baada ya hapo nini kiliendelea?Siku moja Bunuasi alitangaza kuwa Mungu anamtembelea nyumbani kwake kila Jumamosi, habari zilisambaa hadi zikafika kwa mfalme. Bunuasi akaitwa na mfalme ma kuambiwa aache kuwadanganya watu. Bunuasi akamuambia mfalme hata wewe kama utataka kumuona njoo.
Mfalme akamuekea masharti Bunuasi kuwa endapo Mungu hatoonekana atamuadhibu. Bunuasi akakubali. Hivyo habari zikaendelea hadi katika uongozi wote wa mfalme. Na kiongozi mkubwa aliyehitaji kuhudhuria katika tukio hilo ni waziri mkuu.
Jumamosi ikafika, watu wengi walikusanyika nje ya nyumba ya Bunuasi wakisubiria kumuona Mungu.
Bunuasi hakuonesha wasiwasi wowote ule. Aliingia ndani na kuweka kiti cha kifahari juu ya zulia zuri. Penbeni yake akaweka fimbo na chini mbele ya kiti akaweka viatu. Pia aliweka joho na kilemba. Vyote hivyo aliviweka kwa staili ya kama mtu kakaa katika kiti.
Baada ya hapo, akatoka nje huku akitabasamu na kusema kuwa Mungu tayari ameshawasili. Pia akasema kwa heshima, ni vyema wakaanza viongozi kwenda kumuona. Na akaongezea kusema kuwa kila mtu atamuona isipokuwa mtoto wa haramu (mtoto wa nje ya ndoa). Hivyo hakuja haja kwa watu hao kupanga foleni kutaka kumuona Mungu, hawatamuona.
Mchakato ukaanza, waziri mkuu akawa wa mwanzo kuingia...
Je atatoka na jibu gani? Na ni ipi hatma ya Bunuasi mbele ya mfalme?
Ila mi nina kumbu kumbu tofauti,kitabu nilikisoma mdogo sana primary school,nakumbuka hakuwa mungu alikuwa malaika.Kilichotokea ni kwamba watu wote kuanzia mfalme mwenyewe kila walipotoka nje ya kile chumba,walidai kuonana na malaika na kuongea naye vizuri sana.Wote walikuwa wanafiki,hamna hata mmoja aliyemwona malaika!baada ya hapo nini kiliendelea?
Hayo yalikuwa ya Bunuasi yasiyotofautiana na ya babu wa Liliondo.
hadithi hii naifahamu japo inatofauti kidogo ila tangu mwanzo wa hadithi hii nilihisi hitimisho lako litakuwa hili.
jaguarpaw,
mi pia naijua hi story,lakini muhusika ni ABDUL na si BUNUAS!kawaida kwenye kila tukio bunuasi hushinda mwisho lakini abdul hushindwa kukamilisha;
hi ilikuja baada ya abdul mpango wake wa kuuza ashes huku akiwaaminisha kuwa ni sugar kushtukiwa,akarudi mjini pembeni ya mji akajeng nyumba ambayo alisema malaika alimwagiza ajenge na atakaa hapo kwa siku kadhaa mtu mwema atamwona na kuongea nae mtu mbaya hatamwona!ndipo watu wakaja wakawa wakiona kiti na viatu lakini wakitoka wanasema wamemwona,habari zikamfikia mfalme naye akaenda akasema amemwona malaika!
Baada ya siku abdul akaenda kwenye jumba la mfalme,kama vile ameshika kitu kwa uangalifu alikuwepo mfalme na mawaziri wake,akamwambia mtukufu mfalme leo wakati malaika anaondoka amenipa hili koti lake nikupe nawe utanipa mabegi mawili ya dhahabu!akavesha mfalme afu akawauliza mawaziri kama kapendeza wakajibu kapendeza,mfalme akalivua akawa kalibeba kwa uangalifu kulipeleka chumban
mkewe akamshangaa ndo nini ivyo mfalme naye akamshangaa ina maana hulioni koti?akamwambia hamna koti apo tuweke jiwe likibaki juu koti lipo likianguka koti halipo wakaweka jiwe likaanguka puu!
Mfalme akarudi ukumbin kama vile kabeba vitu viwili vizito,akamwambia abdul wakati malaika anaondoka alipitia kuniaga na akanipa mabegi haya mawili ya dhahabu ukiniletea koti!
dah!kweli mkuu hiki kitabu umekisoma vizuri sana,nadhani nili confuse jina la abdul na abunuasi!jaguarpaw,