Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Burundi ametekwa nyara katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura na watu wenye silaha wakiwa wamevaa sare za jeshi la polisi la nchi hiyo, kwa mujibu wa familia yake.
Leopold Habarugira mwenye umri wa miaka 54, kutoka chama cha Development (UPD) , ni miongoni mwa wanasiasa wachache wa vyama vya upinzani waliobakia katika taifa hilo tangu lilipoingia katika mgogoro mwaka 2015 .
Aidha, Mke wa mwanasiasa huyo Liberates Nzitonda, amesema kuwa yeye na mume wake walikuwa wakifanya mazoezi na ghafla wakaona gari linakuja upande wao, likiwa na watu watatu wenye silaha na wakiwa wamevalia sare za polisi, ambapo walimchukua mume wake na kumlazimisha kuingia kwenye gari lao.
Hata hivyo, msemaji wa jeshi la polisi nchini humo, Pierre Nkurikiye amekanusha kuhusika kwa jeshi hilo huku akisema kuwa jeshi hilo halina taarifa yeyote kuhusiana na mwanasiasa huyo.