Burundi yapata Ikulu mpya

Burundi yapata Ikulu mpya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Balozi wa China nchini Burundi Bw. Li Changlin na waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw. Ezechiel Nibigira wamesaini hati ya makabidhiano ya jengo la Ikulu ya Burundi lililojengwa kwa msaada wa China.

Akiongea kwenye hafla ya kusaini hati ya makabidhiano kwenye Ikulu mpya kwenye eneo la Mutimbuzi, kaskazini mwa Bujumbura, balozi wa China Bw. Li Changlin amesema makabidhiano hayo ni alama ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Burundi, na kwamba ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaweka mkazo katika kuboresha maisha ya wananchi wa Burundi na mazingira ya kazi ya watumishi wa umma wa Burundi.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw. Nibigira ameishukuru China kwa kujenga Ikulu hiyo, ambayo Burundi haijawahi kuwa nayo tangu ijipatie uhuru mwaka 1962, na kusema kwamba hii ni mara ya kwanza katika historia kwa Burundi kupata miundombinu mizuri, na imethibitisha uhusiano imara wa kisiasa na kidiplomasia uliopo kati ya Burundi na China.
 
Ina maana mgerumani hakujenga hata jengo la hadhi kama ilivyo Magogoni?
Burundi wana mali asili gani ambazo wachina wanachota na wanazipitisha wapi? Mnasema mabeberu mnasahau beberu mkubwa ni huyu mliyemkaribisha kwa mikono minne na ataondoka na kila kitu. Subiri hata maini na figo zenu zitaanza kunyofolewa ndo mtamjua mchina.
 
Nchi ya Burundi ilikuwa chini ya Mbelgiji
Kumbuka kabla ya vita ya kwanza Burundi, Rwanda na Tanganyika plus Namibia na nchi nyingine ziligawiwa kwa ujerumani according to Berlin Conference agreement tuliitwa German ost Africa. Walipozichapa wenyewe na mjerumani kushindwa, wale walioshinda waligawana makoloni. Tanganyika ikapewa UK under protectorate, Wabergigi wakapewa Burundi na Rwanda wakapewa Wafaransa ingawa kwa Rwanda sina uhakika.
 
Burundi koloni la ujerumani au Portugal?


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Mjerumani alitawala Tanganyika jina alilotupa, Burundi na Rwanda na nchi nyingine kama Namibia ila hizi nchi tatu zilikuwa zimeungana. Watu walikuwa wakitoka Burundi na Rwanda kuja Tanganyika kama nchi moja na hata kabla ya wajerumani wakati wa watemi, kulikuwa na migration ya watu. Ureno walitawala Msumbiji na nchi nyingine za West Coast. Baada ya vita ya pili Namibia ilichukuliwa na wareno.
 
Kwani ile ya magogoni nani kaijenga si wakoloni wa kijerumani. Au Tanganyika imewahi kujenga ikulu yake wenyewe?


Ndukiiiii [emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️[emoji125]‍♂️

Acha wenge Mkuu. Kwa sasa tuna Ikulu tuliojenga kwa mikono yetu wenyewe.

Jaribu kutembele Chamwino...
 
Acha wenge Mkuu. Kwa sasa tuna Ikulu tuliojenga kwa mikono yetu wenyewe.

Jaribu kutembele Chamwino...
Chamwino ikulu ndogo au kubwa? Unajua maana ya ikulu?.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom