Business in Comoro

Business in Comoro

Mkuu! Anza biashara ya mbuzi mara kwani kuna jamaa kasema unaweza uza hata mbuzi 100 kwa siku. Changamkia DILI na nasikia ndafu ndiyo inalipa na ujuwe malipo ni USD TU.

UNASIKIA!
Ushaur wa bure.... EPUKE BIASHARA ZA KUTEGEMEA KUSIKIA UTALIA SANA
 
  • Thanks
Reactions: SDG
kuna biashara nyingi tu mfano, nyama unaweza peleka ngombe au nyama mbuzi n.k, pia nafaka ngozi n.k kama uko serious nicheck
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Biashara ipo kwa sababu demand ni kubwa na bei za kule ziko juu pia, ila jamaa warushi sana na wabaguzi . Option nzuri ni kufanya ubia na mwenyeji kama utapata bahati ya kumpata, au umpate mngazija anayeishi huku bongo. Dar wako wengi tu.
Mimi nilishajaribu kufanya biashara huko. Miezi 6 ya kwanza nikaenda vizuri baadae nikarushwa euro 4,500 sikukata tamaa. Baadae nikaambiwa mzigo wangu (cost tzs 3.7) umetupwa baharini, bahari ilichafuka. Kufuatilia nikaambiwa ndio zao. Nikaacha hiyo biashara.
Aliyenipeleka huko naye akadhulumiwa vitunguu akaambiwa katika tani 3 aliyopeleka tani 2 ni maganda ya nje, uchafu, wakati yeye alivisafisha kabla ya kutuma.
kukaa kule pia ni gharama maisha yao yako juu sana. Kama utaamua kufuatilia kwa karibu ina maana utatumia muda mrefu kule, na faida yote utaimalizia hoteli na msosi.
Wanatumia sana euro kuliko pesa yao.
Samahani huu ulikuwa ni mwaka gani na ilikuwje ukazulumiwa kiasi hiki Cha fedha
 
Kitu kimoja cha ajabu ni kwamba hawa jamaa hata wakikudhulumu sijui kwa nini huwa hata roho haiumi kabisa sijui wanakusomea dua kabla ya kukupiga changa au sijui wanafanyaje hawa jirani zetu
 
Kitu kimoja cha ajabu ni kwamba hawa jamaa hata wakikudhulumu sijui kwa nini huwa hata roho haiumi kabisa sijui wanakusomea dua kabla ya kukupiga changa au sijui wanafanyaje hawa jirani zetu
Ushawahi kufanya nao biashara mkuu?
 
nafikri biashara ya madawa ya binadamu inalipa comoro. kuna jirani zangu wamehamia huko kwa ajili ya hiyo biashara.
Hivi unaweza kunisaidia connection na wauzaji wa medical supplies and equipment kwa bei za jumla ndani ya dar es salaam?
 
Back
Top Bottom