Burhani Charitable Health Centre Hali ni MBAYA!

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
nipo Burhani Charitable Health Centre, Wagonjwa ni wengi lakini kuna jamaa wanaendelea na Ujenzi (marekebisho ndani ya hospitali).

Wanatindua zege, wanapiga kelele vibaya mno, nimewaambia wahudumu hapa waongee nao ili waendelee baada ya masaa ya kazi wamegoma, kwa maelezo kwamba nikaongee nao mwenyewe, nimeenda kuongea na mafundi wamegoma kwa maelezo kwamba wao wanakwenda na muda, hivi napoandika msg hii kuna kelele sana humu ndani, kuna vumbi kali sana na wagonjwa ni wengi kwenye foleni wakisubiri kuingia LABORATORY.
 
eti ili kupunguza vumbi lisizagae sana, sasa wameamua KUZIMA FENI, anayemfahamu kiongozi yeyote wa hapa burhani naomba mtusaidie kumshtua au tuwekee namba hapa tuombe msaada, hali ni mbaya
 
Back
Top Bottom