Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,552
Burundi. Sasa ni rasmi kwamba Burundi imekuwa nchi ya kwanza mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kujiondoa ikiwa ni mwaka mmoja tangu ilipowasilisha maombi yake.
Oktoba 27, 2016, Burundi iliwasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki-moon ikieleza kuhusu kusudio la kuanza mchakato wa mwaka mmoja kujiondoa. Burundi ilichukua uamuzi huo baada ya mahakama hiyo kuanzisha juhudi za kuchunguzi juu ya uwezekano wa kuwepo uhalifu wa kivita zilipoibuka vurugu mwaka 2015 wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwania muhula wa tatu
Pia, Gambia chini ya mtawala wa zamani aliyeko uhamishoni sasa Yahya Jammeh alianzisha mchakato wa kujiondoa ICC akilalamikia upendeleo kwa kutofanya uchunguzi na hatimaye kushtaki uhalifu unaofanywa nan chi za magharibi badala yake mahakama hiyo imejikita Afrika tu.
Lakini rais mpya wa taifa hilo Adama Barrow alitengua noti ya kujitoa iliyowasilishwa na Jammeh.
Umoja wa Afrika (AU) ulihamasisha nchi zote za Afrika kujiondoa katika mkutano wa mwaka ukidai kwamba mahakama hiyo haitendi haki kwa kushughulikia uhalifu wa bara la Afrika tu. Uamuzi huo ambao haukuwa shuruti la kisheria kwa utekelezaji ulipingwa na Nigeria na Senegal.
Kenya na Uganda pia zilitishia kujiondoa ICC wakati Zambia ilianzisha mchakato wa kupata maoni nchi nzima ikiwa iamue kujiondoa au ibaki kuwa mwanachama. Asilimia 93.3 ya waliotoa ushauri wao wamesisitiza nchi ibaki kuwa mwanachama ICC.
Afrika Kusini ilianzisha mchakato rasmi wa kujitoa mwaka 2016, hivyo kuwa nchi ya pili kuomba kujiondoa kwenye Mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo.
Lakini Mahakam Kuu ya Afrika Kusini mwaka huu 2017 ilisema uamuzi wa serikali kujiondoa ICC ulikuwa kinyume cha katiba na batili.
Pamoja na Burundi kujitoa, bado ICC ina uwezo kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo. Lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote wa siku zijazo.