Burn importation promote exportation

futikamba

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
243
13
Habari zenu wan JF.
Kwa kichwa cha habari hapo juu, napenda kuwasilisha. Tanzania ni nchi kubwa sana na yenye uwezo wa kutajirika vema ikiwa viongozi wetu watawajibika kama inavotakiwa na kuacha tamaa za pesa ndogo ndogo na kuwaza ufisadi daily.
Siku hizi, tanzania yetu imekuwa dampo la nchi nyingi tu duniani kutuletea bidhaa zao. Mfano mdogo tu, Blue Band. Hii bidhaa inaingizwa nchini kutoka eti hapo Kenya tu. Ina maana hapa TZ sisi tumeshindwa kweli kutengeneza siagi kwa ajili ya consumption yetu na export?
Huo ni mfano mdogo tu nimeutoa. Lakini ukiangalia kwa marefu na mapana, kuna vitu inabidi kusema ukweli vizuiwe kuingia nchini. Kama viongozi wa nchi yetu wangeliangalia hilo kwa kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuwapatia elimu na vifaa and especially wale wenye vipaji nna hakika Tanzania yetu ina mali nyingi sana za ku-export. Zilizopo sokoni kwa sasa hazitoshi. Akili na uwezo tunao. Nia yetu inadharauliwa na viongozi wetu. TUFANYEJE??
 
Wangeweza kuongea kodi kwa bidhaa zinazoingia na kupunguza kodi ya bidhaa za ndani huku wakiziboresha kiwango ingesaidia sana thamani ya shillingi ya KiTz kuongezeka kweli. Sisi hata toothpicks tunaimport jamani!
 
Punguzeni maneno maneno kwanza, bila imports nchi hii itakufa njaa. Kuna vitu vingi mno ambavyo nchi inahitaji kutoka nje hata hivyo vifaa na teknolojia unavyoongelea vya kuwapa wajasiria mali unafikiri vinatoka wapi? Ni lazima uwe na uwiano ili unayoyataka yawepo na pia ni vyema kukubali kuwa sisi ni zero na hatuna budi kuagiza kutoka nje vingi tu.
 
Bwana asikwambie mtu i kwakweli watanzania akili hatuna,angalia nchi kama china,hakuna uhuru hata kidogo ila ngalia jinsi watu wanvyojitoa kwenyi umasikini,sio serikali inawatoa kwenye umasikini,
ila ntakuunga mkono kwenye kutoa elimu ya ujasiriamali,kama serikali ikifanya hivi nadahani umasikini utaisha.kwa upande mwingine tusilaumau sana serikali sisi wananchi pia tunamakosa.hatujishughulishi ipasavyo.
 
Back
Top Bottom