Biashara ipo kwa sababu demand ni kubwa na bei za kule ziko juu pia, ila jamaa warushi sana na wabaguzi . Option nzuri ni kufanya ubia na mwenyeji kama utapata bahati ya kumpata, au umpate mngazija anayeishi huku bongo. Dar wako wengi tu.
Mimi nilishajaribu kufanya biashara huko. Miezi 6 ya kwanza nikaenda vizuri baadae nikarushwa euro 4,500 sikukata tamaa. Baadae nikaambiwa mzigo wangu (cost tzs 3.7) umetupwa baharini, bahari ilichafuka. Kufuatilia nikaambiwa ndio zao. Nikaacha hiyo biashara.
Aliyenipeleka huko naye akadhulumiwa vitunguu akaambiwa katika tani 3 aliyopeleka tani 2 ni maganda ya nje, uchafu, wakati yeye alivisafisha kabla ya kutuma.
kukaa kule pia ni gharama maisha yao yako juu sana. Kama utaamua kufuatilia kwa karibu ina maana utatumia muda mrefu kule, na faida yote utaimalizia hoteli na msosi.
Wanatumia sana euro kuliko pesa yao.