Bus gani zuri Dar - Babati?

Gari nzuri ni mbili 2.... Pole pole ile mpya....ukikuta ya zamani usipande......na God is One...Yaliyobaki ukipanda utaboreka ukiwa ndani ya gari
 
Umenikumbusha enzi zile niko dareda sec.tulikuwa tunayatimia mabasi ya mtei ama prince line kwani mmiliki wake yuko gongoh na ilikuwa rahisi kuyakodi[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Mtei ndo master wa hiyo route. Dar-BBT via Dodoma.
Sema gari zake sio Luxury ila ni za uhakika. Otherwise Polepole ana gari mpya ambayo ni luxury. Ila Karibu sana Babati. Niko Nyunguu hapa. Ukifika ukahitaji conpany ya wana JF wenzio pm me
Nyunguuu! Napapata sana hapo karibu na tank la maji na Msikiti.
 
Panda bus linaitwa pole pole au God is love ndio pamba hizo
 
checki na Katarina wa dar!!!(dareda)
 
Nahitaji kusafiri kesho, naomba msaada wa bus zuri from Dar to Babati.

Asanteni.
Unapitia njia ipi kama Arusha ni vidaladala vya kumwaga na kama kupitia Dodoma,Singida hadi Babati mabasi ni mengi tu ,ila sijawahi kuona basi la moja kwa moja la Dar hadi Babati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…