Business in Comoro

Alifanya bz gani? nilikuwa na plan kujua habari za kuwauzia mbuzi miaka ijayo,kumbe jamaa ni zurumati!!!!!.Pole yake.

alipeleka nafaka, lakini ninaamini wapo wafanyabiashara wengi wanaopeleka bidhaa huko na kufanikiwa vizuri
 
nafikri biashara ya madawa ya binadamu inalipa comoro. kuna jirani zangu wamehamia huko kwa ajili ya hiyo biashara.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Comoro wana import almost kila kitu,pesa wanapata kwa ndugu zao walio Ufaransa na ulaya.ILA Biashara na WaComoro inabidi uwe very sensitive na cultural issues zao,inabidi uwasome kwa karibu sana.kitu kibaya walichonacho ni TRA yao,unaweza kufika na mzigo ukapewa kodi ya Ajabu ili ushindwe then mali inachukuliwa na mcomoro etc,
Kuna mama mcomoro amefanikiwa sana na biashara ya Nyama.
Kuna anaitwa George Kizenga,ana uzoefu mkubwa na hawa jamaa,pia ni Agent wa Sigara comoro alinipa dondoo za hawa jamaa.
Njia nzuri ni kufanya partnership na mcomoro.
 
Na mimi najua hivyo kuwa nyama ya mbuzi/ng`ombe kule ni bonge la bz, ngoja tufuatilie zaidi.
Nilisikia biashara ya mbuzi inalipa,niliambiwa unaweza kuuza mbuzi kuanzia dollar 100.
 
kwa nini comoro na siyo pemba, zanzibar au nchi zingine za jirani kama rwanda, zambia, msumbiji, kenya, uganda na burundi? tatizo ni ufinyu wa fikra huwezi kubeba biashara zako kwenda kuuza nchi ingine bila kufanya utafiti eti unategemea wema wa watu wa huko. Haya maendeleo ya dunia sijui kwa nini yametuacha mbali hivi watz, sisi ni bongo lala ile mbaya
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Biashara ipo kwa sababu demand ni kubwa na bei za kule ziko juu pia, ila jamaa warushi sana na wabaguzi . Option nzuri ni kufanya ubia na mwenyeji kama utapata bahati ya kumpata, au umpate mngazija anayeishi huku bongo. Dar wako wengi tu.
Mimi nilishajaribu kufanya biashara huko. Miezi 6 ya kwanza nikaenda vizuri baadae nikarushwa euro 4,500 sikukata tamaa. Baadae nikaambiwa mzigo wangu (cost tzs 3.7) umetupwa baharini, bahari ilichafuka. Kufuatilia nikaambiwa ndio zao. Nikaacha hiyo biashara.
Aliyenipeleka huko naye akadhulumiwa vitunguu akaambiwa katika tani 3 aliyopeleka tani 2 ni maganda ya nje, uchafu, wakati yeye alivisafisha kabla ya kutuma.
kukaa kule pia ni gharama maisha yao yako juu sana. Kama utaamua kufuatilia kwa karibu ina maana utatumia muda mrefu kule, na faida yote utaimalizia hoteli na msosi.
Wanatumia sana euro kuliko pesa yao.
 
eje mfanyaje za mnono kwezi Uwe makini ukokosea umeliwa ni watu wa mkopo so ukikopwa uwe na subra hata miaka kadhaa

Pima jiulize then chukua maamuzi
 
eje mfanyaje za mnono kwezi Uwe makini ukokosea umeliwa ni watu wa mkopo so ukikopwa uwe na subra hata miaka kadhaa

Pima jiulize then chukua maamuzi

Mpaka hapa ni kwamba hawa jamaa si wazuri, mimi hela zangu bado ni za mawazo,nikopwe 2011 halafu nilipwe 2015,
Basi ngoja nishuke kwa Wareno hapo naweza okota kidude.

Hivi njia ya Kwenda Sheli sheli si inapita kwa wajuba wa Somalia?
 
Uzoefu wangu kwa watanzania wanaofanya biashara nje ya Tz,wanafanya biashara kiujima.thus why wanadhurumiwa,wanakata mitaji na wanakutana na problems kila siku.nimeliona hilo kwa macho yangu South africa,kenya na ata biashara za mkoa kwa mkoa!. Popote pale ata Comoro biashara nzuri ni ile registered and follow all law and regulations.Watanzania tufanye biashara kisomi. Kata leseni ya biashara,kata Tin ,fanya utafiti na jua wateja wa hicho utakacho fanya,fungua akaunt Exim (wapo comoro) then fanya biashara uone kama utadhurumiwa.uwezi peleka vitunguu then ukasubir viuzwe na mkomoro ndo akupe hela yako.why ucfungue duka mwenyewe?.
 
Biashara ipo lakini ni matapeli sana wale jamaa...nilidhulumiwa ng'ombe mwaka mmoja uliopita baada ya kuingia mkenge kwamba nipeleke mzigo then nilipwe mzigo ukishafika..duh!!!mpaka leo ni stori tu nimefuatilia sana kulekule bila mafanikio na nikaingia gharama zaidi ...nikawa mpole....hawaeleweki kabisa wale jamaa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Biashara ipo lakini ni matapeli sana wale jamaa...nilidhulumiwa ng'ombe mwaka mmoja uliopita baada ya kuingia mkenge kwamba nipeleke mzigo then nilipwe mzigo ukishafika..duh!!!mpaka leo ni stori tu nimefuatilia sana kulekule bila mafanikio na nikaingia gharama zaidi ...nikawa mpole....hawaeleweki kabisa wale jamaa

Bado nasisitiza, hawa jamaa ni vimeo. Pole ndugu yangu kwa hayo yaliyokukuta. Maadamu Comoro ni kimeo vipi hapa jirani Usheli sheli?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom