Bungeni: Zitto aigalagaza Serikali, Spika ashindilia msumari wa moto!

Na RTC ziko wapi ndugu zangu?? Nakumbuka tulikuwa tunaenda viwanda vya serikali (Mashirika ya Umma au SU) kwenye ziara za kishule, tulienda Magunia Moshi, General Tyre Arusha, Kilimanjaro Machine Tools, TPC, Mtibwa Sugar Estates (nilifanyia field yangu hapa) nk, viko wapi??
 
mkuu cheap popularity kwa vitu vya msingi kama hivi kweli.acha unazi kaka. uwe objective n will be a greater thinker

usimuhukumu kwa sababu yawezekana kabisa hayo anayoyasema Zitto huyu jamaa hayaoni,hebu jiulize kwa mfano Serikali iliua kilichokuwa kiwanda cha zana za kilimo pale Mbeya (ZZK) leo imeleta mwekezaji na imempa kibali amejenga kiwanda cha bia ili watu walewe muda wote waache kufanya kazi.Wakati huo huo tunahubiri sera ya KILIMO KWANZA.Hata kujua hili ni cheap popularity? Tuamke ndugu zangu.
 
Duh Tanzania hata viwanda vya kubangua Korosho vinatushinda?

Kweli siasa za Tanzania ni mumbo jambo tu basi!
 
Orodha ni ndefu:
1. Kiwanda Nguo Arusha (KILTEX) Gereji la Classic Tours
2. Kiwanda cha Magunia Moshi (Tawi la Chuo Kikuu cha Mwenge)
3. General Tyre Arusha
4. Kiwanda cha Ngozi Moshi
6. Canvas Morogoro
7. Hoteli za TAHI
8. MUTEX
10 MWATEX - N.K.
 
Na RTC ziko wapi ndugu zangu?? Nakumbuka tulikuwa tunaenda viwanda vya serikali (Mashirika ya Umma au SU) kwenye ziara za kishule, tulienda Magunia Moshi, General Tyre Arusha, Kilimanjaro Machine Tools, TPC, Mtibwa Sugar Estates (nilifanyia field yangu hapa) nk, viko wapi??

SU meanz
SERIKALI UMENISAHAU
 
Naibu Waziri Fedha akijibu swali Bungeni leo,alisifia mafanikio ya Ubinafsishaji.Mh. Zito akauliza swali la nyongeza na kusema anasikitishwa na Serikali kusifia mafanikio ya ubinafsishaji na kutoa mifano kuwa 1980s, viwanda vya korosho vilikuwa 12 leo 1 tu chafanya kazi.

Akaongeza Mwatex, Mbeyatex, Sunguratex viko wapi leo. Mkulo kajibu ati swali la Zito ni jipya (kwa kuwa kataja Textile Industry)! Spika Makinda akamgeuzia kibao Mkulo kuwa swali la Zito ni valid lakini hamshinikiza atoe jibu!

Kanuni ko vipi?

Mkullo anajua kuwa Sera ya Ubinafsishaji haikuwa, wala hata sasa haina Tija, kwa hiyo haina Mafanikio. Zitto alitamani Serikali ikiri hivyo! Kiserikali Mkullo alikuwa lazima ajaribu kulikwepa swali hilo, ila hakua na mbinu nzuri, ndo maana Spika akambana! Asingeweza kulijibu swali lile kwa ufasaha, kwani ni ukweli usiopingika kuwa sera nzima ya ubinafsishaji ililenga kuyagawana mashirika yaliyokuwa tayari na tija kubwa ili waasisi wa sera hiyo wajinufaishe kwa kuyamiliki wao wenyewe! Mfano Sigara, NBC, Madini, Nishati nk. Ndo maana mashirika kama AN-BEN yaliundwa kujimilikisha uzalishaji wa umeme! Taasaisi nyingine ambazo zilikuwa bado Tegemezi, kwa maana ya kutegemea Ruzuku ili mambo yaende ndo hizo zikaachwa zife kabisa kabisa!
 
chezea zitto kabwe nyie,kijana makini huyu,big up my next prezdaa

Naheshimu maoni yako binafsi, kati ya watu nawadharau ni yeye. Hakuna mtu ambaye anaweza kuwa pande mbili at a time. Jaribu kufikiria bila ushabiki utaona na swali lenyewe ni obvious sana hakihitaji hata kutumia akili sana
 
Ni sifa gani inatumika kuwapa watu nafasi za kuwa mawaziri? Kuna wengine hawastahili kabisa kuwemo ndani ya baraza la mawaziri. Uchumi umeporomoka ndani ya miaka hii ya huyu bwana kuwa waziri lakini bado yumo tu. What point does he want to prove?

Sifa mojawapo ni kuwa Kilaza! Nyingine ni kuwa swahiba!
 
Yah! bwa mdogo jepesi yupo right bse mpk sasa ukiachia hizo textiles to be absolutely perish kwenye korosho ndio kabisa kwa mfano juzi watu watandahimba walifunga barabara kuishindikiza serikali wapate malipo ya pili*(bonus) na korosho sasa hivi zinazovuna hapa kwetu nchini nikwaajili ya export katika viwanda vya nje wakati korosho ni lulu kuanzia bibo,ganda lake mpk mafuta yatokanayo na maganda........dah! cjui tumekwama wa[pi watanzania we have everything but we are absolutely poor......!
Waktabahuuu!
 
Mi naona ni busara ya hali ya juu kaionyesha waziri,
Huwezi kujibu hata kama hujui, pale ni bungeni na unahitaji kuwa na evidence ya majibu unayotoa.
Ni sahihi kwa waziri kuomba swali lile liwe katika maswali ya msingi ili alifanyie kazi sijaona tatizo.

Ila zitto ni mwiba hata muasisi analijua hilo.
Zitto for presidency 2015.
 
Mkullo ame-over stay kwenye hiyo nafasi hafai.

Hii nafasi atafutiwe mtu ambaye si mbunge kabisa..au mbunge wa kuteuliwa (expert)
 
Si walishazoea tabia za kasuku,wanadhani bungeni kumejaa mazuzu,acha waaibike na 2015 tunawapiga chini wote.
 
Back
Top Bottom