Wewe umesema. Nitfute baadaye nikupe pipi.Hakuna kukaa.nasema mawazo haya ni potofu.cuf wana ndoa na ccm,nccr kadhalika,tlp ndo usiseme.udp mnajua.chadema nenda mwenyewe.jenga upinzani hadi kieleweke.nafurahi wapinzani feki wameonekana mapema.chadema mwendo mdundo.
Kwa mtazamo wangu nimeyapokea matokeo ya uspika ( makinda kura 265 na marando kura 53) kama kuna upizani ndani ya kambi ya upinzani ambao ulianza wakati wanachagua kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, nimesikia cuf nao watachagua kiongozi wao licha ya chadema kumchagua mbowe kutokana na kutimiza masharti kwa kanuni za bunge, huu ni mpasuko ndani ya kambi ya upizani na haswa huletwa na cuf, niwaombe wabunge wa upinzani kukaa ili waweze kutoa hizi tofauti zao, maana kama wanataka kuibomoa ccm lazima wawe kitu kimoja.
Na wale tisa (9) ambao kura zao waliziharibu hao umewaweka wapi? kwamba ni popo hawajulikani wako upande upi?
Source!? Ondoa spin zako hapa we mjinga. Nenda kule ccm ukawambie ujinga wako huu.Yaliyotokea ni haya hapa:
Kutoka ndani ya uvungu wao...
Walikaa Chadema na CUF ili waone wataingiaje Bungeni. Kabla ya Uchaguzi wa Spika, Hamad Rashid alitaka kugombea Uspika, Chadema wakamwambia hapana wacha Agombee huyu Mwanasheria, wewe utarudi katika kambi ya upinzani kwa cheo chako kile cha awali, na kwa kufanya hivyo tutagawana madaraka. Hamad akawakubalia na kuondoa azma yake ya kugombea U-Spika alipofanya hivyo, Zito akaibuka na kusema Wataunda kambi Chadema peke yake bila kushirikisha vyama vingine. hilo nalo. Hapo ndipo Marando alipozikosa kura ambazo zingemvusha kwenye Uspika. Na hii imefanyika kutokana na ufinyu wa fikra (kama sio viongozi waandamizi wa Chadema kupewa chochote toka CCM) wakidhani kwamba umaarufu unatokana na kuongoza kambi ya upinzani bungeni bila kuwa na ushirikiano kutoka vyama vingine. Walichokisahau Chadema ni kuwa CUF walijaribu kutoshirikisha vyama vingine awali na kisha wakajirekebisha, na hapo wasiomjua Slaa ndipo walipomtambua. Ila kwa kwa hili la ubinafsi wa CHADEMA wameumaliza UPINZANI Tanzania. Tutafute kaburi tuuzike...
Tusubiri kuundwa kwa chama kipya kisicho na damu ya U-CCM-CCM.:sad:
Nawasilisha.
Jamani kumbukeni kwamba hata Zanzibar CUF waliingia kwenye makubaliano baina yao na CCM. Na hawakushirikisha chama chochote kingine.
Nawashangaa ambao mnaamini kuwa CUF wanaweza kuwa na ushirikiano na Chadema ktk bunge la JMT wakati huo huo kuwa na ushirikiano na CCM katika baraza la wawakilishi Zanzibar! Only a foul will buy this idea. Kumbukeni CCM ni ile ile ya Zanzibar na Bara na vile vile kwa CUF.
Kama mlifuatilia kwa makini mwenendo wa Prof. Lipumba wakati wa kampeni, kutangazwa matokeo na kisha kuapishwa kwa Rais wa JMT ni wazi alikuwa against Chadema zaidi kuliko ambavyo alikuwa against CCM. Kifupi alikuwa akimpigia kampeni JK. Na hii yote ilitokana na kutotaka kuharibu ndoa yao (ulaji wao) na CCM kule Zanzibar.
In short, hizo ndo hulka za viongozi wa bara la Afrika. Wamejaa ubinafsi na uzandiki.
Maalim Seif ameshasahau watu waliomwaga damu na maelfu kukimbilia nchi zingine kama wakimbizi!!
Baada ya CUF kuungana na CCM kuunda serikali ya mseto, ni vizuri watanzania wote waelemishwe kuwa chama pekee cha upinzania kilichobaki Tanzania ni Chadema. Kulikuwa na nafasi ya vyama vingine kama TLP, NCCR navyo kuwa vyama vya upinzani. Lakini baada ya TLP, NCCR na vyama vingine kuungana na CUF bungeni inamaanisha kuwa CUF, TLP, NCCR vyote vimeungana na CCM. Hivyo, kama ambavyo tumeendelea kutoa elimu ya uraia kwa watanzania, tuendelee kuwafahamisha na waelewe kuwa chama cha upinzani na ambacho kinatetea masilahi ya Watanzania nchini kwetu ni Chadema pekee. Ujumbe huu na uenee nchi nzima sasa.
Yaliyotokea ni haya hapa: