Mkuu kama utaweza kanunue mazao katavi sehemu moja inaitwa bonde la mpimbwe katika vijiji vya kibaoni kwao na mh.pinda,usevya,tupindo,mbede,mwamapuli,chamalendi,ukingwa na vijiji vyote vya bonde hilo,nenda kanunue mahindi kwa gunia tsh 40 mpaka 50 hiyo ni bei ya kununulia,ukifika tafuta dalali wa kukununulia mzigo kutoka vijijini utamlipa kila gunia sh.1000,usafiri wa gunia kutoka kijijini hadi maeneo ambayo gari inaweza kupita haizidi sh 2000_3000,kipindi unakusanya mzigo wako unapanga chumba cha kuishi hapo hapo kijijini ikibidi unapanga na chumba cha kuhifadhia mazao yako ukiwa na dalali watatu ndani ya wiki mbili umekusanya mzigo wa kutosha na magari ni mengi sana yanayobeba mazao kutoka huko katavi kuleta mikoa mingine,gharama ya gunia moja kulisafirisha kulitoa mfano majimoto au mwamapuli kijijini kulileta shy,mwanza au bariadi ni tsh 10000 ikijumuisha nauli,kupakiza na kushusha gunia kwahyo ukiwa na gunia 100 utazisafirisha kwa gharama ya milioni 1,000,000 ukiyafikisha mazao mkoani unayaweka stoo kwanza kusibili bei iwe nzuri kuanzia miezi ya kumi na mbili,wa kwanza na wa pili ndipo unasukuma mzigo wako ukiwa makini faida utatengeneza si chini ya sh 40 elfu kwa gunia hapo tumetoa gharama zote za usafiri,dalali,mfuko,stoo ya muda,watu wa kuyasafisha na kuyawekea dawa mahindi ili yasipeche kwa urahisi mf una gunia 100 utatengeneza faida ya 4milioni ndani ya miezi kuanzia huu wa nane hadi wa pili mwakani ambpo mzigo wako utauza tena ukiwa umetulia kwako, if upo seriazi andaa ml.5 ya kuanzia biashara hiyo,pia kuna mazao kama karanga yanabei mbaya sana kule gunia debe sita sh.elfu 30 ni wewe kuchagua maindi au karanga.ukiwa tayari nitafute nikuunganishe pale pale kijijini kwa mawakala wanao nunua mazao na sehemu ya kuhifadhia natumia simu nimechoka kuandika ukihitaji nitakufafanulia vizuri zaidi,mkuu kazi kwako
Sent using
Jamii Forums mobile app