Buni wazo la biashara mtaji juu yangu

Buni wazo la biashara mtaji juu yangu

Maberere

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
316
Reaction score
93
Nashukuru nimempata mdada kupitia jukwaa hili wa kuniuzia kiduka changu cha nguo na mambo yanaenda vizuri. Karibuni kijitonyama mumuchangie,

leo nina wazo hili.
Kulingana na kuwa na majukumu binafisi,

Nitatoa million mbili kwa kijana yeyote wa kitamzania ambaye atakuwa tayari kubuni biashara au kutafuta fursa au office ya aina yeyote harali.

Hiyo biashara itakuwa yangu yeye atakuwa kama nimemwajiri japo atakuwa amebuni na kuanzisha biashara hiyo.

Leseni nitamchukulia mimi TRA,

Location au eneo au frem ya biashara atatafuta mwenyewe ila nitaiilipia mimi na mumiliki wa nyumba au Frem hizo atanitambua mimi kama mkodishiwa,

Biashara isiwe mobile (easy to be moved).

Bizaa tutaenda kununua wote hadi hapo tutakapoaminiana,

Mauzo ya kila siku yatawasilishwa kwa namna tukavyopatana,

Eneo la biashara ni sehem yeyote mkoa wa Dsm au mkoa wa Pwani.

Awe na umri unaotakiwa kisheria kuajiriwa,

Awe tayari kunipeleka kwa kwa ndugu au mtu anaetambulika.

Atatakiwa kwenda naye mahakamani kwa ajili ya kuapa akiwa na vizibitisho (dhamana) inaweza ikawa barua, vyeti na picha n.k... Hii itasaidia siku akikimbia nikimkamata niweze kumuadhibu kisheria na kihaki.

Jinsia yeyote na Elimu yeyote,

Asiwe mkubwa saana hadi nikawa namuogopa kusaidiana katika kukuza biashara yetu. (umri wa kati tu).


Sihitaji business plan nahitaji wazo lako tu, mfano sema nitafungua Grocery sehem flan au nitafungua stationary sehem flan nk. Na mimi nitapima wazo lako nikilikubali ndo tutaanzia hapo.

awe mwaminifu.
 
Hela inaweza kuongezeka ila isizidi 4,000,000.
 
Hapo unaajiri? Malipo haujayasema, hadi mahakamani loooh,
una masharti halafu unaonekana kuangalia upande mmoja yaani wako tu.

au unataka ndoa?
hapana nina mke mkuu, malipo tutaelewana tu.
 
Hela inaweza kuongezeka ila isizidi 4,000,000.


Napendekeza Biashara hizi tofauti…
1.Tufungue Duka la nguo nguo za watoto… wa kike na kiume! Spesheli, zinauzika hizo.
2. Tufungue Duka la Nafaka… mchele,na maharage ni vitu vinavyo pata wateja saana! Kulingana na eneo la biashara.
3. Stationary… yenye mashine ya Photocopy,laminator,binding, na kuuza Kadi mbali mbali pamoja na Gift papers.

Hizo hapo ^^^^ mojawapo ni Biashara ambayo inafaa kwa hela ambayo haitakiwi kuzidi milioni 4.
Na mimi naiweza kuifanya vizuri saana!!
Hayo masharti sio issue saana as long mimi ni Mwaminifu wasi wasi wa nini?
Ni hayo Ndugu…
zaidi tukutane PM
 
Kikubwa tukutane pm haina haja ya kuorozesha aina au wazo la biashara hapa! Hapa wachawi wengi.
 
Mm nataka partnership!

Ww huwezi kuniajiri, eti nikuuzie business idea then uniajiri!?

Kajipange!
 
Nakusaidia tu, sitaki malipo. Fungua ofisi ya Recruitment ;-
Wafanyakazi wa majumbani kila kichwa $2000
Wafanyakazi Mahoteli kila kichwa $2500
Wafanyakazi carwash kila kichwa $1800
Soko kuu lipo M/E , China, Far-East,nk. kama upo tayari PM imed.
 
Nimeipenda hiyo, l can give the same offer. Halafu faida tunagawana 60% ya faida yangu. Kama uko interested niPM.

I mean, nami napokea wazo la biashara, kama mwenye uzi mtaji wangu.
 
mkuu,kuna mashamba kibao yako wazi nje ya mji dar,unanunua kwa bei nafuu,au unakodisha kwa less cost,
Kibaha,mkulanga & Rufiji etc,u
Unaweza nunua boda boda 2,sitasimamia wafanyakazi wa hayo mashambani ,wala we huhitaji kuwepo kila siku,hao vijana wa boda boda watahusika kupeleka chakula mashambani kwa ajili ya kuwalisha wafanyakazi wakati wa kulima na inakuwa ni one time cost ya kulima,kupalilia na kuvuna,same time nje ya mji hakuna vizuzi vya boda boda wala ajali za lazima..
baadaya miezi 3 utakuwa umerudisha mtaji wako wote na faida juu...then unaweza endelea au ukafungua hardware,

unalima na kila baada ya siku 90unatanu duka la hardware...

kilimo cha ufuta,mananasi,pensions etc yanastawi mazingira yoyote tena kwa less uanglizi..

karibu,

dbuberwa@imbank.co.tz
 
Nakusaidia tu, sitaki malipo. Fungua ofisi ya Recruitment ;-
Wafanyakazi wa majumbani kila kichwa $2000
Wafanyakazi Mahoteli kila kichwa $2500
Wafanyakazi carwash kila kichwa $1800
Soko kuu lipo M/E , China, Far-East,nk. kama upo tayari PM imed.

Yaani ule dola 2000 halafu mtoto wa watu aende kuwa Punda huko majuu,
mweee!!!
Wewe unaweza kukubali afanyiwe mwanao hivo?
 
NOTED:-

Sina nia ya Human Trafficking.

kazi , uwezo na Makubaliano kwa radha period.
 
mahakamani??? ....kisa nini hasa!! ndo uaminifu unapatikana huko?? ...mtu aniambie chochote lakini sio habari za mahakamani aisee....kama kazi za siku hizi ndivyo zilivyo peaneni wenyewe tu.
 
Back
Top Bottom