Ni upi ufanisi wa mahakama ya kimataifa?

code0

Member
Apr 16, 2021
6
6
ivi kwa yaliyotokea IRAQ,AFGHANISTAN,SYRIA NA LIBYA kwa taifa la marekani kuuwa maelfu ya watu nakinachoendelea GAZA kwa ISRAEL kuua maelfu ya watu, watoto wafanyakazi wa Umoja wa Kimataifa na Madaktari halafu dunia ipo kimya mpaka south afrika ikaja fungua kesi.lakini URUSI ilipovamia UKRAINE tulisikia kelele namakemeo yakila aina kutoka Magharibi.

Je, Mahakama zakimataifa yaani ICC nimpango maalum kwaajili yanchi furani? Na je kwa kukosa usawa huu inamaana nafaida kuwepo kwake
 
Zingatia yafuatayo:

1) Afrika Kusini haijaishtaki Israel ICC. Imeishtaki ICJ. ICC inahusika na watu waliotenda uovu, na ina uwezo wa kutoa adhabu kama vile kuwafunga jela. Lakini ICJ, ni mahakama ya Umoja wa Mataifa inayohusika na migogoro baina ya mataifa. Haiwezi kumtia mtu binafsi hatiani. Kikubwa inachofanya ni kueleza tu kama kuna geneocide au la! Lakini hakuna adhabu. Ndiyo maana baadhi ya nchi zikishtakiwa, huwa zinaamua hata kutoenda kujitetea.

2) Kwa suala la Ukraine, Russia ilitoka nchini mwake na kwenda kuivamia na kuikalia Ukraine. Wala Russia haikuvamiwa na Ukraine.

3) Kwa suala la Iraq, hakuna nchi ingeweza kuishtaki US au Taifa lolote kwa maana lilikuwa ni Azimio la umoja wa mataifa. Na mataifa 49 yalishiriki kwenye kuishambulia Iraq yakiongozwa na US, UK na Ufaransa.

4) Huko Syria, Misri na Libya, US isingiweza kushtakiwa kwa sababu yenyewe haikuanzisha vita bali ni makundi ya ndani kwenye mataifa hayo ambayo yalikuwa yanaonewa na watawala wao. Hivyo wao walienda kuwasaidia wasiangamizwe. Na hilo ni utekelezaji wa sheria ya kimataifa kuwa kama kuna genocide inatokea mahali popote pale, basi Taifa lolote linaruhusiwa kuingilia kati kwa nia ya kuwaokoa wale walio kwenye hatari ya kumalizwa na watawala wao.

5) Afganstan na Gaza ni matukio yanayofanana. Magaidi yameingia kwenye nchi nyingine, yamefanya mauaji makubwa kisha yametorokea nje ya nchi. Sheria za kimataifa zinayapa mataifa yaliyovamiwa haki ya kujilinda, kuwasaka wauaji popote pale ili kuondoa madhara na kuondoa kabisa tishio. Mathalani magaidi ya Hamas hata yangekimbilia Tanzania, Israel ingekuwa na haki ya kuyasaka na kuja kuyaua hata hapa kwetu ingawa katika kuyaangamiza, inaweza kutokea wakaangamizwa hata wasiohusika. Sheria za kimataifa, zinawataka waliovamiwa kuwa makini ili wasilete maafa kwa wasiohusika, lakini hata wasipokuwa makini, hakuna adhabu iliyotajwa.
 
Back
Top Bottom