Bungeni: Zitto aigalagaza Serikali, Spika ashindilia msumari wa moto!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Naibu Waziri Fedha akijibu swali Bungeni leo,alisifia mafanikio ya Ubinafsishaji.Mh. Zito akauliza swali la nyongeza na kusema anasikitishwa na Serikali kusifia mafanikio ya ubinafsishaji na kutoa mifano kuwa 1980s, viwanda vya korosho vilikuwa 12 leo 1 tu chafanya kazi.

Akaongeza Mwatex, Mbeyatex, Sunguratex viko wapi leo. Mkulo kajibu ati swali la Zito ni jipya (kwa kuwa kataja Textile Industry)! Spika Makinda akamgeuzia kibao Mkulo kuwa swali la Zito ni valid lakini hamshinikiza atoe jibu!

Kanuni ko vipi?
 
Wana jf leo spika wa bunge amenifurahisha sana hasa baada ya kumweleza waziwazi mh. Mkulo kuwa hajajibu swali aliloulizwa na mh. Zitto. Kwa ufupi ni kuwa mh. Zitto aliitaka serikali ieleze mafanikio ya ubinafsishaji iwapo miaka ya 1980 kulikuwa na viwanda 10 vya kubangua korosho na mpaka leo kimebaki kimoja; akauliza ni mafanikio gani hayo ambayo serikali inajivunia? Mh. Mkulo akataka swali hilo liletwe kama swali la msingi na sio la nyongeza, lakini Mh. Spika akamwambia mbele ya wabunge kuwa hajajibu swali. Jamani wanawake wakiwezeshwa kumbe wanaweza sana!
 
YAELEKEA ILEKAULI MBIU YA "ZINDUKA" IMEMKUMBA MH. SPIKA :heh::heh::heh:
 
Huyu mkulo anadharau sana..nakumbuka bunge lilopita aliitwa na spika kujibu swali hukusimama kuashiari kuwa amegoma..huyu jamaa amelewa na pesa zetu pale wizarani.
 
Mkulo anapwaya sana! Spika alikuwa na fursa ya kumpasha Mkulo lakini anazuiwa na Party coccous. Nimeangalia kwa makini mchezo wa Mkulo alipokuwa anajibu swali as if ana ubia na serikali. Ameniboa sana~!
 
Viwanda vingi baada ya kuuzwa hoo wawekezaji uchwara wamevigeuza maghala ya bidhaa hafifu kutoka nje shame on u mkulo.
 
Kuna wale wanaoamini kuwa mawazo na sera mbadala zinaweza kutokea kwa walioko ndani ya Chama, wakisikiliza majibu ya huyu kilaza watajua kuwa wanajidanganya. Hakuna lolote zaidi ya kuoneana haya, kulindana, na kufikiri kuwa wananchi ni mbumbumbu!
 
Haya mambo hayatajificha kamwe! Madudu yao wanadhani waTZ bado wataendelea kupokea uongo wao!!

Shame on them!!
 
Huyu mkulo anadharau sana..nakumbuka bunge lilopita aliitwa na spika kujibu swali hukusimama kuashiari kuwa amegoma..huyu jamaa amelewa na pesa zetu pale wizarani.

kumbe ana jeuri eeeh......! Anamgomea hadi spika? Hii hatari kwelikweli.......!
 
haya ndiyo mafanikio ya chama tawala, tunaongozwa na mawaziri wavivu wa kufikiri na waliojaa dharau na kiburi, shame to mkulo
 
Back
Top Bottom