Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Ujamaa...
Waislam wanajua kuwa serikali inajua.

Waislam tegemeo letu ni kuwaelimisha wananchi wote wajue tatizo linaloikabili nchi yetu.

Serikali ndiyo ya kuwapa Waislam majibu si yule ambae ananufaika na dhulma iliyopo.

Mradi wewe ushatufahamu sisi tumetosheka.
''Hawashauli,'' ''Kufikili,'' ''Ikwilili,'' ''busala...''
Dini itakusaidia nini katika maisha ikiwa unabagua watu
 
Hiyo Sheria ya kutokufungua mabucha ni Kwa Dar tu au Tanzania nzima? nauliza hivi kwasababu huku Arusha tuna kula kitimoto kuliko nyama yoyote na Kila mtaa ukienda utakuta mabucha Sasa inakuwaje Sheria iwe Kwa Dar peke yake
 
Wavaakobazi sio wakuwachekea ukiwachekea utavuna mabua..wengi ni brainwashed sana na uwezo mdogo wa kufikiri kama huyu mzee mleta uzi.

Sasa mnaenda kuvunja mabucha ya nguruwe yanawahusu nini kama huli kitu kaa tulia..wanapenda sana chokochoko hawa viumbe.

Ni imani isiyopenda amani bali fujo na chuki ndio msingi wa hii imani.

#MaendeleoHayanaChama
Walienda kuiba nyama tu
 
Hiyo Sheria ya kutokufungua mabucha ni Kwa Dar tu au Tanzania nzima? nauliza hivi kwasababu huku Arusha tuna kula kitimoto kuliko nyama yoyote na Kila mtaa ukienda utakuta mabucha Sasa inakuwaje Sheria iwe Kwa Dar peke yake
Mpuuze huyo mzee..illusion za udini zinamchanganya akili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Huyu Mzee ni mdini sana na mwenye chuki na ukiristu
#25
--------------------------------------------------------------------
Edward A Chapa said:

Wewe ni mdini Una udini. Hapo ndio natofautiana na wewe! Na mtu kama wewe ndio kila sehemu mnaweka udini na Kupanda mbegu mbaya ya Udini katika nchi yetu. Kila kitu wewe unaleta Udini tuu. Ninyi mnarudisha nyuma maendeleo kwa ajili ya Udini.
---------------------------------------------------------------------

Bwana Edward huijui historia ya uhuru na sababu walioshika serikali wanaiogopa.

Laiti wazee wetu wangekuwa wabaguzi wa dini Nyerere asingekuwa kiongozi wa TAA, TANU na Tanganyika.

Je, unawajua waliompokea Nyerere Dar es Salaam ya miaka ya 1950 na kuishi na yeye kama ndugu yao?

Unajua nyumba aliyoishi Nyerere Dar es Salaam baada ya kuacha kazi ya ualimu Pugu?

Unaijua historia ya Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy na Nyerere na Mama Maria?
Je na ya Ali Msham na Nyerere na Mama Maria?…

JIBU

Bwana Edward huijui historia ya uhuru na sababu walioshika serikali wanaiogopa.

Laiti wazee wetu wangekuwa wabaguzi wa dini Nyerere asingekuwa kiongozi wa TAA, TANU na Tanganyika.

Je, unawajua waliompokea Nyerere Dar es Salaam ya miaka ya 1950 na kuishi na yeye kama ndugu yao?

Unajua nyumba aliyoishi Nyerere Dar es Salaam baada ya kuacha kazi ya ualimu Pugu?

Unaijua historia ya Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy na Nyerere na Mama Maria?
Je na ya Ali Msham na Nyerere na Mama Maria?

Je ya Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Nyerere?
Je historia ya Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi na Max Mbwana na Nyerere?

Bi. Shariffa bint Mzee na Suleiman Masoud Mnonji na Sheikh Yusuf Badi Lindi, Mtwara na Mikindani Waislam wengi wasio na hesabu Tanganyika nzima.

Wapi umesikia wametajwa?
Hawa walimbagua Nyerere kwa kuwa alikuwa Mkatoliki?

Hivi kuandika historia za mashujaa hawa waliofutwa katika historia ya uhuru wetu ndiyo imekuwa ubaguzi wa dini?

Au hujui kama historia hii ilifutwa?
Unawajua waliotishwa na historia hii na bado inawatia hofu hadi leo?

Nini sababu ya uoga huu?

Je uliridhika kuona kuwa historia hii haikuwa inafahamika na leo unachukia kuona mimi nimeiandika na watu wameanza kujua ukweli.

Unajua kuwa wenye madaraka ya kuongoza nchi si Waislam na mgao ni 20:80?

Rais Mkapa alielezwa hali tuliyonayo na akaomba ushahidi na ushahidi akapewa na Prof. Hamza Njozi kupitia kitabu cha mauaji ya Mwembechai.

Kitabu kilipigwa marufuku.
Huu ndiyo udini wenyewe.

Hili ni tatizo na linafahamika.
Wewe ungeridhika kuona Waislam wamehodhi serikali kwa 80%.

Sidhani.
Hii ndiyo mbegu mbaya uliyoitaja ati inapandwa na Waislamu.

Ukipenda naweza nikakusomesha somo hili.

Udini ulianza tu baada ya uhuru mwaka 1961 kwa kuwekwa mikakati ya kufuta historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hii ni mada ya inayojitegemea yenyewe.

Soma historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika si hii iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981.

Soma kitabu cha Abdul Sykes na mwandishi ni mie.
Kitabu kinakwenda toleo la tano toka kuchapwa mwaka wa 1998.

Kitabu kimependwa kwa kuwa kina historia ya kweli inayowavutia wasomaji wengi wao ni vijana wa kizazi ambacho hakikuwepo wakati wa kudai uhuru.

Ukweli wote umo humo ndani.

Kitabu hiki ndiyo sababu ya kuandikwa Biography of Julius Nyerere ikidhaniwa kuwa kinaweza kujibu masuala ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.

Yapo mengi.
Ikiwa hujui kitu uliza wenye kujua ufahamishwe.

Mimi siandiki kufanya maskhara.
Naandika kuitafutia amani ya kweli nchi yangu.

Naandika ili viongozi wetu wachukue hatua kurekebisha hali hii.
Angalia picha hizo hapo chini.

Ulipatapo kuziona popote.
Ziko nyingi sana na zinajieleza wenyewe.

Je unaona ni sawa kuwa historia hii isifahamike?
Bado unaamini kuwa Waislam ni wabaguzi hata baada ya ushahidi huu?

1660795158960.jpeg
1660795214988.png
1660795276324.jpeg
 
Hui...
Nimewasilisha mada nzima Kenyatta University kuhusu sakata la kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe.

Mimi ukiniulliza kwa nini hili lilitokea nitakwambia kuwa serikali ililishughulikia vibaya tatizo hili.

Watendaji walikosa busara.
Nimesoma mada yako Mzee wangu...Mashallah ni nzuri Sana....na nimefurahishwa na harakati za Sheikh Kassimu na nimehuzunishwa na mapito aliyopitia pia...lakini alipambana kadri ya uwezo wake..Allah amstiri moja wake.
 
Einstein,
Namna yangu ya uandishi ni tofauti sana.

Huenda kwenye mambo yanayoeleza hali za nyakati.

Ningeandika vinginevyo taazia hii isingechemsha watu kama unavyoona.

Nimeeleza tukio la mabucha na msimamo wa serikali na vipi Waislam walivyosimama kuikabili serikali.

Nimewaleta BBC, wahariri wa magazeti na jinsi viongozi wa nchi kuanzia Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na Katibu wa CCM walivyolishughulia tatizo la mabucha.

Yako mengi.

Lakini nia yangu ni kukutaka wewe msomaji uhiangaishe akili yako na hivyo kuwapima hawa viongozi.

Viongozi walitupa lawama kwengine na kusema kuwa waliovunja mabucha nia yao ilikuwa kupindua serikali.

Je, huoni kuwa hapo yapo mengi ya kujifunza?
Binafsi nimeona viongozi wameshindwa kusimamia mamlaka Yao....ilikuwa ni ishu rahisi Sana na kutafuta ufumbuzi wake na ndio maana baada ya kuona wameboronga wakajificha ktk kivuli cha kuleta habar mpya kuwa hao wahuni walitaka kuiangusha serikali...upumbavu mtupu
 
Ni hivi hakuna kitu muhimu kwa mwanadamu na Serikali kama kujua falsafa uliyoiamini na kuifata.

Kuna falsafa ya Mungu na Falsafa za Wanadamu.

Kazi moja kubwa ya falsafa za Wanadamu ni kugawa jamii ktk makundi makuu mawili.

1. Binadamu aliyekamilika.
2. Binadamu nusu.

Binadamu aliyekamilika wanafalsafa wanasema ndiye anaepaswa kuwa kiongozi.

Na binadamu nusu ni yule mtawaliwa.

Kwa uoni wangu hali ya waislam tokea Uhuru na sasa matokeo ya kukumbatia falsafa ya ujamaa na itikadi ya Usekyula bila kujua madhara yatayayowakuta.

Ninyi ni watawaliwa na ndio kwa maana mko mnakimbilia siti za nyuma ktk bus.

Ujamaa ni imani kama zilivyo imani nyengine. Ujamaa ni imani isiyoamini uwepo wa Mungu. Na Usekyula ni kujitenga serikali na dini.

Tunahitaji kuwa na Falsafa mpya ya nchi.

Falsafa na itikadi itakayounganisha imani ya uwepo wa Mungu na kuheshimu haki za kila mtu wakiwemo wenye imani za dini.

Na kwamba hakuna anayefaidika au kupungukiwa kwa sababu ya imani yake.

Ujamaa ni Kielezo tosha kuwa ni Vikwazo kwa waislam. Na Serikali ya Ujamaa ni kandamizi na ingawa kuna sheria ndogo za serikali za mitaa inayokataza bucha za nguruwe kuwa karibu na makazi ya watu kama ilivyo kwa baa na kumbi za starehe lkn Serikali za kijamaa hufanya Upendeleo kwa vikundi vya kidini mojawapo?!

2. Na hutunga Sheria na sera zinazozuia uhuru wa kidini kwa wengine!???!

3. Serikali za kijamaa zinawawekea mipaka ya kuafuamini kwa kidini?!?!

4. Na kunyanyasa kwa vikundi vya kidini.

Kuandika historia hii ni hatua moja. Lkn inapotokea wanachama wa CHADEMA wanaungana na vyama vya Kijamaa (CCM na ACT) ktk sakata hili in wazi waislam watahitaji chama kingine kitakachotunza utamaduni, mila na desturi za kila jamii. Ili pale mtz anapoamua kwenda kuishi ktk jamii yenye utamaduni, na mila tofauti na za kwake. Aziheshimu.

Hili ndilo tatizo lililopo kwa tz kwa sasa.

Pale jamii za wachungaji wanapokuja kwa Waswahili na kuwatawala na kutaka kuwalazimisha tamaduni za watu wa mufindi na arusha na mbeya kulala na nguruwe ktk zizi moja wanadhani watu wenye ustaarabu na huo watavumilia.

Na suluhisho ya mambo haya ni tuje na chama kipya kitakachokuja na falsafa mpya. Falsafa ya serikali ya shirikisho.

Kila kanda iwe na serikali iliyo na mamlaka zaidi ya kujiamulia mambo yao wenyewe.

Ukienda arusha hutoshangaa kuona mabucha kila baada ya nyumba 10. Huo in utamaduni wao. Tusiwalazimishe kubadili. Kama vile mufindi nguruwe zinazurura kama mbuzi. Huo ni utamaduni wao.

Lakini wanapokuja ktk mini yenye ustaarabu tofauti wasitake kulazimisha.
Wanapaswa kukubaliana na utamaduni wao.
Kongole kwako mkuu
 
Ni maeneo gani maalum kwa ajili ya kuishi Waislamu? Sheikh Rashid alizungumzia huu mkasa wa Kuvunja mabucha ya Nguruwe. Nlikuja kuona ulikuwa ni Umaamuma, ushetani na kutokuelimika. Mtoto alitumwa makusudi akanunue nyama ya nguruwe ili akija ionekane muislamu kisha kauziwa nyama ya nguruwe. But ukitumia tu common sense.
1. Nyama ya Nguruwe bei yake ipo juu.
2. Bucha za Nyama ya Nguruwe haziuzi ya ng'ombe wala mbuzi.

Sasa muuzaji kama alimuuzia mnunuaji nyama ya nguruwe je alijuaje kuwa ni muislamu na hatumii kitimoto?

Je huyo mnunuaji kama alienda moja kwa moja bucha ya nyama ya nguruwe akasema tu nataka nyama kilo 1 muuzaji alikuwa na kosa gani?

Lakini bila chembe ya unafiq hata chembe ni waislamu wangapi wanakula kwa siri kitimoto? Ule mkakati naufahamu sana na baadhi ya wahusika walikuja kukiri baadaye kuwa lengo lilikuwa ni kuzusha chokochoko. Wakirejea na Mkutano uliofanyika Abuja Nigeria miaka hiyo. Na maazimio yake. Na ufadhili ambao ulikuja tolewa na Muamar Ghadaf...

Haya mambo tupo ambao tunayafahamu na hatuuingi mkono sababu ni upuuzi mkubwa sana. Mwinyi alitoa tamko kubwa kipindi kile. Hilo hujaliweka 😁😁😁😁 sababu ni mwenzetu. Umeangalia matamko ya wakristo peke yake.😁

Siku zinavyozidi kwenda hata sisi tunakuona umepoteza mwelekeo.tunashindwa kukutetea maana unataka nasi tuanze kuonekana mafala...no way.
 
Komeo...
Kuna mambo huandikwa hapa huwa nayakalia kimya sisemi neno kwa kuwa itakuwa ni kubishana ma ghadhabu kupanda mfano wa maneno, ''no way,'' ''mafala'' na mfano wa hayo.

Lakini yapo maneno hupenda kuyatolea kauli.
Mimi hafarajika kuleta elimu ambayo si wengi wanayo.

Mkutano wa Abuja unazungumzia ''The Two Headed Dragon'' mpango wa kueneza Uislam Afrika.

Hayo yote ni ''fake.''
Ikiwa mtu atapenda kuamini vitu kama hivyo huna la kumfanya.

Allah kakataza ndani ya Qur'an kulaziisha dini.
Hakuna Muislam anaeweza kuweka mikakati ya kuhujumu imani nyingine.

Allah kakataza kwa kuwa anajua hatari yake.

Halikadhalika kawakataza Waislam wasidhulumu na wao wasikubali kudhulumiwa.

Haya ndiyo mafunzo ya Uislam.
Kama huniamini mimi waulize masheikh watakueleza ukweli.
 
Mzee ulikimbia aisee, haiwezekani uhudhurie shura pamoja na Hassan Halafu Hassani akamatwe we muda mchache usionekane eti umeitwa Nairobi, kumbuka kwenye stori ya kuna shehe mkuu alikamatiwaa njiani akitorokea Nairobi wakamrudisha Dar (ulidai alikuwa anaenda kwenye matibabu)
Nimecheka sana usiku huu.. wewe una utani na Mzee wetu Mzee Mohamed Said
 
Nimecheka sana usiku huu.. wewe una utani na Mzee wetu Mzee Mohamed Said
Einstein,
Hakuna aliyekimbia.

Kwangu mimi haya si mambo ya kufanya kejeli na maskhara.

Nimekujibu ili ufahamu kuwa nategemea adabu kutoka kwako.

Lakini ikiwa kama unadhani mimi ni mtu wa kuchezewa tafadhali fikiri mara mbili.

Vinginevyo nitasitisha mjadala na wewe.
Siko hapa kukejeliwa.

Mimi ni mtu na heshima yangu.

Lakini kukusaidia ungeweza kuniuliza ilikuwaje sikukamatwa na wengine wakakamatwa.

Hapa kuna stori nzuri ningependa kuieleza kama ungeuliza kwa adabu na heshima

Tafadhali tambua mimi si muhuni.
 
Einstein,
Hakuna aliyekimbia.

Kwangu mimi haya si mambo ya kufanya kejeli na maskhara.

Nimekujibu ili ufahamu kuwa nategemea adabu kutoka kwako.

Lakini ikiwa kama unadhani mimi ni mtu wa kuchezewa tafadhali fikiri mara mbili.

Vinginevyo nitasitisha mjadala na wewe.
Siko hapa kukejeliwe.

Mimi ni mtu na heshima yangu.

Lakini kukusaidia ungeweza kuniuliza ilikuwaje sikukamatwa na wengine wakakamatwa.

Hapa kuna stori nzuri ningependa kuieleza.
Tafadhali tambua mimi si muhuni.
Mzee Mohamed Said

Sijaelewa ni kwa nini umekwazika kiasi hicho, mimi nimemnukuu EINSTEIN112 ambae kwenye post yake anasema kuwa ulikimbia, mimi nimecheka kwa sababu nimechukulia kwamba ameamua kukutania,

members wengine humu ni kama wajukuu zako tu, ni watoto wadogo, ndio maana nikamwambia kwamba ana utani na wewe.

Pamoja na kuheshimu mchango wako wa kitaaluma, mimi ninakuheshimu wewe binafsi, tunapotofautiana kimtazamo tunajadili kwa hoja, wala siwezi kukukejeli hata siku moja.

Naomba niwie radhi kama post yangu namba 264 hapo juu imeonyesha kukukosea adabu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom