
Last edited:
Bustani ya Edeni ni "biblical parable" iliyotumika to describe the "ancient beatiful earth" kabla ya uasi wa Ibilisi na then wanadamu

Kwa Kiebrania neno "Adeni/Edeni" linamaanisha "sehemu nzuri na yenye kuvutia mno." Kutokana na uzuri huo, dunia ilifananishwa na bustani. Sote twajua namna bustani zinavyopendeza na zilivyo sehemu za utulivu na amani.

Kumbuka mwandishi wa kitabu cha Mwanzo, Musa hakuwepo kipindi cha uumbaji ila alipata maono kutoka kwa Mungu. Kama ilivyo kwa kitabu cha Ufunuo wa Yohana, Danieli, Ezekieli, Zekaria nk, kitabu cha Mwanzo kina portions za apocalyptic writings (mafumbo, alama, namba nk). Kwa mfano: Tunda la mti wa katikati, mti wa ujuzi wa mema na mabaya, mti wa uzima, nyoka nk... Haya ni sehemu ya mafumbo hayo.

Jiulize kama Edeni ingekuwa ni sehemu moja duniani, iko wapi sasa? Mungu alipowafukuza watu kutoka Edeni ile na kuweka walinzi alimaanisha nini?

Nikipata muda nitakuja kuelezea.
 
unaonaje kwa kutumia hii adea yako mtu akisema ghalika haikuwepo?? au sodoma na ghomora hazikuwepo ni biblical parables???
 
Nakataa jinsi mdau alivyosema 'Eden' ni mafumbo ya kibiblia.Biblia imegawanyika katika sehemu nyingi.mf historia,nyimbo na injili.hizi ni baadhi tu. Edeni ilikuepo hapa duniani ila ni sehemu inakokutanikia mito minne,yaan hiyo ephrats,Tigrits n.k eneo hili linapatikana mesopotania ya zaman,tafuta kwa sasa ni Nchi gani.Baada ya gharika maumbile ya dunia yalibadilika.
 
WanaJamii,

Kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na huruma kwa kufika siku ya leo.Nimeona leo,tuache siasa za magufuli kidogo na tuweze kuelemishana ni kuhusu biblia na maandiko matakatifu.
Mwenyezi Mungu anasema,watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa.Kusoama biblia ni sehemu ya kujua mambo na kumjua uweza na utukufu wake Mwenyezi Mungu muumbaji.

Swali la leo,ningependa kujua bustani ya eden ilikuwa wapi katika ulimwengu wa leo.Kwa kifupi tu naweza kusema,wazungu wamepotosha sana khusu hili na kuhusu image halisi ya Mungu wetu pamoja alituumba kutokana na mfano wake;lakni Mungu anaonekana ni mtu mweupe tu.Kwahyo na mambo mengine nahisi yatakuwa yamepotoshwa khusu bibilia tofauti na wenzangu waislam ambao wao vitabu vyao vimebaki kama vilivyo na hadithi zao hazina utofauti na bibilia,tofauti yetu mimi sijui ni wapi.

Hivyo nafungua majadala tujuzane ni wapi bustani ilikuwepo na tutazidi kuulizana maswali pale utata unapokuwa.Nawakaribisha waislam maana wengi wao wanao ufahamu wa kwenye biblia na naomba huu mjadala uwe wa amani?

Ilikuwa Tanzania. we uoni nchi ilivyokuwa na maajabu ya kila namna??.Mpaka raia wake ni waajabu.
 
Navyoelewa mimi ni kua bible imesema Adam na eva walipotenda dhambi walifukuzwa ndani ya bustani na kuanza kuishi maisha ya tabu sasa hii edeni inaonekana haikua duniani Bali juu ya anga
Na hao wanaosema Iraq waache kukariri abrahamu alikua huko na alitakiwa kuondoka
 
Back
Top Bottom