Burundi nao waitosa Tanzania!

Burundi nao waitosa Tanzania!

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Wakubaliana kuunda rasimu ya shirikisho la EAC
By James Gashumba, EANA
Arusha, Septemba 20 , 2013 (EANA)- Mkutano wa maafisa waandamizi kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wa kuharakisha Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki umekubaliana kuanza kuandaa rasimu ya katiba ya shirikisho hilo.

Kama ilivyokuwa kwa timu ya wataalamu walioandaa Itifaki ya Soko la Pamoja, timu ya kuaada rasimu ya katiba ya shirikisho la kisiasa itajumuisha wataalamu mbalimbali kutoka nchi zote tano wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

''Tumekubaliana juu ya taratibu na jinsi ya kuhakikisha kwamba ipo miongozo iliyowazi juu ya kuandaa rasimu hiyo ambayo hatimaye itafikia katika hatua ya mwisho ya kuundwa kwa shirikisho la kisiasa,'' Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni alisema baada ya mkutano wa mawaziri mjini Kampala mwishoni mwa wiki.

Wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda Juni mwaka huu walikubaliana kuongeza kasi ya kufikia lengo la shirikisho la Afrika mashariki.
Pia katika mkutano uliofanyika Mombasa,Kenya, Agosti mwaka huu, Burundi nayo iliunga mkono hatua hiyo ambayo pia inalenga kuimairisha miundombinu chakavu ndani ya kanda hiyo ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo wa Kampala juu ya shirikisho la kisiasa ni wa kwanza wa aina yake ambapo maafisa waandamizi kutoka Rwanda, Kenya,Burundi na Uganda wamehudhuria tangu kikao cha utatu kilichofanyika mjini Entebe, Uganda Juni, mwaka huu.

Mawaziri kutoka nchi mbalimbali wananchama wa EAC waliopewa dhamana ya maandalizi ya shirikisho la kisiasa watatoa ripoti ya hatua iliyofikiwa mbele ya mkutano wa wakuu wa nchi za EAC utakaofanyika Oktoba, mjini Kigali, Rwanda.

Tanzania haimo katika mchakato wa shirikisho
Nchi hizo nne za EAC zinatumia baadhi ya vipembele katika mtangamano wa Afrika Mashariki ambavyo vinaeleza kwamba baadhi ya wananchama ndani ya jumuiya wanaweza kwenda kasi zaidi kuliko wengine katika baadhi ya masuala yanayohusu mtangamano.

Mahakama ya Afrika ya Mashariki (EACJ) ilitoa uamuzi mwaka 2009 kwamba hatua ya aina hii inaendana sawia na mahitaji ya muafaka katika kufikia maamuzi ndani ya EAC.

JG/IM/NI
 
Hizi ndoa za mkeka zina matatizo yake, sijafahamu utafiti wa kina uliofanywa nao zaidi ya kufikiria msukumo tu wa kiitifaki kutokana na wimbi la Tanzania kujitangaza katika anga za mataifa mbalimbali duniani na kuonekana kukubalika na kuvutia viongozi mbalimbali kuitembelea.

Kuna nchi kama Uingereza, na pengine hata Uswizi hazikujihusisha kwa undani katika shirikisho la Ulaya, hata hivyo pamoja na kugomea kuingia katika sarafu ya Ulaya na kuruhusu tu mzunguko wa sarafu hiyo katika nchi, bado sijaona kuathirika na bado inaonekana kiuchumi kuendelea kutengamaa.

Kwa vile Tanzania ni mwanachama wa nchi za ushirikiano wa kiuchumi nchi za kusini mwa Afrika, sioni haja ya kuhangaika na ndo ya mkeka ya hawa Museveni, Kenyata Wanyarwanda. Tuwaache waendelee na yao, ipo siku watakapokuja kugutuka kuingia kichwakichwa ndipo wakapofahamu kwa nini Tanzania tumekuwa muhimu kwao na kwamba uzoefu katika masuala ya shirikisho baina ya nchi na nchi si kama kukaribisha jirani wakutanapo kwenye kilabu cha pombe kukaa meza moja, ni mambo mazito yanayohitaji uchambuzi, utafiti na kupima kwa kina vinginevyo ni kumnufaisha fulani ambaye ameshindwa kutupa kete kwa Mtanzania aliye makini na kuhitaji muda wa kupima na kutafakari kabla ya kuchukua hatua.

Tanzania kuna kila la kujivunia na nyota inaendelea kumulika kwani tukituliza kichwa kuna kila dalili ya kuwa taifa la viwanda tokana na utajiri wa chuma huko wilayani Ludewa, chuma ambacho pia ni moja ya nguzo kubwa katika uundwaji wa viwanda vikubwa. Vigumu kuchukua chuma kukisafirisha nje ni ghali bora kujenga viwanda nchini na hivyo kulinufaisha taifa kiuchumi. Tuwaache waendelee na ndoa ya mkeka, ipo siku watajua na kurudi wenyewe kuanzia njia za vichochoro kwa aibu kabla hawajapiga hodi mlangoni.
 
Mbona majirani wanatushitukia hivi kulikoni? inawezekana tuna matatizo!!
 
hatuna haja ya kufanya haraka waacheni wafanye yao na sisi tufanye yetu mda ukifika tutaungana nao mbele kwa mbele
 
Candid umesema ukweli
mimi sioni sababu ya kuhangaika na hili shirikisho
Mfano mwingine mzuri ni Norway haipo kwenye shirikisho la nchi za ulaya
wanatumia sarafu yao wenyewe na uchumi wao uko imara sana
shirikisho la nchi za kusini inatosha waache hao wanaoitaka ardhi yetu kwa vitisho watapetape tuu
 
Sio majirani tuu wanatuonea jealous hata mataifa ya nje
Utajiri ulioko Tz unatisha
Inahitaji tuamke tuu watz tutumie hizi fursa
hao majirani wanatapatapa tuu hawana lolote
Hatuhitani ndo za mkeka!!!!!!!


Mbona majirani wanatushitukia hivi kulikoni? inawezekana tuna matatizo!!
 
waundee tu afadhali East Africa zibaki nchi mbili ya kwao na ya kwetu
 
Ujirani maana yake nikuwa na mutual benefits.

Ukiwakwaza jirani zako either kwa

-kiburi cha ukubwa wako au
-dharau,
-ama majivuno au
-kuwanyanyasa (fukuza fukuza)

Yanayotokea ni matokeo ya hayo hapo juu, wala sio ajabu- Adabu kwa wote sio upande mmoja.
 
HATA NCHI ZOTE ZIJITENGE BADO TZ ITASIMAMA KWA MTAZAMO HUU:
Mataifa yote ya Afrika Mashariki yameiona Tanzania kama taifa lisilojua umuhimu wa kutumia na kusimamia rasilimali zake kwa maendeleo ya taifa na watu wake lakini hili si jambo la kubezwa kwa mlango mwingine wa kufikiri.

Tanzania ni taifa ambalo kwa udhaifu wake limejikuta likijijenga vizuri kwa kuongeza vyanzo vingi vya ndani vya uchumi tofauti na mataifa mengine katika ukanda huu achilia mbali usaidizi wa bajeti ambao kila nchi katika ukanda huu unapata toka nchi za ughaibuni tofauti na mataifa mengine kama Kenya na Uganda ambayo yanategemea sana uwekezaji walioufanya nje ya nchi zao na hasa Tanzania.

Angalia vizuri, Tanzania inauwezo kiasi gani wa kuajiri watu wake katika sekta binafsi na sekta za umma, ongezeko la pato la taifa, ongezeko la uwekezaji wa ndani kutoka kwa wazawa, mataifa yote ya Afrika mashariki yanaona kuwa Tanzania ndio mahali sahihi pa kufanya uwekezaji mkubwa.

Kama viongozi wetu wataona jambo hili na kujua namna ya kutumia mianya hii, hata waungane na kuunda umoja wao ndani ya umoja bado Tanzania itaendelea kuwa ndio mama kwao na taifa kubwa sio tu kwa ukubwa wa eneo la ardhi bali lenye uwezo wa kuamua taswira za mataifa mengine.

Uhuru Kenyata(UK), Paul Kagame(PK) na Museveni(M7) wote wanajua kuwa bila Tanzania hakuna Afrika mashariki na kujitoa kwa Tanzania katika jumuiya hii ni kiama kwa mataifa yote yaliyobakia.

Tatizo ni kujisahau kwa Waziri husika na nina mashaka sana na nini anamshauri JK juu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki au yuko bize na mbio za urais 2015.
 
Hakuna ugonjwa mbaya kama ukosefu wa fikra huru, Je wote mnaosupport hao walio tutenga na kuona kuwa mkuru/ watz wana mtatizo mmeshawahi kusoma kitabu cha "An Enemy of the People "? Basi kitafuteni kama mtakielewa na kukipeg kwenye scenario iliyopo hamtabwabwaja kama mnavyofanya.
 
Candid Scope,

Siyo kweli hayo unayoyasema. Muingereza kwa sasa anaporomoka si kawaida. Hata huduma zao za kulisha watu bure na kuwapa nyumba sasa wameanza kuzibana. Kiuchumi ameshazidiwa na Brazil na alipotaka kujitoa EU, China na USA walimwambia hata asiote kufanya hivyo.

Kuhusu Swis, hata wao wamejiingiza kimya kimya kwenye Schengen maana walikuwa wanakosa pesa kibao. Kujiondoa kwa Rwanda, Burundi na Uganda, kutakuwa na madhara makubwa sana kwetu na hapo mtu asikudanganye. Labda na sisi tuje tujifanye kawa Waswizi kwa kujiingiza kimya kimya kwenye Schengen na Uganda, Rwanda na Burundi huko mbeleni maana itakuwa na faida kwao na sisi.

Anyway, siasa za Africa zinabadilika badilika kutokana na Rais. Kesho wakija Marais wengine, watagombana na watarudisha ndoa na Tanzania. Inabidi katiba zetu kwanza zibadilike na nchi iwe na msimamo na siyo RAIS.
 
Last edited by a moderator:
Hatuna haraka sana, ngoja kwanza tumalize oparesheni Kimbunga halafu tupeane vitambulisho vya Uraia.

Baadae tuweke kura ya maoni ili wote tutoe maamuzi kwa pamoja kama tuingie huko au tuendelee kusubiri!
 
Kikwete apunguze umbea kwa mataifa makubwa! Kutumika tumika tu. Majirani wanatuchukia kwa sababu hiyo
 
Back
Top Bottom