Burundi: Mwanasiasa wa upinzani atekwa na watu wenye silaha wakiwa na wamevaa sare za polisi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,279
2,000
Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Burundi ametekwa nyara katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura na watu wenye silaha wakiwa wamevaa sare za jeshi la polisi la nchi hiyo, kwa mujibu wa familia yake.

Leopold Habarugira mwenye umri wa miaka 54, kutoka chama cha Development (UPD) , ni miongoni mwa wanasiasa wachache wa vyama vya upinzani waliobakia katika taifa hilo tangu lilipoingia katika mgogoro mwaka 2015 .

Aidha, Mke wa mwanasiasa huyo Liberates Nzitonda, amesema kuwa yeye na mume wake walikuwa wakifanya mazoezi na ghafla wakaona gari linakuja upande wao, likiwa na watu watatu wenye silaha na wakiwa wamevalia sare za polisi, ambapo walimchukua mume wake na kumlazimisha kuingia kwenye gari lao.

Hata hivyo, msemaji wa jeshi la polisi nchini humo, Pierre Nkurikiye amekanusha kuhusika kwa jeshi hilo huku akisema kuwa jeshi hilo halina taarifa yeyote kuhusiana na mwanasiasa huyo.
 

charty

JF-Expert Member
Oct 28, 2013
7,414
2,000
Siasa mbaya mno,hivi hawa waheshimiwa hawaoni kazi zingine za kufanya zaidi ya kung'ang'ania madaraka!
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,279
2,000
Sasa basi hawa waupinzani wakitaka wawe salama inabidi kukaa kimya tu
Mkuu.. Pamoja na yote, naona kuendelea kukaa kimya ni mbaya zaidi kwa vile hamsha hamsha ya upinzani inasaidia japo kidogo

Kwasababu tunafahamu mengi zaidi kutokana na hizi tawala
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom